Uonezi katika udahili 2017, Maombi chuoni na kila chuo unalipa

Uonezi katika udahili 2017, Maombi chuoni na kila chuo unalipa

Hakika Watanzania sasa tunasomeshwa namba na nashangaa wale wanaounga mkono kila kinachofanywa na serikali. Kufikia mwaka jana ili vijana wetu wasome vyuo vikuu maombi yalikuwa yanafanywa sehemu moja tuu nayo ni TCU na mzazi ilikuwa unalipa shs 50,000/ pekee ukisubiri nafasi ya kusoma kijana atapangiwa wapi.

Sasa hivi serikali inayojinasibu kujali raia wake imesema kila mtu ata apply chuo atakacho mwenyewe, sio jambo baya lakini sasa wamelifikiria hili jambo la kulipa wakati wa maombi wakati mtu hana hakika ya kupata nafasi katika chuo anachoomba?

Maana ili kujipa nafasi ya kuweza kupata chuo mwanafunzi atawajibika kuomba vyuo vingi kadiri awezavyo na hapo hapo lazima alipe application fee kila chuo kwani hana hakika kipi atapata.

Kwa hili wazazi tulikuwa tunalipa 50000/ sasa tunaweza kujikuta tunalipa hata milioni, jee huku ndio kumjali mwanachi? Kwa nini malipo yasifanywe kama admission fee kwa wale watakao chaguliwa tuu?

Haya mambo ya kutekeleza mawazo ya mtu mmoja anayokurupuka nayo na kuzoza majukwaani yanatuletea shida kubwa sana na kufanya maisha ya Watanzania kuwa ya misukosuko.
wakati anaongea mkulu udsm pale c mlishangilia?
tulia dawa iwaingie
 
Unayajua maisha ya Mtanzania wa kawaida au unazoza tuu? Kuna sababu gani kulipa 50000 kwa kila chuo utakachoomba? Kwa nini hiyo hela asitozwe mwanafunzi kama admission fee pale atakapokuwa kachaguliwa?

Ndiyo mkome kurohoja bila facts!! Wenyewe , mlikuwa kila siku kwenye majukwaa na mitandao ya kijamii mkiomba TCU iondolewe ama msifanye udahili kupitia CAS ya TCU hayo hamkuyawaza!!?

Sikia, hata ulaya, USA, Asia unalipia application fees kulingana na vyuo unavyohitaji na kila chuo unalipia. Na hakuna huo ujinga wa eti ulipie baada ya kuchaguliwa, unalipa unasubiria kama hujakidhi vigezo application fee yako ndiyo kwa heri hiyo.

Rais, Dr Magufuli, nampongeza sana , maana aliwasikiliza ninyi wenyewe na kuwapa mnachokitaka. Basi bila hiyana, akainua kalamu akaandika na akatamka basi mmekipata mlichokitafuta na ndivyo mlivyotaka.
 
Kama siaminiamini! Ni kweli walioapply kwa mtindo mpya wametozwa sh.elfu 50 kwa kila chuo????
Leo hii kuna vyuo sivitaji.Ila cha kwanza ni 30000/= Tshs,cha pili nikaangalia ni 50000/=Tshs.Aliyeandika mada labda kaka hajaeleweka ila ukiwa una apply ndio utaelewa kisemwacho.Acha tu.Tusishabikie shabikie tu.
 
Tatizo ni kulalamika kwa watanzania badala ya kuonesha njia mbadala.
Zamani, ulikuwa unaomba vyuo tofauti tofauti na unalipia application fee, watu wakasema tuwe na CAS ndipo TCU ikaanzishwa.

Hata miaka 10 haijaiisha, ninyi ao hao , mkaanza oooh oooh, TCU mara sijui hawako makini , mkatoa tuhuma bila kuonesha njia ya kusahihisha makosa au udhaifu wa TCU.

Wengine, wakamwambia hadi rais, aiondoe TCU.

