Vitu vya kuepuka 2024 ili uendelee kuwa salama zaidi

george aloyce

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
1,197
1,835
Miongoni mwa vitu vya kuogopesha sana ni hasira,watu wanapopatwa na hasira wengine hufanya matendo ambayo daaah 🥹🥲 ,unasema jamani vipi hivi?ila ndio matendo na yashakua yamefanyika

Ndugu yangu, katika haya maisha, katika kuishi kwako, kwenye pitapita zako, katika mambo Yako, chunga sana kuchokoza hasira ya mtu, yaani chunga, chunga, sana, ogopa, tena ogopa kabisa.

Unajua Kuna watu wagomvi, kuna watu wapenda chokochoko, kuna watu mashujaa wa ujinga, kuna watu wakorofi, Kuna watu wasumbufu, Kuna watu wanatafuta ubaya, Kuna watu wapenda sifa na Kuna wale watu aaaah mie nammudu huyo, nitamkomesha huyo,haniwezi huyo, ndugu yangu tunapoelekea mwaka 2024 pamoja na mambo mengine EPUKA KUCHOKOZA HASIRA YA MTU

Kuwa mjinga, kuwa mzembe, kuwa mwoga, jifunze kushinda ndani Yako na kuwa dhaifu mbele Yao ni mbinu Fulani hivi ya kijinga ila itakusaidia sana kuepukana na rabsha zisizo na msingi lakini kubwa kujiepusha na majanga dhidi yako, dhidi ya familia Yako ama watu uwapendao

Mfano Mtu ajifunze ama awe na utaratibu hata wa KUTEMBELEA mahakamani na pengine kusikiliza kesi mbalimbali basi utashangazwa na umbali mwanadamu anaweza kwenda kwasababu ya hasira ama kumkomesha Mtu mwingine

Unaweza kuwa uko katika mazingira ambayo hayakupi NAFASI ya kujua matukio mbalimbali ya kimaisha isikupandishe kichwa ukadhani hayo matukio hayapo,yapo Tena mengi,Tena yanatisha

Watu wanauliwa
Wanatiwa ulemavu
Zinauliwa familia zao
Watoto wanabakwa na kulawitiwa
Watu wanaambukizwa UKIMWI kusudi
Watu wanaokotwa vifurushi
Wanatiwa vichaa
Watu wanakutwa na majanga mengi sana

Kwasababu tu wanachokoza hasira za watu

Yaani ziko athari nyingi sana zinazoletwa na watu kuchokoza hasira za wengine,hasara ambazo hazimithiliki Wala hazipimiki lakini ndio zinakua zishafanyika

Unaweza kufanya jambo dogo sana lakini likanyanyua hasira kuu na muda mwingine jambo dogo likanyanyua hasira ya mambo mengine madogomadogo ama ya nyuma wanasheria tunaita Cumulative provocation.

Kwamba unamchokonoa Mtu kidogokidogo mwisho anajaa upepo anakufanya jambo baya ,kwasababu tu ulishamchokoza akakuvumilia sana ama kwa muda mrefu Sasa amekosea ustahimilivu kwa kuendelea kuhimili unayomfanyia

NDUGU ZANGU KWA MWAKA 2024

Epuka sana magomvi na watu
Kuchokonoa watu
Kutafutana undani na watu
Kutafuta ushujaa kwa watu
Kuchokoza hasira ya mtu

Yaani jambo lolote ambalo litakutia matatani kwa namna moja ama lingine LIKWEPE na hii iendane na kujiepusha na watu ama makundi yanayokutia ushujaa wa kukuangamiza maana Kuna namna unaweza tengenezewa picha ya kujiona shujaa lakini ule ushujaa wako ukawa unakuchimbia shimo la kukuangamiza,wapo watu wengi sana wameingia matatani kwasababu tu ya makundi wanayoambatana nayo

Ndugu yangu, chunga chunga sana mie Huwa naambia watu wanaonizunguka usichokoze hasira ya mtu, USIMCHOKONOE Mtu, Usigombane na watu, usikosee watu kwa makusudi, usianzishe uadui ama vita mahala ambapo hapana vita ama uadui lakini pia usimpimie Mtu.

Yaani usiseme nikifanya hivi nitamkomesha, nitamnyoosha,atakoma,atateseka,atahangaika, kifupi usipime reaction ya mwingine kwenye chochote as long as huyo mwingine sio wewe, maana ukiwa wewe unaweza kujipima mwingine, uwe unamjua ama kutomjua usimpime.

Hata mke /mume unaoyelala naye kitanda kimoja usimpime ,wapo watu wengi wameuliza na wenzi wao na hawakuwahi kuwaza watawaua na kama wangewaza wangewakimbia muda mrefu sana lakini shida nini WALIWAPIMA ukiwa na utaratibu wa kusoma ama kusikiliza kesi za mauaji basi utajifunza mengi kubwa utajifunza KUOGOPA WATU sio udhaifu KUOGOPA WATU

Penginepo hapo pichani palikua na UGOMVI, ama sintofahamu ama rabsha kiasi tendo dogo limeamsha hasira na kufanyika tukio kubwa la kutisha

Tutasikitika
Tutasema hajafanya sawa
Tutasema ni wazimu
Tutasema naye hatokua salama

Lakini katika yote kwako ama kwa familia hasara itakua ishatokea.

Kwahiyo kuepusha hasara kwepa maudhi, kwepa shida, kwepa magomvi,kwepa vita, epuka kuudhi, epuka kuchokonoa, epuka kuzifuata ama kuzitafuta hatari

Isipokua kwa bahati mbaya tu,maana katika maisha migongano haiepukiki ila hakikisha hutafuti migongano isipokua Ile tu ilokutafuta yenyewe.

Kazi yangu kukumbushia mwenye kuelewa na aelewe

MWAKA 2024 EPUKA KUCHOKOZA HASIRA YA MTU.

1704116292210.jpg
 
Back
Top Bottom