Uoga wa Zitto Kabwe kwa Tulia Ackson

Uoga wa Zitto Kabwe kwa Tulia Ackson

Jamii ya wanazuoni imekuwa ikijiuliza ni kwanini mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe anampiga vita mgombea unaibu spika Dk.Tulia Ackson.

Wanahoji ni kwanini Zitto Kabwe anamhofia huyu mwanamama wakati ana vigezo vyote vinavyompa "credibility" ya kugombea.Imefikia hatua Zitto anamnadi Mussa Azzan ambaye ni mbunge wa Ccm na kusahau kuwa yeye ni mpinzani ndani na nje ya bunge.

Hapa ndipo dhana ya usaliti kwa Zitto Kabwe inapozidi kumea kwenye masikio ya watanzania.Zitto Kabwe hataki kukubali kuwa siasa ya bunge sio yake peke yake.

Mnakumbuka sakata la aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TPDC ambaye PAC ikiongozwa na Zitto Kabwe iliamuru akamatwe na kuwasilishwa polisi!?Tena kwa makosa ambayo PAC ilikuja kuangukia pua!!

Namzungumzia Andilile Mwainyekule.Huyu ni mume wa ndoa wa Dk.Tulia Ackson.Zitto Kabwe anauona ugumu wa yeye kuiyumbisha serikali kwa skendo za kupika kama kiti kitasimamiwa na Dk.Tulia Ackson.

Zitto Kabwe anahofia Dk.Tulia Ackson kutumia mwanya wa kujua kwa undani sakata la TPDC na kuiokoa serikali na hoja ambazo Zitto Kabwe anategemea kuziibua na kuziendeleza.

Suala hapa sio unaibu spika bali ni maslahi ya mifuko ya Zitto Kabwe na hatma ya maisha yake ya kisiasa.

Naona walio nyuma ya kivuli cha Mzee wa Monduli wanatoa macho, JK anasema wameenda kujitafutia Riziki zao tuwaache kwa sababu hawatapata kitu.
 
Vichwa vya panzi wengi sana humu, jana uliunga mkono hiki, leo kile basi ni kutaabika tuuu
 
Mleta mada rudi ukajipange upya majority hatujakuelewa cheap politics kwa sasa hazina nafasi hapa kazi tu majungu kahawani
 
Zitto siyo kabisa kwa maslahi ya taifa, mi mwenyewe nilisoma maoni yake hadi nikashangaa sana hoja kama zile kutolewa na zitto, nikajisemea hapa lazima kuna kitu si bure

Kumbe yule mkurugenzi wa TPDC ni mume wa Tulia, haaaa sasa naunganisha dots, ndo maana kumbe Zitto anashikwa na tumbo la kuhara

Na pia tuitazame miswada ya gesi iliyoigizwa bungeni kwa dharula...yawezekana serikali ya awamu ya nne ndio inafosi haya ili ikapate mlinzi bungeni...ni vigumu kwa sifa kwa watanzania mamimlioni huyu mama afikie kwenye peak within 67 day??

The QN is YYYYYYYYYYY????????????????????
 
Looking for popularity can lead one in making him/her self to look cheap and foolish
 
Leo nimemsikia Zito akimtetea Ndungayi.Kweli lisemwalo lipo,kama halipo,linakuja.
 
Hamna haya ya kuumiza kichwa kuhusu issue za Zitto.

Toka lini Zitto aliwekwa ndani kama wenzake akiwa CDM? Ukipata jibu hilo utajua Zitto ni nani katika nchi hii.

Kumbe kuwekwa ndani ni kipimo cha mwana siasa bora? Au asiye msaliti? Nilikua sijui
 
Hakuna hoja zaidi ya majungu na chuki kwa Zitto tu.

Hivi kumuunga mkono Zungu ni usaliti?

Anamsaliti nani sasa?

Dada tafuta biashara nyingine, Zitto muache afanye yake.
 
Hapana Zitto anajulikana kwa usaliti usitake kumtete wakati fani yake ipo wazi.

The Tomorrow People

Zitto kajenga hoja yake based on separation of Power kati ya Bunge na serikali wewe unaleta hoja ya ndoa za watu?

Mambo mazito juu ya mustakabali wa taifa letu unataka kuyahamishia kwenye trivialities.Inakuwa matrimonial case?

Baadhi yetu watanzania sijui tukoje.
 
Zitto anapinga mteule wa Serikal Dr.Tulia kuwa Naibu Spika tunaambiwa anatumika, angeunga mkono pia angeambiwa anatumika, kuna wanasiasa wajinga kwa kukosa kwao hoja sasa wamepanga kumshambulia Zitto kwa Lolote atakalosema, hili Ni bunge lenye mawazo tofauti, kama hoja ya Zitto huikubali jenga hoja ya kuvunja hoja ya Zitto. Huyu Kijana ana haki zote za Kibunge ikiwa ni pamoja na kupinga mawazo ya mtu au kundi jingine lolote au kuwa na mawazo tofauti na wengine!!
 
kipindi job anapitishwa kuna majitu yalikuja na hoja za uzoefu bungeni sasa nasubir kuona kati ya huyo Akson na Zungu nani mzoefu bungeni.Small mind
 
Du! Nilianza kumsifia daktari kumbe ni mambo ya who knows who....ngachoka tayari
 

1. Sijawahi kumsikia Mkurugenzi Mkuu wa TPDC aitwaye Andilile Mwainyekule. Huyu aliongoza TPDC mwaka gani? Au ndiye aliyepo sasa?

2. Kama huyu dada anakwenda bungeni kuiokoa serikali na kumtetea mumewe, nina budi kuungana na Zitto kumkataa. Hatufai. Hatutaki watu wanaokuwa installed kwenye hizi nafasi kwa malengo binafsi. Tunataka watu wanao earn hizi nafasi kwa uwezo wao na bila kubebwa.
 
Mi kwa uwelewa wangu mdogo naona mama bi. Tulia hata mama ni au atakuwa naibu spika bado atakuwa ameshushwa kulingana cheo cha awali au
 
Back
Top Bottom