Uonevu unaofanywa na Maofisa wa polisi wa Upelelezi hapo Airport Dares-Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uonevu unaofanywa na Maofisa wa polisi wa Upelelezi hapo Airport Dares-Salaam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Aug 22, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu wana JF na pia viongozi wa Serikali wanaohusika ningependa kuwataarifa kuwa kuna vitendo vinafanywa na baadhi ya Maofisa wa Polisi wa Upelelezi hapo uwanja wa Ndege wa kimataifa Wa Dares-Salaam.

  Hawa Mapolisi wa kipelezi wakikuona unatoka nje ya nchi wanakungoja tu umalize kutoka nje ya uwanja na hukukamata mpaka kwa ofisi zao za kipelelezi na kuanza kukuhoji na pia kukuweka ndani kwa muda wanaotaka wewe bila ya kosa lolote na wanaanza kukusachi wakihisi labda wewe ubeba madawa ya kulevya na endepo hautakuwa na hayo madawa watakuachia lakini kwa masharti lazima ukae kwao uende Toilet mara 3 ndio waweze kukuachia.

  Na wakikuachia wanavizuia vitu vyako ulivyokuja navyo toka nje ya nchi eti wanavichunguza kwa muda basi hata kama ndio wanavichunguza haitowezekana wewe wakuache na vitu vyako wavizuie tena sio kwa muda mchache inachukuwa hata mwezi mmoja wanavichunguza.

  Sasa inakuwaje hivyo vitu vyako ulivyokuja navyo wavichunguze kwa huo muda wa mwezi na haswa ukizingatia umekuja na mabegi ya nguo, zawadi kwa ndugu zako simu ya mkononi, Computer ya Laptop na vitu vingine vidogo vidogo?

  Ninachoshangazwa mimi inakuwaje hivyo vitu vyako vinazuia kwa muda wa mwezi eti kwa sababu ya kwa uchunguzi? Swali hili itabidi tumulize Kaimu kamishna mkuu wa Upelelzi ndugu Fred Nzoe inakuwaje watu wake waliopo hapo kiwanja cha ndege cha kimataifa kuwanyanyasa raia wema?

  Kwa hivyo vitendo vyao vya kuzuia mizigo yao kwa huo muda wa mwezi mzima kwa kisingizio cha kuvichunguza hivyo vitu?

  Hayo yametokea kwa rafiki wangu alie toka nje hivi karibuni kafanyia hivyo na kila akienda huko Kiwanja cha ndege cha kimataifa cha hapo Dares-Salaam anazungushwa mara aambiwe kuwa Mkuu wa kituo wa Polisi hayupo njoo keshokutwa na akienda hiyo kesho kutwa hurushwa tena njoo tena kesho kutwa hii kweli ndugu zangu wana JF na Viongozi wa Serikali wanaohusika tutaendelea kweli?

  Kwa fikira zangu hao wanaohusika hapo Aiport inaonyesha wanataka Rushwa wapewe pesa ili wapate kumuachia huyo Rafiki yangu vitu vyake walivyovizuia bila sababu yoyote ile ya maana. Je Ndugu Wana JF Mnalichukulia vipi hilo suala na hivi karibuni Mheshimiwa ndugu Rais wa nchi yetu JM Kikwete aliwakemea maofisa wa kuzuia rushwa wawajibike kikazi sasa ikiwa Mapolisi wetu wa kipelelezi wanamzungusha huyo rafiki yangu kumpa vitu vyake sasa inapata mwezi hawajibiki, je hao aliowakemea Ndugu Rais JM Kikwete maofisa wa kuzuia Rushwa wanafanya kazi gani?

  Ningeomba mnisaidie hilo tatizo langu maoni yenu ndugu wana JF wenzangu asanteni sana.
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kama hii ni kweli imetokea, plus malalamiko mengine kibao dhidi ya uwanja wetu wa ndege si ajabu mkasikia mtu kaamua kujivalisha mabomu na kwenda kujilipua pale airport ili wakose wote. Manake wamezidi sasa!

  Kha!
   
 3. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  duh! Hivi kwa nini? Kwa nini tunanyanyasana? Hii inanifanya nichukie Tanzania. Lakini nchi ni kama mtoto, huwezi kumchukia. Hivyo ni wa kufunzwa adabu.
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Aug 22, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  nakushauri kwa suala kama hili ni VIZURI UKAMUONA MWANASHERIA ATAKUSAIDIA SANA KATIKA KUDAI HAKI YAKO NA KUBAINISHA UKWELI WA TUKIO ZIMA.

  Mtafute mwanasheria afungue kesi dhidi ya Jamuhuri na mkuu wa polisi.
   
 6. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Kuhoji na kusearch ni jambo la kawaida. Ila hii ya kuweka watu ndani kwa muda wanaotaka inashangaza. Kama walivyochaingia waliotangulia bora utafute lawyer
   
 7. m

  madule Senior Member

  #7
  Aug 22, 2009
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani wana Forum,, Hizi habari zinawafikia walengwa?? au tunajibizana wenyewe tuu katika hii fora!, Mie ni Junior kabisa naona mawazo yote ni pevu na makini kwa saaana lakini nijulisheni walengwa wanayapata?

  [FONT=&quot]Footprints on the sands of time are not made by sitting down.[/FONT]
   
 8. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Madule,

  kwanza karibu sana barazani.

  hakika sisi hapa hatujali kama yanawafikia walengwa au laa ila nia yetu ni kumpa ushauri mtoa mada nini akifanye ili kuhakikisha haki ya anaipata kwa kufata njia sahihi za kisheria.
   
