Unywaji pombe salama

Wimsha

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
518
503
Wale wenzangu tuanaoenda maeneo ya kujirusha hebu tujikumbushe basics za unywaji salama. Mimi nazijua zifuatazo (ingawa mara zingi zizifuati)

1. Epuka kukaa baa ambazo ni hatarishi ; hakikisha unakaa baa ambayo ni rahisi kwako kurudi nyumbani

2. Nidhamu ya kiwango cha kilevi ni muhimu ni bora ukanywa taratibu na kwa muda mrefu. Kula chakula ni muhimu pia.

3. Ukienda bar tafuta sehemu ambayo utakuwa peke yako. Usikae kwenye meza ambazo zina kampani nyingine tayari “huwajui”.

4. Ukiagiza kinywaji fanya mawasiliano na mwili wako hasa ku- control mkojo. Hakikisha umemaliza kinywaji chako kabla ya kwenda short call na ukirudi anza na fresh bia na fresh glass.

5. Daima jenga uhusiano “mwema” na anayekuhudumia kwani kumbuka unapoingia baa “you are a dead body”. Ni huyo muhudumu wako atakeyekuhakikishia usalama wako.

6. Ni busara kujenga utamaduni wa kutoa “tip” kwa huduma uanyopewa. Siku moja itakusaidia maradufu.

7. Heshimu chaguo la kinywaji chako na kamwe usiige au kuchanganya vinywaji “vileo”.

Wewe unazifahamu zipi zingine?
 
Kwa hapa Nairobi hayo ndio maisha halisi ya mtu yeyote anaeingia bar. Ukizubaa unawekewa mchele fasta. Ila kwa TZ nadhani hali siyo mbaya kiasi hicho kukaa bar kwa tahadhari
 
Ukienda baa hakikisha una kiasi cha fedha cha kutosha unywaji wako. Usisumbue wenzako wakununulie bia/pombe.
 
Wale wenzangu tuanaoenda maeneo ya kujirusha hebu tujikumbushe basics za unywaji salama. Mimi nazijua zifuatazo (ingawa mara zingi zizifuati)

1. Epuka kukaa baa ambazo ni hatarishi ; hakikisha unakaa baa ambayo ni rahisi kwako kurudi nyumbani

2. Nidhamu ya kiwango cha kilevi ni muhimu ni bora ukanywa taratibu na kwa muda mrefu. Kula chakula ni muhimu pia.

3. Ukienda bar tafuta sehemu ambayo utakuwa peke yako. Usikae kwenye meza ambazo zina kampani nyingine tayari “huwajui”.

4. Ukiagiza kinywaji fanya mawasiliano na mwili wako hasa ku- control mkojo. Hakikisha umemaliza kinywaji chako kabla ya kwenda short call na ukirudi anza na fresh bia na fresh glass.

5. Daima jenga uhusiano “mwema” na anayekuhudumia kwani kumbuka unapoingia baa “you are a dead body”. Ni huyo muhudumu wako atakeyekuhakikishia usalama wako.

6. Ni busara kujenga utamaduni wa kutoa “tip” kwa huduma uanyopewa. Siku moja itakusaidia maradufu.

7. Heshimu chaguo la kinywaji chako na kamwe usiige au kuchanganya vinywaji “vileo”.

Wewe unazifahamu zipi zingine?
Bar ni sehemu ya kujiachia sitaki kujipangia masharti wala kupangiwa, badala ya kuburudika nitakuwa nawaza vigezo na masharti (kuachana na vile vya msingi )
 
nilivyokuwa nakunywa nilikuwa natoa tip balaa. mabaamedi wakiniona wanaanza kushangilia.
 
Kwa hapa Nairobi hayo ndio maisha halisi ya mtu yeyote anaeingia bar. Ukizubaa unawekewa mchele fasta. Ila kwa TZ nadhani hali siyo mbaya kiasi hicho kukaa bar kwa tahadhari
Mchele unauhusiano na vyombo
 
Haha kweli hapa tumekutana, wengine tumezoea kunywa bar jirani na nyumbani au hata kama ni ya mbali basi jua nipo na mwenyeji au mtu anayeifahamu vizuri hiyo bar.
Sometimes hutokea unajikuta upo bar ambayo hufahamu na hapo ndipo umuhimu wa hizo tips unapokuwepo. Usimwamini kila anayekuhudumia especially usiku bali umakini wako ndio afya yako
 
Back
Top Bottom