Uoga wako wa utotoni uliishaje?

Uoga wako wa utotoni uliishaje?

Daah umenikumbisha miaka ya 2004 kama sio 2005 ile filamu ya inshuka nimetoka kuangalia video show mida kama ya saa nne usiku napopaswa kwenda kulala ni mbali kama km 4 mwisho wa kijiji ndo kulikuwa na mifugo yetu nimefika mitaa fulani nikaona kama ndondocha nikiinamaa linainama,nikirudi nyuma naona kama kinanifata nilitimua mbio hadi nyumbani nikalala kwenye mabanda ya uani niliogopa kugonga dingi alijua nimeshafika kwenye mifugo toka saa 12 jion,asubuhi napita pale nakuta kumbe ni kisiki toka siku ile nikawa nikifika pale usiku natuna kama nimeshinda vita
 
Mimi kwetu nimezaliwa wa kike peke yangu, kwa hiyo nilikua nalala chumba cha peke yangu, nilikua naogopa na ikifika usiku nalala na taa mpaka asubuhi, mama alikua ananitegea nimelala anaingia anazima taa,

Cha ajabu uoga huo haujaniisha hadi leo, siku Mr akisafiri sizimi taa hata moja ndani ya nyumba, kuanzia za sitting room,jikoni, bafuni, taa za nje koridoni na za chumbani zinawaka usiku kucha mpaka asubuhi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Tena nahamishia watoto wote chumbani kwangu ili nisione kama niko peke yangu mpaka akirudi ndio maisga ya kawaida yanaendelea, sijui huu uoga utaniisha lini mimi
Utaisha ukijitahidi na kujizoesha kulala peke yako bila taa. Amini ni jitihada yako tu.
 
Kabisa,naogopa sana hao viumbe
mkuu wale viumbe hata hawatishi hizo ni hisia tu za woga zilizojengeka juu ya hao viumbe, hebu kuanzia leo zikatae hizo hisia za woga uone ka utawaogopa tena.
 
Daah umenikumbisha miaka ya 2004 kama sio 2005 ile filamu ya inshuka nimetoka kuangalia video show mida kama ya saa nne usiku napopaswa kwenda kulala ni mbali kama km 4 mwisho wa kijiji ndo kulikuwa na mifugo yetu nimefika mitaa fulani nikaona kama ndondocha nikiinamaa linainama,nikirudi nyuma naona kama kinanifata nilitimua mbio hadi nyumbani nikalala kwenye mabanda ya uani niliogopa kugonga dingi alijua nimeshafika kwenye mifugo toka saa 12 jion,asubuhi napita pale nakuta kumbe ni kisiki toka siku ile nikawa nikifika pale usiku natuna kama nimeshinda vita
kwa hiyo kule kuinama na kuinuka zilikua hisia za woga tu mkuu?
 
mkuu wale viumbe hata hawatishi hizo ni hisia tu za woga zilizojengeka juu ya hao viumbe, hebu kuanzia leo zikatae hizo hisia za woga uone ka utawaogopa tena.

Mmh!sidhani kama nitaweza

Nilishawahi kutoka nje ya hostel uchi sababu ya hao wajusi...nafikiri ni kitu nimekubali nakiogopa,siwezi kuwazoea
 
duh! pole mkuu, kwa hali hiyo kweli huwezi kuwazoea.
 
mimi haujaisha nalala na Mwanga (Tochi) hadi leo
Naogopa kuogelea
Naogopa majengo marefu
yani mambo ni mengi
Majengo marefu me nayaogopa mboo..vile viduka vya k.koo vya ngazi za chuma hua navitazama tu ikibidi basi napanda na miguu na mikono ka nyani [emoji23][emoji23][emoji23]
 
hofu hasa hua ni nini mkuu hata upande ka nyani?
 
Mimi kwetu nimezaliwa wa kike peke yangu, kwa hiyo nilikua nalala chumba cha peke yangu, nilikua naogopa na ikifika usiku nalala na taa mpaka asubuhi, mama alikua ananitegea nimelala anaingia anazima taa,

Cha ajabu uoga huo haujaniisha hadi leo, siku Mr akisafiri sizimi taa hata moja ndani ya nyumba, kuanzia za sitting room,jikoni, bafuni, taa za nje koridoni na za chumbani zinawaka usiku kucha mpaka asubuhi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Tena nahamishia watoto wote chumbani kwangu ili nisione kama niko peke yangu mpaka akirudi ndio maisga ya kawaida yanaendelea, sijui huu uoga utaniisha lini mimi
Hii hali haitakuisha kwasababu imejijenga nakuwa habit. Habit is a tendency that becomes nearly or completely involuntary.
Maisha yako yote bila taa hutajisikia comfortable ukiwa alone. Na maisha haya tunatafuta comfortability in all We do.
 
Majengo marefu me nayaogopa mboo..vile viduka vya k.koo vya ngazi za chuma hua navitazama tu ikibidi basi napanda na miguu na mikono ka nyani [emoji23][emoji23][emoji23]
Kwani si kunakuwa na zile supportive bars, kwanini usizishike wakati unapanda?
 
Mi uwoga wangu ulikuwa nikiangaalia movie ya kutisha usiku sitting room. Bhasi kwenda chumbani hapo ni mtiti mpaka niongozane na baba au mama yeye akiwa mbele. Issue sasa taa ya room ikishazimwa, nikiangalia dirishani hata kama curtains zimeshushwa mind inatengeneza picha yale madude yapo pale yakisubiria mlango ufungwe yanifuate; Hizo kelele zake hapo watu wote watajaa chumbani. Kibaya zaidi nilikuwa king'ang'anizi wakutaka kuangalia hizo movies wakati zinawekwa.
Woga uliniisha baada ya tabia yangu ya kulia alafu haji mtu na mlango umerokiwa kwa nje, nitajifunika shuka gubigubi hapo mpaka usingizi unanipitia, asubuhi najikuta niko powa. Mazoea yakajenga tabia mpya
 
Majengo marefu me nayaogopa mboo..vile viduka vya k.koo vya ngazi za chuma hua navitazama tu ikibidi basi napanda na miguu na mikono ka nyani [emoji23][emoji23][emoji23]
sipandagi kule mm[emoji2][emoji2]
maana muda wote zinanijia picha za kuteleza au ngazi kuanguka
 
Ahaha.Nakumbuka enz hizo nikiangalia "mkanda" wa Yesu tu ooohhhh ndan hapaingiliki usiku.Hasa peke yangu.😂.naona kama malaika wAnanitokea hiv!!!!!😆😆😆
 
Hii hali haitakuisha kwasababu imejijenga nakuwa habit. Habit is a tendency that becomes nearly or completely involuntary.
Maisha yako yote bila taa hutajisikia comfortable ukiwa alone. Na maisha haya tunatafuta comfortability in all We do.
Ni kweli, ni kama habit
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom