Uoga wa Zitto Kabwe kwa Tulia Ackson

Uoga wa Zitto Kabwe kwa Tulia Ackson

1. Sijawahi kumsikia Mkurugenzi Mkuu wa TPDC aitwaye Andilile Mwainyekule. Huyu aliongoza TPDC mwaka gani? Au ndiye aliyepo sasa?

2. Kama huyu dada anakwenda bungeni kuiokoa serikali na kumtetea mumewe, nina budi kuungana na Zitto kumkataa. Hatufai. Hatutaki watu wanaokuwa installed kwenye hizi nafasi kwa malengo binafsi. Tunataka watu wanao earn hizi nafasi kwa uwezo wao na bila kubebwa.

3. Zitto amekuwa akidai kwa muda mrefu sasa mikataba ya mafuta na gesi iwekwe wazi na kila mtu aweze kuisoma kujua kilichomo. Hata kama ana maslahi binafsi, madai haya ni ya msingi na yeyote mwenye kuitakia mema nchi anapaswa kuunga mkono madai hayo bila kujali ni kama ni mume wa Dr. Tulia anaiongoza TPDC. Wananchi kupitia wawakilishi wetu tunapaswa kushiriki zaidi katika michakato ya uingiaji wa mikataba hii.
 
Kipindi cha escrow andilie alikuwa kaimu mkurugenzi mkuu
 
Ipo shida mleta mada

You have missed a bigger picture
 
pamoja na kuwa wengi wamekunanga kwenye huu upuuzi wako ulioleta hapa, mimi nakuambia hivi; Zitto is there to stay. whether you like or not. after all upo pande zipi hapa dar nikutoe out angalau ukapunguze mawazo!

Jamii ya wanazuoni imekuwa ikijiuliza ni kwanini mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe anampiga vita mgombea unaibu spika Dk.Tulia Ackson.

Wanahoji ni kwanini Zitto Kabwe anamhofia huyu mwanamama wakati ana vigezo vyote vinavyompa "credibility" ya kugombea.Imefikia hatua Zitto anamnadi Mussa Azzan ambaye ni mbunge wa Ccm na kusahau kuwa yeye ni mpinzani ndani na nje ya bunge.

Hapa ndipo dhana ya usaliti kwa Zitto Kabwe inapozidi kumea kwenye masikio ya watanzania.Zitto Kabwe hataki kukubali kuwa siasa ya bunge sio yake peke yake.

Mnakumbuka sakata la aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TPDC ambaye PAC ikiongozwa na Zitto Kabwe iliamuru akamatwe na kuwasilishwa polisi!?Tena kwa makosa ambayo PAC ilikuja kuangukia pua!!

Namzungumzia Andilile Mwainyekule.Huyu ni mume wa ndoa wa Dk.Tulia Ackson.Zitto Kabwe anauona ugumu wa yeye kuiyumbisha serikali kwa skendo za kupika kama kiti kitasimamiwa na Dk.Tulia Ackson.

Zitto Kabwe anahofia Dk.Tulia Ackson kutumia mwanya wa kujua kwa undani sakata la TPDC na kuiokoa serikali na hoja ambazo Zitto Kabwe anategemea kuziibua na kuziendeleza.

Suala hapa sio unaibu spika bali ni maslahi ya mifuko ya Zitto Kabwe na hatma ya maisha yake ya kisiasa.
 
licha ya kumkubali zitto ila kwahili simuungi mkono eti ana sifa ni sifa gani alikuwa anazitaka kwa dr tuli anyway hakuna alizaliwa na sifa. hayo mengine ya mume wake dr tuli siyaamini sana
 
Rais atafanya kazi yake tu hata wakijifanya kumhujumu, tunaelewa kwamba sahivi Tz tuna watu wanajiita watz lakini kimtizamo wao ni sawa na wazungu, hawaioni Tz kama nchi na ardhi walikozaliwa ..wanakaaa mda wote wanataka kuiumiza tu, na walaaniwe.
 
Japo mimi simkubali zitto huyu ya wa leo labda aonyeshe mabadiliko, lakini hoja yako haina kina. unaleta hoja mpya
maana zito katoa vitu vya msingi wewe unajibu vitu vingine.

ungeleta hoja tofauti tungekuelewa unless otherwise ulitaka tujue mume wa huyo dada nalo sio jambo baya japo halina faida kwa sasa.
naomba kutofautiana na mleta uzi
 
The Tomorrow People

Zitto kajenga hoja yake based on separation of Power kati ya Bunge na serikali wewe unaleta hoja ya ndoa za watu?

Mambo mazito juu ya mustakabali wa taifa letu unataka kuyahamishia kwenye trivialities.Inakuwa matrimonial case?

Baadhi yetu watanzania sijui tukoje.

Ahahahaaa mkuu umenchekesha Sanaa. Akijbu haya maswali atatambua uelewa wake ni wa kiwango gani
 
Last edited by a moderator:
Kwani naibu spika anachaguliwa lini?
Na CCM wamemsimamisha huyo Dada na nani?
 
Una maama kazi ya Tulia itakuwa kumsaidia mumewe? Makubwa
Yaani jumps insider information
 
licha ya kumkubali zitto ila kwahili simuungi mkono eti ana sifa ni sifa gani alikuwa anazitaka kwa dr tuli anyway hakuna alizaliwa na sifa. hayo mengine ya mume wake dr tuli siyaamini sana

Alihomaanisha zito huwezi kuchaguliwa na rais uwe naibu spika,yaan haiitaji elimu ya chuo kuliona ilo.hulka ya wanadamu ni kumtumikia alyemfanyia mazuri,sasa hapo huon kuwa uyu naibu spika atalinda maslai ya serikal?kama hata ilo hujaliona bas hufai kuitwa binadamu
 
Kwa akili yako wewe matope unaona sawa kwa mke wa Mkurugenzi mkuu wa TPDC kuwa speaker kipindi hiki kuelekea uchumi wa gesi na mafuta?
 
Huyu Tulia Ackson,nimeona cv yake amechaguliwa tena kua naibu mwana sheria mkuu wa serikali.Kuna taarifa pia kua ana tarajiwa kua ndio naibu spika.Vyeo hivi viwili kwa wakati mmoja inakuaje?jamani nisaidieni munao jua hii mambo.
 
Cheo cha Naibu mwanasheria sheria raisi amekitengua sasa amechaguliwa kama mbunge pia amepitishwa na CCM kuwania nafasi ya unaibu spika.
 
Back
Top Bottom