Basi, rais , ameona isiwe nongwa, tatizo ni CAS ya TCU mkajibu ndiyooooooo, basi, akauliza mnataka iweje, mkajibu wenyewe, tuombe vyuoni wenyewe direct.

Tena, hata mwaka haujaiisha tangia mjirohojeshe hivyo, mmeishaanza oooh, gharama, oooh usafiri, oooh, kama kozi inahitaji watu 100 , tukaomba 300, inakuwaje!?

Ndiyo mkome. Tena, naomba vyuo viwakomeshe kabisa kwenye cut off points na idadi ya wanafunzi kwa kila faculty/ program ndiyo mkome kulialia bila sababu.
 
Hakika Watanzania sasa tunasomeshwa namba na nashangaa wale wanaounga mkono kila kinachofanywa na serikali. Kufikia mwaka jana ili vijana wetu wasome vyuo vikuu maombi yalikuwa yanafanywa sehemu moja tuu nayo ni TCU na mzazi ilikuwa unalipa shs 50,000/ pekee ukisubiri nafasi ya kusoma kijana atapangiwa wapi.

Sasa hivi serikali inayojinasibu kujali raia wake imesema kila mtu ata apply chuo atakacho mwenyewe, sio jambo baya lakini sasa wamelifikiria hili jambo la kulipa wakati wa maombi wakati mtu hana hakika ya kupata nafasi katika chuo anachoomba?

Maana ili kujipa nafasi ya kuweza kupata chuo mwanafunzi atawajibika kuomba vyuo vingi kadiri awezavyo na hapo hapo lazima alipe application fee kila chuo kwani hana hakika kipi atapata.

Kwa hili wazazi tulikuwa tunalipa 50000/ sasa tunaweza kujikuta tunalipa hata milioni, jee huku ndio kumjali mwanachi? Kwa nini malipo yasifanywe kama admission fee kwa wale watakao chaguliwa tuu?

Haya mambo ya kutekeleza mawazo ya mtu mmoja anayokurupuka nayo na kuzoza majukwaani yanatuletea shida kubwa sana na kufanya maisha ya Watanzania kuwa ya misukosuko.

kwani shida iko wapi... kama umepiga fresh advance (form 6) una mbili yako ya uhakika au kijiti chako kizuri ya nin uhangaike na mivyuo vingi vingi eti kisa ntakosa nafasi... WTF ww km unakomaa na UDOM chagua zako UDOM tulia... mara sio unataka SUA hapo hapo unataka UD mara ARDHI ndo utadondosha hata 2K
cha muhim ni kujua unaenda kusoma course ipi UNI, km unataka health faculties jua una mbili yako tamu au kijiti kizuri tena chenyewe kile, asa mtu ana three hapo hapo anataka health faculties unaangukia pua ni bora uchague education UDOM au MUCE au DUCE utulie kuliko kung'ang'ana na ushindani...
wenzako wametia misuli iliyo_aim UD, MUHAS ww unapiga msuli af una_aim kwmb nikikosa huko ntaenda hata education,,, bro/sis subiria embe chini ya mnazi
 
Ni kweli, zamani ilikuwa una apply popote ulipo ilimradi unaweza kupata huduma ya mtandao kwa gharama ile ile elfu 50 na unaweza kuomba hata vyuo vitano.

Lakini sasa inakubidi kila chuo ulipe hiyo elfu 50, na kutokana na haki hakisi inakubidi ufike mahala husika. Sasa mfano mtu yuko kigoma tusema angalau aombe vyuo vinne viwili tusema Dar es salaam, kingine Mwanza na kingine Songea, ina maana gharama za ku apply ni laki 2. Bado gharama za usafiri kufika maeneo husika na gharama za malazi kwa siku atakazo kuwepo maeneo husika. Hizi gharama ni kubwa. Matokeo yake mtu anaweza aka apply sehemu moja au mbili na kuongeza uwezekano wa kukosa nafasi.

