Ungewapa ushauri gani hawa?

Mzee Mwanakijiji leo nitakujibu kimjini-mjini kidogo. Nitajibu baadhi tu ya hoja zako.

a. Migomo isiyo ya lazima isitokee
Migomi isiyo ya lazima ilitokea lini? Inayotokea sasa yote ni ya lazima. Kama huu wa sasa wa UDSM ulikuwa wa lazima sana. Yaani serikali ina pesa za kupeleka ndege 7 kuzika mtu mmoja halafu inakosa vijishilingi vya kuwapa wanafunzi elfu 20 ada! Mbona ukiwapa watoto elfu 20 shilingi milioni 4 kila mmoja zinafikia jumla ya shilingi bilioni 80 tu! Hizo ni chini ya kiasi kinachochotwa BoT kila mwaka!

Elimu ya Juu inapatikana kwa kila atakaye

Wewe sasa Mzee Mwanakijiji sijui unataka nikueleweje! Yaani unataka universal college education? Bado tunataka kufikia universal secondary education. Huenda tukafikia kipindi cha elimu ya juu kupatikana kwa kila awazaye, lakini sio kila atakaye. Wengine wanataka lakini hawawezi (hazipandi).

Familia zinaweza kumudu elimu ya juu
Kusomesha taifa la kesho si jukumu la familia peke yake. Lazima serikali iendelee kutumia kodi zetu kusomesha watoto wote wenye uwezo. Wazazi watachangia, lakini sii jukumu lao tu. Na nakubaliana na mwenzetu aliyeshutumu tabia ya sasa ya kuchangia sherehe na mazishi tu. Lazima kuchangia elimu. Viko vikundi vya michango ya kuzikana, lakini sijasikia kikundi cha michango ya kusomesha. Kuna kosa hapo.

Najua Msuya alisema "kila mtu abebe Msalaba wake" lakini mtu anapoanguka chini ya Msalaba wake inabidi Simeoni wa Kirene alazimike kubeba naye.
 
Unaombwa utoe ushauri wa jinsi ya kutatua matatizo ya elimu ya Juu nchini ili hatimaye:

a. Migomo isiyo ya lazima isitokee
b. Elimu ya Juu inapatikana kwa kila atakaye
c. Familia zinaweza kumudu elimu ya juu
d. Elimu ya Juu inakuwa ni ya kiwango cha juu katika ubora wake na kuandaa wanafunzi katika ushindani wa soko la ajira la kimataifa.
e. Kuwaandaa wanafunzi kuwa watafiti na kuchangia utaalamu wao katika mabadiliko ya jamii yetu.
f. Kujenga nidhamu ya kisomi nchini.

NB: Yawezekana kuna kaubaguzi ka aina fulani hapa kwa kufocus kwenye elimu ya juu tu. Mniwie radhi.

Ngoja tuangalie haya yafuatayo:

(a) Elimu ya chuo kikuu ni ngumu na hasa katika mazingira ya hapa kwetu ambapo wanafunzi wanakuwa wanakabiliwa na ukweli kuwa wakifeli mitihani yao watafukuzwa na kupata fedheha kutoka kwa jamii yao. Kwa hiyo wanafunzi wengi walioko chuo kikuu huwa hawahitaji bughudha za aina yoyote kusudi waelekeze nguvu zao katika masomo. Hata hivyo wakishavurugwa kidogo tu, basi huwa hawawezi kabisa kugawanya muda wao kati ya kukabiliana na bugudha hizo na vile vile kufuatilia masomo yao. Huanza kwa kupuuza bugudha zile na kuendeleza nguvu zao kwenye masomo hadi pale inapoonekana kuwa bugudha zile hazitaondoka ndipo huamua kuweka masomo pembeni ili wakabiliane na budhudha zile kwanza. Sasa hicho ndicho chanzo cha migomo. Kumbuka kuwa vijana wale ni watu waliokomaa kiakili na wanasoma kozi tofauti tofauti huku wakitoka kwenye background tofauti vile vile. Wakishakubaliana jambo basi ujue jambo lile lina ukweli fulani na ni muhimu kwa viongozi kulichukulia jambo hilo kwa uzito unaostahili bila kutumia njia za mkato mkato.


