Ungewapa ushauri gani hawa?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Unaombwa utoe ushauri wa jinsi ya kutatua matatizo ya elimu ya Juu nchini ili hatimaye:

a. Migomo isiyo ya lazima isitokee
b. Elimu ya Juu inapatikana kwa kila atakaye
c. Familia zinaweza kumudu elimu ya juu
d. Elimu ya Juu inakuwa ni ya kiwango cha juu katika ubora wake na kuandaa wanafunzi katika ushindani wa soko la ajira la kimataifa.
e. Kuwaandaa wanafunzi kuwa watafiti na kuchangia utaalamu wao katika mabadiliko ya jamii yetu.
f. Kujenga nidhamu ya kisomi nchini.

NB: Yawezekana kuna kaubaguzi ka aina fulani hapa kwa kufocus kwenye elimu ya juu tu. Mniwie radhi.
 
Now you're trying to be funny.....
 
Kwa mtazamo wangu,
a. Migomo isiyo ya lazima isitokee
-- Sisi kama wazazi tunaangusha watoto wetu hatuwafundishi mentality ya kujitegemea wakati wanakua. Mtoto likizo kazi kuzurura au kukaa tu nyumbani na kusubiri kulipiwa kila kitu. Inabidi mentality ya kijamaa itoke kwenye jamii yetu watu wawe watafutaji (wazazi kwa watoto) ili mtoto hadi anafika chuo kikuu anajua thamani ya elimu anayotafuta na ugumu wa maisha yalivyo hivyo kama haki yake atadai kwa nguvu lakini atajua na waibu wake. Utakuta sehemu kama cafeteria pale wanawahudumu ambao sio wanafunzi sasa nini kinazuia mwanafunz mmoja kuomba kazi hata shift ambayo hana vipindi. Vijana wetu wakifika chuo kikuu status quo inawaharibu utakuta mda wanao wakutosha lkn ukifika mtihani hawajajiandaa kwahiyo wanadesa lkn mi naona yote hii ni kwasababu tu hawakujifunza jinsi ya kutafuta kitu katika life.

-- Wanafunzi wa vyuo vikuu wajue wameenda pale kutafuta maisha sio "Sunday School", so time is of the essence especially to them maana ulimwengu na opertunities havisubiri mtu. Ukiangalia vijana wetu wengi siku hizi wanaona chuoni ni kama sehemu ya kukulia kwahiyo wakipata tatizo tu huwa wana option mbili moja kuongea na uongozi wakikataliwa wanachotaka wanagoma.

b. Elimu ya Juu inapatikana kwa kila atakaye
-- Kila anayetaka awe tayari kuitafuta, kama mtu anajua kuwa mwaka flani mwanangu atakuwa anaingia chuo kikuu na zitahitajika kiasi fulani kwa ajili ya 40% ya mkopo atatafuta. Kwa wale wasio na uwezo wengine watakosa wengine waende kwenye vyuo ambavyo vitawawezesha kujitegemea mapema zaidi. Tatizo la wengi wetu watanzania kujituma na kujitegemea kudogo kila mtu anataka akaajiliwe akitoka chuo kikuu. Familia zifanye strategic planning badala ya kumsomesha mtu diploma ya banking waangalie uwezekano wa yeye kusomea FTC au kitu kama hicho ambacho akitoka hapo anaweza hata kutengeneza vigoda au akajiingiza kwenye shughuli za ujenzi ambazo asilimia kubwa zinafanywa na watu wasio na ujuzi huo kwahiyo atakuwa na advantage huko.

-- Tujidai kuwa wakati tunapata uhuru nchi nzima ilikuwa haina uwezo wa kujisomesha, then serikali ikaja ikasomesha watu, sasa hawa waliosomeshwa tulitarajia wao ndio wawe washauri wazuri wa ndugu zao (watoto, wajomba,shangazi) waliobaki kule kijijini au katika hali ya umaskini. Lakini hamna kitu kama hicho hadi leo wanafunzi wetu wanafikiria kama walivyokuwa wanafikiria wanafunzi wa mwaka 1990, ukiangalia kisa ni umimi. Wale waliosoma hawakuweza kuwashauri wenzao (ambao ni ndugu zao) kwamba nyakit zinabadilika na approach kwenye elimu ibadilike. Ukiangalia vitu walivyogomea watu mwaka 1992 ndio hivyo hivyo wanavyogomea mwaka huu hii inaonyesha watu waliomaliza toka mwaka huo 1992 walipoingia serikalini au makazini walijitoa kuwa wadau waelimu ya juu. Yaani kwasababu wao washapita sio tatizo lao tena maana kama wasingekuwa wa mimi aidha sera zingebadilika au mtazamo wa jamii ungebadilika.