 9. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu, lakini lazima tuwe fair na polisi. NI kweli uwanja wa ndege wetu una mengi ya kulalamikiwa. Lakini vipi tunaweza kubalance kazi halisi na halali wanayotakiwa kufanya, na huo uhalifu unaofanywa na baadhi ya polisi wasiowaaminifu. Kuna wakati kunakuwa na genuine reasons za kuwashikilia watu na kuwauliza. Labda useme tatizo liko pale ambapo wale wanaofanya hayo madudu ndio wanapita kwa ulinzi juu na wale wasiofanya ndio wanakumbwa na marororoso hayo.
   
 10. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Asante sana Mkuu [​IMG] Shy umeweka vipi hayo maelezo yangu?
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Asante sana Mkuu HM Hafif kwa kunipa website inayohusu hao wanaotunyanyasa hapo Dar airport maana mambo kila kukicha yanazidi hapo Dar Airport asante sana Mkuu HM Hafif
   
 13. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Naamini wana haki ya kuku-search lakini sidhani kama wana haki ya ku-hold vitu au mizigo yako kwa mwezi mzima. Nafikiri kuna channel nzuri ya kufikisha huu ujumbe au malalamiko kama haya. Naamini makamanda wa polisi waliweka namba zao za smu kwa public, na wewe unaweza kuzibomoa tu na kuwaeleza kinachojiri hapo eapoti.
   
 14. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hakuna kauli polisi wanaipenda kama hiyo. "Tunafanya uchunguzi" ni kipengele kinachokuwa abused kupindukia.
  Wanaweza kukuweka kizuizini kwa makusudi wakilazimisha rushwa, wakakung'ang'ania kwa siku mbili usitoke - kisa, "bado tunafanya uchunguzi". Wakuu wa vituo vya polisi ndiyo balaa!

  Niseme kwamba, tunahitaji kwenda na wakati tuwashurutishe hawa viongozi watekeleze kile tunataka.

  Langu ni moja tu leo, kwamba POLISI ni kundi linalohitaji kufanyiwa uchunguzi kuliko raia, wezi wanaotumia silaha, au wauza unga. Vinginevyo, utamaduni utajengeka wa kupiga na kuua polisi.
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  Aug 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Wale wan nnta masikion hata uwaseme awabadiliki....labda cha kukusaidi siku nyingine usikubali wakusachi ukiwa mwenyewe...wana tabia ya kubambikiza vitu kama bangi..nk kwenye begi...nahisi tatizo ni mishahara midogo wanaendekeza njaa mpaka ******
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Sijawahi kupita airport nikitoka nje bila kubananishwa mlango na hawa jamaa. Well, wanafanya kazi yao, na ni vigumu sana kujua nani ni mhalifu na nani siye. Wanafanya kama wacheza kamari. Na pengine kwa aina ya mafunzo na uzoefu wa kazi yao, wanapata mashaka wakiona mtu mwenye sifa zinazolingana lingana na wahalifu.lakini kama walivyosema wengine, lazima wajue ku balance.Vinginevyo inakuwa kero kwetu wasafiri na wasiishie huku tu kwetu, waende na kwa VIP pia. Who knows dawa zinaingizwa zaidi upande gani
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Vinginevyo inakuwa kero kwetu wasafiri na wasiishie huku tu kwetu, waende na kwa VIP pia. Who knows dawa zinaingizwa zaidi upande gani

  WAKAMUULIZE DIRIA
   
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Aug 25, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu mpaka wakati huo huyo Rafiki yangu aliyezuiliwa vitu vyake hapo Dar Airport hajapatiwa na hao Mapolisi wa upelelezi wamesema kuwa endapo hatotowa Shilingi laki moja hawatampatia hata kama mwaka atakuwa anakwenda hapo Airport Dar kuviulizia vitu vyake hata kama itakuwa mwaka mzima hawatampatia hivyo vitu vyake je Ndugu zangu Wana Jf hiyo ni haki jamani? Au ndio hivyo nchi yetu haiwezi kwenda mbele mpaka kwa Rushwa? nimejaribu kuwapelekea habari hii yote Wizara ya mambo ya ndani na Kamishna Mkuu wa polisi wa Upelelezi wa Nchi lakini mpaka leo hawajanijibu. Sijuwi wamenitia kapuni?kwa sababu hayo yanayofanyika hapo Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha hapo Dar Airport hata hao wakubwa wanajuwa ila wamekaa kimya sasa Tutendelea kweli kimaisha? ndugu zanguni wana Jf na Viongozi wa Serikali wanaohusika nawaombeni munisaidie ili huyo rafiki yangu aliyezuiliwa vitu vyake hapo Kiwanja cha ndege Dar Airport aweze kupewa haki yake asanteni
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  Aug 25, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Dawa yao unaongea kiingereza tu! Akikusalimu wewe mkate lugha anakuacha.Mbinu hii imenisaidia nakatiza..tu.halafu ukiwa umevaa nadhifu suti ya nguvu wanakuwa na wasi wasi na wewe hata kukubebea mizigo yako na kukuwekea kwenye usafiri wako pale nje. Vaa Tshirt na jeans, ama kaptura na malaba lazima wahangaike na wewe.
   
 20. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #20
  Aug 25, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mnh, mkubwa ndio kusema 'yu ruk zat saspishaz'? "try" to change your appearance.

  ...mwenyezi Mungu amrehemu. :(
   
Loading...