(b) Serikali itambue kuwa elimu ya juu ni ya lazima kwa kila raia aiwezae. Katika bajeti ya serikali kuwe na kipaumbele kwenye elimu na kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima. Mpaka sasa hivi Tanzania ina uwezo mkubwa sana wa kutoa elimu ya juu bure kwa raia wake wote ila tu haijapanga na kutumia raslimali zake vizuri. Mimi niliwahi kusoma na wanafunzi wa kutoka Botswana wakiwa wanalipiwa na serikali yao kuliko skolaship niliyokuwa nimepewa na wajerumani. Tunaweza kufanya ya Botswana bila wasi wasi kama viongozi wetu wataamua: Kupanga ni Kuchagua.

(b,c) Kumpa elimu ya juu kila aitakaye si jambo rahisi sana bila kuangalia uwezo wake. Nadhani tunachotakiwa hapa ni kuweka viwango vya elimu ya juu itakayolipiwa na serikali na ile ambayo kila mtu atajilipia binafsi. Mimi nadhani kwanza tunahitaji kuimarisha elimu ya sekondari na baraza la mitihani ili wanafunzi wote wamalizao form 6 wawe na nafasi sawa mbele uchaguzi wa kuingia chuo kikuu. Uvujaji wa mitihani na tofauti za mazingira ya masomo baina ya shule na shule huwafanya baadhi ya wanafunzi wawe "at a disadvantage" hata kama wana uwezo mzuri sana kimasomo. Baada ya kuwa ni standard nzuri huko sekondari, serikali iweke skolaship za kushindania na viwango vya kuzipata. Kwa mfano kuwe na skolaship za Engineering, Medicine, Law, Science, na specialization nyingine na viwango vyake vijulikane wazi wazi. Wanafunzi wa fom 6 waambiwe tangu huko form six kuwa washindanie skolaship hizo kutegemea na viwango vya pass zao za mitihani; viwango vyenyewe viwe reasonable siyo vile vya kukaangana. Kwa hiyo mwanafunzi anayeshindwa kufikia viwango vitakiwavyo kwenye skolaship zile aridhike kuwa hakufikia kiwango. Skolaship hizo ziwe zinalipia gharama zote za mwanafunzi siyo tena kudai michango kutoka kwa wazazi.


(c) Kwa wale ambao watashindwa kufikia viwango vya skolaship kwa margin ndogo wapewe second chance ama kwa kutakiwa warudie mitihani au wachukue mikopo ya elimu isiyokuwa na riba; na kuwe na utaratibu wa kuhakikisha kuwa mikopo hiyo inalipwa kweli.



(d,e, f) Viongozi wa taasisi za elimu ya juu wasiwe wanateuliwa na rais, badala yake wawe wanapatikana kwa search process. Kama CEO wa TANROADS alipatakana kwa search process basi hata viongozi wa vyuo vikuu wawe wanapatikana kwa njia hiyo. Hii itawafanya wawe more academic kuliko kuwa political. Kwa sasa wanafunzi wakiipinga serikali ya Kikwete, basi Mkuu wa chuo atachukua hatua ya kuwanyamazisha kwa nguvu akiogopa kuwa kikwete anaweza kung'oa kibarua chake hata kama wanafunzi wale wako sahihi. Ni muhimu wakumbuke kuwa Chuo kikuu kinaundwa na Wahadhiri, Wanafunzi, na Vyumba vya madarasa. Vitu vinginevyo vilivyoko chuo kikuu ni kwa ajili ya kusaidia Wahadhiri na Wanafunzi wakutanapo kwenye Vyumba vya Madarasa yao waweze kupanuana maarifa kwa ufanisi zaidi. Kwa sasa inaonekana kama vile Chuo Kikuu ni Viongozi!!
 
Unaombwa utoe ushauri wa jinsi ya kutatua matatizo ya elimu ya Juu nchini ili hatimaye:

a. Migomo isiyo ya lazima isitokee
b. Elimu ya Juu inapatikana kwa kila atakaye
c. Familia zinaweza kumudu elimu ya juu
d. Elimu ya Juu inakuwa ni ya kiwango cha juu katika ubora wake na kuandaa wanafunzi katika ushindani wa soko la ajira la kimataifa.
e. Kuwaandaa wanafunzi kuwa watafiti na kuchangia utaalamu wao katika mabadiliko ya jamii yetu.
f. Kujenga nidhamu ya kisomi nchini.