TCU hawakuwa wakiwapangia tu wanavyotaka, bali waliangalia wenyewe vigezo kwanza ndio wapate nafasi katika maeneo husika. Hivyo hivyo ukikosa basi wanaenda sehemu ya pili uliyoomba mpaka utapata inayokufit. Sasa hivi kuna uwezekano wa mwenye sifa zaidi kukosa sehemu akapata mwingine mwenye sifa ya chini au watu wengi kujazana sehemu moja na wengine wakakosa wakati kuna sehemu watu wachache. Chuo hakiwezi kudahili wachache kiseme kisubiri wenye sifa zaidi labda wanakuja bali watabeba tu kwani wengine ni biashara

Waangalie utaratibu mzuri wawasaidie watoto maskini, hivi walivyofanya sasa inawaumiza na italeta kelele nyingi
Maombi yanafanyika kwa njia ya mtandao,sasa gharama unazopiga za kwenda mahala husika penye chuo zinatoka wapi?
Nakubaliana na wewe kwa namna moja ama nyingine itaongeza gharama kwa wanafunzi lakini haitofikia kiasi ulichokipigia mahesabu.
 
Acha upumbavu watu wanaongelea ghalama ww unaleta zako

Sent using Jamii Forums mobile app

Tatizo lako ni elimu , elimu , elimu!!

Let me take you into facts, we had CAS in TCU some of you claimed that TCU its not effective enough then, mkaomba kuwa wanafunzi watume maombi wao wenyewe wanakopenda kusoma.

Basi, mkapewa mnachohitaji leo hii hata miaka 10 haijaisha mnaanza kujitoa ufahamu!

Any way, sometimes its good to teach a fool in a hard way.
 
wazazi tuna kazi jamani.... alietoa order ya kufuta TCU kufanya admissions naona alisahau kutoa order ya kupunguza admision fee

Haaaa haaaaaa teeeh.
Pole sana, wala hakuna aliyetoa order ya kuondoa admission kupitia CAS ya TCU, bali yalikuwa ni maombi ya wananzengo wenyewe basi, rais akauliza mnahitaji nini!? Wanasema TCU isidahili bali wanafunzi waombe vyuo wanavyooenda mwenyewe.

Rais, akauliza jingine, wakasema hakuna, Baba. Basi, kesho yake watu wakapewa walichoomba.

Any way, hii itatoa funzo la kufanya upembuzi yakinifu kabla ya kuomba jambo Fulani.
 
Aliyekataa mfumo ulokuwapo si ni baba Bashite!! [emoji16] [emoji16] [emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwanza, Simfahamu uliyemtaja kwenye comment yako.

Ila ninachojua wanazengo ndiyo walilalamika kuwa TCU inawapangia watu vyuo wasivyovipenda pamoja na kozi.

Basi, ndiyo mmepewa nafasi ya kuomba vyuo mnavyovipenda wenyewe.
Tena, mnaanza kuleta porojo.

Aiseeeh, acheni unaaaa,
 
Watakuita Mchochezi

Sasa sijui TCU ilianzishwa yanini.

Wizi mtupu tu halafu eti wanasema serikali inawajali wananchi.

Wezi watupu hawa
 
Haya mambo ya kusema "serikali inayojali wananchi" ni upuuzi mtupu wakati inawazalishia ugumu wa kimya kimya kila siku.
Kwa ujumla watanzania hawajui walitakalo, kila jambo ni kulalamika tu. Wakati admission Centre ilikuwa TCU mlilalamika kuwa wanapelekwa kwenye vyuo msivyovichagua, na sasa mpeleke maombi moja kwa moja chuoni mnalalamika. Kwani hamkujua kwa kila njia zina changamoto zake. Hebu muwe mnatafakari kwanza kabla ya kulalamika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hapa wamerudisha system ya zaman ambapo mtu unaomba vyuo vingi na unachaguliwa ambapo umefit hata sehem mbili na ww unamade a choice kwa kwenda,,,sema now iyo pesa ndo tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni kulalamika kwa watanzania badala ya kuonesha njia mbadala.
Zamani, ulikuwa unaomba vyuo tofauti tofauti na unalipia application fee, watu wakasema tuwe na CAS ndipo TCU ikaanzishwa.

Hata miaka 10 haijaiisha, ninyi ao hao , mkaanza oooh oooh, TCU mara sijui hawako makini , mkatoa tuhuma bila kuonesha njia ya kusahihisha makosa au udhaifu wa TCU.

Wengine, wakamwambia hadi rais, aiondoe TCU.

Basi, rais , ameona isiwe nongwa, tatizo ni CAS ya TCU mkajibu ndiyooooooo, basi, akauliza mnataka iweje, mkajibu wenyewe, tuombe vyuoni wenyewe direct.

Tena, hata mwaka haujaiisha tangia mjirohojeshe hivyo, mmeishaanza oooh, gharama, oooh usafiri, oooh, kama kozi inahitaji watu 100 , tukaomba 300, inakuwaje!?

Ndiyo mkome. Tena, naomba vyuo viwakomeshe kabisa kwenye cut off points na idadi ya wanafunzi kwa kila faculty/ program ndiyo mkome kulialia bila sababu.
Kujadiliana na MTU ambaye hajitambui ni shida. Sikia kijana, serikali haifanyi kazi zake kwa kukomoa RAIA wake kwa vile eti waliwahi kulalamika. Jee walio lalamika ni wote?mbona Leo kuna wanaolalamika Jpm ni dikteta na hajajiuzulu na kusema kuna watu wanalalamika?
Ni wajibu wa serikali kutafuta unafuu kwa watu wake.
Mfumo huu mpya ni mzuri, lakini kuna haja gani kuweka gharama kubwa kwa maombi ambayo hayana uhakika wa kupata?
Tuwazungumzie wale wazazi wanao ishi chini ya dola moja kwa siku sio sie ambao tuna akiba kwenye mabenki hata hatujui ni ngapi. Huo ndii uzalendo
 
kwani shida iko wapi... kama umepiga fresh advance (form 6) una mbili yako ya uhakika au kijiti chako kizuri ya nin uhangaike na mivyuo vingi vingi eti kisa ntakosa nafasi... WTF ww km unakomaa na UDOM chagua zako UDOM tulia... mara sio unataka SUA hapo hapo unataka UD mara ARDHI ndo utadondosha hata 2K
cha muhim ni kujua unaenda kusoma course ipi UNI, km unataka health faculties jua una mbili yako tamu au kijiti kizuri tena chenyewe kile, asa mtu ana three hapo hapo anataka health faculties unaangukia pua ni bora uchague education UDOM au MUCE au DUCE utulie kuliko kung'ang'ana na ushindani...
wenzako wametia misuli iliyo_aim UD, MUHAS ww unapiga msuli af una_aim kwmb nikikosa huko ntaenda hata education,,, bro/sis subiria embe chini ya mnazi
Ungekaa pembeni tujadili tunaolipia na kujua fedha inapatikanaje na standard life ya wale wa vijijini. Wewe subiri chakula cha jioni mama akuite ule ulale
 
J
Tanzania watu wengi sana ni vilalamishi sana, mliikataa TCU sasa udahili wa moja kwa moja vyuoni nao mnaanza kuleta nongwa!?

Ngoja muisome namba ndiyo mtakoma.
Mtanzania ni kigeugeu sana, ndo maana Mh, anasimamia kwenye misimamo yake tu. Anawajua sana watz
 
Kizazi cha Fb kimekuja na huku, TCU ilikua inawachagulia vyuo mkalalamika , sasa hivi utaratibu wa zamani umerudi ilimpate vyuo mnavyotaka bado mnalalamika. Hivi kunamtu huwa anawaambia muombe Chuo zaidi ya kimoja? Kama huna hela omba Chuo kimoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom