Uoga wako wa utotoni uliishaje?

Uoga wako wa utotoni uliishaje?

mimi haujaisha nalala na Mwanga (Tochi) hadi leo
Naogopa kuogelea
Naogopa majengo marefu
yani mambo ni mengi
Hapo kwenye majengo marefu na kuogelea tupo pamoja
 
Mimi kwetu nimezaliwa wa kike peke yangu, kwa hiyo nilikua nalala chumba cha peke yangu, nilikua naogopa na ikifika usiku nalala na taa mpaka asubuhi, mama alikua ananitegea nimelala anaingia anazima taa,

Cha ajabu uoga huo haujaniisha hadi leo, siku Mr akisafiri sizimi taa hata moja ndani ya nyumba, kuanzia za sitting room,jikoni, bafuni, taa za nje koridoni na za chumbani zinawaka usiku kucha mpaka asubuhi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Tena nahamishia watoto wote chumbani kwangu ili nisione kama niko peke yangu mpaka akirudi ndio maisga ya kawaida yanaendelea, sijui huu uoga utaniisha lini mimi
mkuu hadi unafamilia bt umwoga kiasi hicho?
 
Naogopa kulala giza na ubibi wangu hivi hivi..nikiwa mwenyewe naacha taa zinawaka na bado usingizi unakuwa wa mang'amng'am
 
We acha tu, tena umeme ukikatika usiku halafu niko peke yangu, ndo nameza kabisa sleeping pills ili nilale
dah! pole sana mkuu bt uoga ni hisia ukizikataa ndo inakua suluhu ya tatizo jumla.
 
Mimi panya hata Nyumba nitahama nasikia kinyaa sana ni bora nishike mavi ya mtu mwingine kuliko kumuona panya
 
Mimi panya hata Nyumba nitahama nasikia kinyaa sana ni bora nishike mavi ya mtu mwingine kuliko kumuona panya
pole sana mkuu bt ujue kuogopa vitu ni hisia, ukizikataa hizo hisia utakiona normal unachokiogopa
 
Natumai hamjambo wananzengo.

Karibu kila mmoja wetu utotoni alikuwa mwoga, hasa mida ya usiku hata ukitumwa ndani pekee ako huendi mpaka usindikizwe bt kuna tukio moja lilikokua sababu ya ule woga kutoweka hivo karibuni hapa kushare namna uoga ule ulimalizika.

Binafsi siku1 tulienda harusi ya mbali kidogo na washkaji, tukaazimia saa4 usiku ndo utakua muda wa kurudi, muda ulipofika wenzangu wakagoma kurudi, dah! nilitokwa kijasho chembamba maana kesho yake nilipaswa kwenda shule.

Nilijitoa mhanga wa kurudi peke angu huku nikijesemea liwalo liwe, nilitembea kwa woga sana huku nikilia kwa majuto kwa nini nilienda bt hatimaye nilifika home na tangu siku hiyo uoga uliisha.

Je, kwa upande wako woga wako ulimalizikaje?
Nilikuwa naogopa watu warefu hususan wageni nilipandikizwa kwamba hao ni majini. Utoto we acha tu!
 
dah! pole sana mkuu bt uoga ni hisia ukizikataa ndo inakua suluhu ya tatizo jumla.
Ngoja nijaribu kwakweli maana mpaka watoto wanajua baba asipokuwepo taa hazizimwi ndani
 
Ngoja nijaribu kwakweli maana mpaka watoto wanajua baba asipokuwepo taa hazizimwi ndani
we jaribu tu utaushinda huo mtihani, we unadhani taa inazuia kitu gani kama sio hisia za woga tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom