Kwako Ummy Mwalimu na Wizara ya Afya, Zindukeni, tunapoteza wataalamu na utaalamu

HustlerD

Senior Member
May 15, 2021
131
425
Wakuu nawasalimu nyote,

Kwanza nipende kuwapongeza Wizara ya Afya kwa namna wanavyoendelea kuboresha huduma za afya katika nchi hii, kwakweli wanajitahidi sana, hakika tumepiga hatua

Sasa tunapozungumzia uboreshaji wa huduma za Afya ni sanjari na kuongeza wataalamu wa afya wa kutosha hasa kwa kada ambazo hatukua nazo nchini ili kuendana na kasi ya huduma kwa ulimwengu wa leo

mimi leo nitazungumzia suala la Wizara ya Afya kutoa ufadhili (Sponsorship) kwa wataalamu wa afya hasa Doctors(watumishi wa umma) kwa kozi ambazo hazipatikani nchini kwa ngazi ya Masters na kuendelea

Nikiwa miongoni mwa zile timu za wadau wanaoshauri na kufuatilia mwenendo wa wataalamu wetu wanaoenda kimasomo nchi za nje hasa kwa level ya masters, kurudi kwao nchini, na nafasi yao ya kuleta mabadiliko chanya hasa kwa utaalamu ambao hatukua nao, naomba leo niwatonye hili,

Vijana wengi wamekua wakijitahidi kuomba kozi za kipaumbele toka wizara ya Afya ambazo haziko nchini wakitegemea kupata ufadhili wa Wizara ya Afya kama wizara wanavyowasihi, yaani ninamaanisha mtaalamu wa Afya anatafuta kozi ya masters na chuo(kama inavyotakiwa), anapambana kutuma maombi na procedures nyingine mpaka anapata barua ya admission kwa gharama zake, wengine mpaka hulipia registration Fees kwenye vyuo hivyo wakati wakisubiri Wizara itoe ufadhili wao (maana vyuo vingi huko duniani intake zao hua ni September tofauti na hapa kwetu ambapo intake za Afya hua ni October pengine mpaka November, )hivyo kushika nafasi asije kosa chuo, na wengine kuanza masomo yao huku wakisubiri ufadhili (ambao majina ya waliopata hutoka November nadhani)

Cha ajabu utakuta kozi kipaumbele ya Wizara ya Afya mtu kakosa ufadhili na ukiangalia kwenye waliopata unakuta wakati mwingine hakuna au yupo mmoja tu, sasa unajiuliza nini maana ya kozi hii kupewa kipaumbele ikiwa hata walioomba huko nje na wakapata hawapewi ufadhili, maana lengo ni kutengeneza wataalamu kwa kila nyanja, au labda mheshimiwa Waziri Ummy ufadhili huo ni wa kujuana..?

Sasa cha kusikitisha tulichokiona huko nje kwenye survey kwenye vyuo saba (Africa vitatu na huko kwingine vinne) baadhi ya wataalamu wetu kwa kua tayar ameshatumia gharama nyingi kupata admission na pengine mpaka registration kalipia, huamua kujilipua na kwenda hivyo hivyo kwa gharama zao,

matokeo yake wengi huishi maisha magumu huko ya kufanya kazi za muda ili kumudu gharama za maisha na wengine hawarudi kwenye taasisi zao pindi wakimaliza masomo yao, kuishia kuajiriwa kwenye mashirika ya kimataifa na kurudi hapa kama wataalamu wa kimataifa(mifano ipo) wakati tulikua nao wangeweza kurudi na wakawatrain wengine wengi zaidi, hivyo kama nchi kuzidi kupoteza wataalamu,

Juzi hapa Naibu Waziri wa Afya Dr Mollel ametoa Tangazo la ufadhili, hivyo kama wadau wa maendeleo ya nchi hii tunaomba liangalieni suala hili kwa upana wake

Kwakua ndiyo muda wa kuomba huo ufadhili, basi pindi majina na kozi za waliopata ufadhili yakitoka, nami nitarejea hapa kuja kutoa mrejesho wa idadi ya waliopata ufadhili kwa kozi hizo za kipaumbele zisizotolewa nchini,

Na tumejaribu kupata baadhi ya wataalamu walioomba kati ya kozi hizo kutoka hospitali na taasisi za afya za umma, kwahiyo tunasubiri tuone Wizara wamejipangaje siyo kutangaza na kusifia tu mara Mama katoa ufadhili sijui wa bilioni Tisa kumbe kila siku ni kusomesha wataalamu kwa masuala yale yale hasa kwa kozi zilizopo nchini, na kila yakitokea majanga mapya tunalazimika kusaidiwa na mashirika ya kimataifa kwa vitu ambavyo tungetumia wataalam wetu wenyewe tuliowasomesha huko nje

Mfano, ni majuzi tu hapa Marburg, Covid na hata Ebola zilitesa sana watu, kazi yetu ni kuomba usaidiz wa wataalamu wa kimataifa, inamaana hatuwezi kusomesha wataalamu kozi za magonjwa ya kuambukiza, pamoja na wanaoweza kuvumbua na kutengeneza hata Chanjo za baadhi ya magonjwa..? na hizo kozi zipo kwenye kipaumbele lakin hatuoni watu wakilipiwa kwenda kusoma, anakomolewa nani, ndiyo maana awamu hii tutakuja na ushahidi wa walioomba ili zisije longo longo mara wataalamu hawaombi, INASIKITISHA

WIZARA BADILIKENI

Ninaambatanisha na list ya kozi hizo za kipaumbele ambazo hazipatikani hapa nchini kutoka wizara ya Afya kwa mwaka huu hapa chini,


Screenshot_20230911_123529_WPS%20Office.jpg
Screenshot_20230911_114210_WPS%20Office.jpg
 
Sijawahi kumuelewa huyo mama, ila ndo basi tu anajua kucheza na media na kujieleza kwingi.
 
Back
Top Bottom