Uonezi katika udahili 2017, Maombi chuoni na kila chuo unalipa

Uonezi katika udahili 2017, Maombi chuoni na kila chuo unalipa

1ca1ab281bc6ebdf32c32f317d267f8c.jpg

Haya ndio tulikuwa tunasema na wamesikia.
 
Nadhani bango lako limeaaidia kwa kiasi kikubwa, Inawezekana katika hili walisahau.
Mkuu nilishasema hapo awali kuwa kuna wakati tunapaswa kuwa VOICE OF VOICELESS, ajabu vijana wa kula kulala wakashambulia bila kutafakari maisha ya wale watanzania wenye kipato cha chini kabisa.
Kweli mtu anatamka eti "kama hela huna ni uzembe wako acha kusoma" ! Lazima kwa wenye akili unajua huyo ni mtu wa aina gani.
 
msipotoshe sio kila Chuo 50000/= kuna 20,000/=kuna 25,000/= kuna 30,000/=

sema serikali imeamua
1.kufanya Biashara
2.kupunguza Idadi ya watakaodahiliwa kwa kukosa nafasi kisa baadhi ya vyuo kuzuia kutoa course na vingine kufungwa kabisa
 
Hakika Watanzania sasa tunasomeshwa namba na nashangaa wale wanaounga mkono kila kinachofanywa na serikali. Kufikia mwaka jana ili vijana wetu wasome vyuo vikuu maombi yalikuwa yanafanywa sehemu moja tuu nayo ni TCU na mzazi ilikuwa unalipa shs 50,000/ pekee ukisubiri nafasi ya kusoma kijana atapangiwa wapi.

Sasa hivi serikali inayojinasibu kujali raia wake imesema kila mtu ata apply chuo atakacho mwenyewe, sio jambo baya lakini sasa wamelifikiria hili jambo la kulipa wakati wa maombi wakati mtu hana hakika ya kupata nafasi katika chuo anachoomba?

Maana ili kujipa nafasi ya kuweza kupata chuo mwanafunzi atawajibika kuomba vyuo vingi kadiri awezavyo na hapo hapo lazima alipe application fee kila chuo kwani hana hakika kipi atapata.

Kwa hili wazazi tulikuwa tunalipa 50000/ sasa tunaweza kujikuta tunalipa hata milioni, jee huku ndio kumjali mwanachi? Kwa nini malipo yasifanywe kama admission fee kwa wale watakao chaguliwa tuu?

Haya mambo ya kutekeleza mawazo ya mtu mmoja anayokurupuka nayo na kuzoza majukwaani yanatuletea shida kubwa sana na kufanya maisha ya Watanzania kuwa ya misukosuko.
Nijuavyo Mimi ni tshs 10,000/ si 50,000/

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale amabo walishalipa 30,000 inakuwaje...maana sasa ni 10,000... [HASHTAG]#naombamuongozo[/HASHTAG]
 
Watanzania bwana huwa hawakosi cha kulalamika hata gharama zingekuwa chini ya hapo watatafuta tu dosari zingine zisizo na macho wala miguu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unataka kusema vyuo vyote una apply online kisha,admission online kila kitu online wewe unaenda tu. Mkuu labda ni mpya hiyo, lakini angalau tunakubaliana kuwa gharama zitaongezeka

Mkuu vp? Kuna chuo ambacho ulipeleka maombi Physically as u think before?!
 
Back
Top Bottom