Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,798
- 71,218
Hakika Watanzania sasa tunasomeshwa namba na nashangaa wale wanaounga mkono kila kinachofanywa na serikali. Kufikia mwaka jana ili vijana wetu wasome vyuo vikuu maombi yalikuwa yanafanywa sehemu moja tuu nayo ni TCU na mzazi ilikuwa unalipa shs 50,000/ pekee ukisubiri nafasi ya kusoma kijana atapangiwa wapi.
Sasa hivi serikali inayojinasibu kujali raia wake imesema kila mtu ata apply chuo atakacho mwenyewe, sio jambo baya lakini sasa wamelifikiria hili jambo la kulipa wakati wa maombi wakati mtu hana hakika ya kupata nafasi katika chuo anachoomba?
Maana ili kujipa nafasi ya kuweza kupata chuo mwanafunzi atawajibika kuomba vyuo vingi kadiri awezavyo na hapo hapo lazima alipe application fee kila chuo kwani hana hakika kipi atapata.
Kwa hili wazazi tulikuwa tunalipa 50000/ sasa tunaweza kujikuta tunalipa hata milioni, jee huku ndio kumjali mwanachi? Kwa nini malipo yasifanywe kama admission fee kwa wale watakao chaguliwa tuu?
Haya mambo ya kutekeleza mawazo ya mtu mmoja anayokurupuka nayo na kuzoza majukwaani yanatuletea shida kubwa sana na kufanya maisha ya Watanzania kuwa ya misukosuko.