Kuna namna huyu Zuzu ACP Ramadhani Kingai afunguliwe Mashtaka personal kama kuna sheria inaruhusu.

Screenshot_20211027-110807.png
 
Imefika wakati ni bora utupwe kwenye kundi la Simba ujue moja labda watakuacha kama wameshiba, kuliko ujikute mikononi mwa hao polisi wenye njaa isiyoisha, utajuta.

Kwa tabia ukali aliyoonesha huyo Kingai pata picha uko chini yake anakulazimisha ukiri atakacho, mateso, vipigo, matusi, ni halali yako mpaka pale utapokiri umekosa hata kama kimsingi hujakosa, wale kina Adamoo ni mashahidi wazuri sana wa hiki nachoandika.

Tatizo wamelelewa na CCM kwa tabia hizo, kuwatesa wapinzani kwa manufaa yao, matokeo yake sasa polisi wame extend unyama wao mpaka kwenye matukio nje ya siasa, wanajua watalindwa na mabosi wao wa CCM, sasa nashangaa kada wa lumumba unakuja kulalamika kwa tatizo mlilolizaa na kulilea wenyewe.
 
Pole yake kijana, ila hivi vitu vya kununua mikononi mwa mtu ni hatari sana, kama kuna ulazima ni bora kumuomba list ya hicho kifaa!
 
Habari za muda huu ndugu zangu.

Kwa kweli Kwa Hali ilivyo, inabidi jambo kubwa sana lifanyike katika nchi yetu kubadili mifumo yetu ya ulinzi na usalama wa raia...
Haya mambo yanaumiza sana na nasikitika watu wanaoshabikia vitendo hivi kwa sababu yoyote ile. Kwa kweli mahabusu za polisi hazina tofauti yoyote na concentration camps za Hitler.

Ukitaka kujua unyama wa polisi ishi karibu na kituo Cha polisi unaweza kuchanganyikiwa mahabusu wanateswa vibaya mno mayowe ni muda wote si usiku si mchana na saa nyingine mtu anapiga mayowe hadi sauti inafifia na kuishia.

Ushauri wangu Jeshi la Polisi lipate IGP toka JWTZ na lifumuliwe mwanzo mwisho lakini pia lifanyiwe mabadliko Kama yaliyofanyika

Mahakamani Askari wafanye kazi za uaskari mambo ya utawala yafanywe na watawala waliosomea utawala labda hivi vitendo vya kinyama vinaweza kupungua kidogo kweli Siro na wenzake wenye roho Kama yake Mungu awalaani kabisa.
 
Wakati huku Tanzania akina Kingai walipandiswa cheo, huko Kenya ambako kuna Rais wa watu hali ni Tofauti.
 
Back
Top Bottom