NB: Yawezekana kuna kaubaguzi ka aina fulani hapa kwa kufocus kwenye elimu ya juu tu. Mniwie radhi.
you're simply sick
 
Kwa ufupi hapa naona kuna tatizo katika mfumo wa Elimu ya juu.Unapoweka msisitizo elimu sekondari halafu mambo yanakuwa kinyume elimu ya juu maana yake unataka kujenga Taifa la wasomi wa kidato cha sita! Naamini tupo watanzania wengi wenye mawazo yanayoweza kubadilisha mfumo wa elimu ila Kwa makusudi kabisa serikali yetu ama imekosa vipaumbele na kutotambua umuhimu wa elimu au kwa makududi wanashuhudia elimu yetu ikididimia kwa sababu wao 'haiwahusu'. Nionavyo mimi wadau wa elimu kwa Tazania hii ikijumuisha maprofesa,waalimu,watu binafsi,mashirika ya elimu,viongozi wa dini,wanafunzi na wazazi kwa pamoja wangekaa chini kufanya mchanganuo wa mfumo wa elimu ya juu unaoendana na mazingira yetu kwa maslahi ya taifa!Matokeo ya mfumo huo yapelekwe serikalini kwa utendaji na kama serikali itaamua kuyatupilia mbali basi kinachofuata: MAPINDUZI!!!.

Hatuwezi kuwa na taifa la migomo kila siu wakati sababu halisi ya matatizo yetu yanatambulika na yanatatulika.
Kwa sababu ya migomo vyuo vitano vipo nyumbani(UDSM,DUCE,MUCE,UCLAS na SUA-MAZIMBU) Walimu wataanza wakwao jumatatu.
Nafikiri serikali inatambua kwamba watu wanahitaji haki zao lakini inataka wagome kwanza ili pengine ithibishe kama wanazitaka kweli ndo watoe!
 
Katika michango yote hapa nimeona Augustine Moshi na Kichuguu wamegusia kitu nilichokifikiria pia: Role of the state/serikali.

Watu wanagoma wanapoona hakuna uwazi au uwajibikaji wa mamlaka husika(serikali).

Serikali ije na mipango ya kutusadikisha/inayoeleweka juu ya uendeshaji wa elimu ya juu. Baba akimwambia mtoto wake hatuna chakula cha kutosha hapa nyumbani; na mtoto akaona mle ndani yamebaki matembele kidogo na sembe kidogo kama chakula chao wote, ni rahisi kuamini; kuliko baba anayeropoka hivyo akiwa ameutwika, baada ya kula mipaja ya kuku, akiwa na machangudoa huko baa.
 
Nimependa sana jinsi Augustine Moshi alivyochangia. Big up man. Amejaribu sana kuwa short and precise. Sio story nyingi zisizo na mchango wowote wa kuzingatia hali halisi ya uchumi wa nchi. Migomo kwenye elimu ya juu itaendelea tu kama hatutabadilisha mifumo mibovu ya utawala wa CCM. Kama tukiendelea kuichagua CCM katika nafasi za ubunge, tusitarajie jipya lolote. Watanzania watashindwa kuchangia elimu maana serikali yao imeoza na jasho lao linaliwa na wachache. Kila mtu hawezi kupata elimu ya juu kutokana na kipato kibovu, pamoja na kutokuwa na uwezo wa kiakili wa kusoma hiyo elimu ya juu. Nchi haiwezi kuwa na wasomi katika mifumo mibovu kama ya sasa. Wasomi wachache walioko wanakimbilia kwenye siasa maana kwenye usomi wao hakuna kuthaminiwa wala malipo yanayoendena na elimu yao. Its a shame kukuta Professor mzima anapakia daladala na wanafunzi. Hapa elimu inaonekana haina maana hata kwa sisi tunaotaka kwenda chuoni. Wasomi hawathaminiwi. Nchi inaendeshwa na wanasiasa wenye uchu na matumbo yao.

Kwa kifupi ni kwamba, ili uweze kujibu hayo maswali ya Mwanakijiji, ni muhimu kukumbuka mazingira na utawala wa nchi. Nchi imekosa utawala makini ndio maana hayo yote yanatokea. Tukitaka majibu basi, ni muhimu kubadilisha utawala ulioko madarakani for 40 years. Nikiwa na maana kwamba no more CCM.
 
Back
Top Bottom