Uongo mbaya sana wakati mwingine

ndalibanza

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
403
379
Jamani mkuje na mawazo ya kuokoa jahazi huku, nipo na jamaa yangu grosary flan hivi! Alikuja mitaa hii kumtembelea manzi wake, kwa bahati mbaya hakumkuta akaamua kujisogeza hapo grosary kupata moja moto moja baridi,, akiwa hapo mara akaingia mtoto mmoja mzuri sana yan huyo demu wake anaweza ingia mara 10 hivi, uzalendo ukamshinda akaamua kuomba namba wakaanza kuchart mdogo mdogo!!

Wakati huo huo kulikuwa na mapaka kama matatu hivi yana kamua mvinyo kwa pembeni huku macho yote kwetu, mara jamaa akapigiwa simu na manzi wake akamuuliza yupo Wapi kwani alikuta missed calls zake, jamaa akadanganya yupo home kwake a naangalia sinema zetu.

Tumekaa kama masaa mawili hivi mara manzi wake huyu hapa nae alikuwa anakuja kupoza koo! Kizaa zaa kikaanzia hapo kwann amemdanganya?? Akatumia mbinu za kivita kumdanganya akaeleweka, na shemeji akajiunga nasi tukaanza kuburudika pamoja, aisee kumbe yale manyau yalikuwa yanausoma mchezo mzima si yakamtonya shem kuwa jamaa amechukua namba ya yule dada mkali!!

Sokomoko kikaanzia hapo shem katoka analia ovyo na kubwatuka kuwa anasalitiwa hadharani na jamaa amevurugwa mana hataki kuharibu na huyu mrembo mpya!!

Kifupi anawataka wote amebaki katumbua macho hapa kama kama gari mpya inayowasha taa ya check engine!! 😅 😅 😅 😅
 
Mbona kama ni wewe unaelezea kwa mgongo wa jamaa yako 😂 ila sio mbaya

Uongo unasaidia na muda mwingine hausaidii ukidakwa red handed
 
Back
Top Bottom