c. Familia zinaweza kumudu elimu ya juu
----Huku Ulaya utakuta mtoto anazaliwa na mzazi anafikiria mwanangu ataendaje chuo kwahiyo wanaanza savings kwa ajili ya kitu kama hicho, huku kwetu wat wengi watasingizia umaskini lakini ukweli ni kwamba ndio maskini wapo lakini kuna sehemu kubwa tu jamii wanaofanya mambo ambayo sio lazima (mfano baba kila siku lazima apitie kilabuni na kupata fegi moja mbili) ambapo kama angekuwa na mipango na marengo bora ya kusomesha mwanae engepunguza vitu visivyo lazima. Ni jukumu letu kama wazazi kuanza kujipoanga mapema, wale wanaoshindwa kabisa watakuwepo na hawakosi katika kila jamii. Kwahiyo wenye uwezo wakiweza kutafuta vyao ndio tutapata nafasi ya kuwa identify na kuwasaidia wasio nauwezo. Tatizo lililopo sasa hivi wakati wa mgomo wote wanajiita watoto wa wakulima lkn ukiangalia maisha wanyoishi wakiwa na fedha utakuta 10% au zaidi ndo wanaishi kama watoto wa wakulima walio vyuo vikuu.

Kwasasa ni hayo tu mzee
 
Mndundu, safi kabisa; nashukuru kwa majibu yako murua. Umenipa mawazo mazuri sana na umeniangazia kwenye masuala fulani. Nasubiri wengine ambao wanaweza kugonganisha vichwa kwenye mada nzito.
 
Niseme kaneno kuhusu hili:

e. Kuwaandaa wanafunzi kuwa watafiti na kuchangia utaalamu wao katika mabadiliko ya jamii yetu

Ni aibu leo kwenye blog ya Michuzi au kwingineko mtu akiweka picha ya mhitimu wa udaktari wa filosofia atatukwana na kubezwa na pengine kupongezwa na watu wawili tu. Lakini weka picha ya atokaye Big brother Africa au mrembo anayerudi kutoka katika mashindano ya urembo utaona hata Mawaziri na Maofisa wetu wa serikali wanavyokuwa wa kwanza kuwapokea watu wa namna hiyo kuanzia Airport!

Ifike mahala tujenge utamaduni wa kuwatuza kwa nguvu wanaotaka kufanya tafiti na pengine kumpongeza rasmi kiserikali kila mtu anayehitimu kwenye level hiyo ya PhD na Thesis zao zipatikane na kutafsiriwa kwa kiswahili na kupitiwa kwa minajili ya kupokea mapendekezo kutokana na matokeo ya chambuzi hizo za tafiti za kisayansi katika idara/wizara husika. Unajua wazazi na hata vijana huona wapi kuna msukumo na mvuto na wakaelekea huko. The push & pull factors zikiwa ni katika ndombolo kama ilivyo kuwa Zaire (enzi zile) kila mtoto aliota siku moja kuimba au kucheza mziki katika kadamnasi na sio kusoma!

Kuanzia sasa tutilie mkazo uanzishwaji na uendelezaji wa Taasisi za utafiti na vyuo vikuu vya sayansi asilia (natural sciences) na teknolojia na siyo kukimbilia tu vile vyenye vitivo vya Arts, humanities etc
 
Unaombwa utoe ushauri wa jinsi ya kutatua matatizo ya elimu ya Juu nchini ili hatimaye:

a. Migomo isiyo ya lazima isitokee
b. Elimu ya Juu inapatikana kwa kila atakaye
c. Familia zinaweza kumudu elimu ya juu
d. Elimu ya Juu inakuwa ni ya kiwango cha juu katika ubora wake na kuandaa wanafunzi katika ushindani wa soko la ajira la kimataifa.
e. Kuwaandaa wanafunzi kuwa watafiti na kuchangia utaalamu wao katika mabadiliko ya jamii yetu.
f. Kujenga nidhamu ya kisomi nchini.

NB: Yawezekana kuna kaubaguzi ka aina fulani hapa kwa kufocus kwenye elimu ya juu tu. Mniwie radhi.

Mchango wangu mdogo tu.
What do you guys think about that "ordering"? Suppose we reverse the order,

f. Kujenga nidhamu ya kisomi nchini.
e. Kuwaandaa wanafunzi kuwa watafiti na kuchangia utaalamu wao katika mabadiliko ya jamii yetu.
d. Elimu ya Juu inakuwa ni ya kiwango cha juu katika ubora wake na kuandaa wanafunzi katika ushindani wa soko la ajira la kimataifa.
c. Familia zinaweza kumudu elimu ya juu
b. Elimu ya Juu inapatikana kwa kila atakaye
a. Migomo isiyo ya lazima isitokee

Sijaridhika kabisa na hoja zilizotolewa na wanachuo. Bila kubadili madai yao (labda kuongeza), wangeweza kuwa na hoja yenye kustahili kusikilizwa.

.
 
c. Familia zinaweza kumudu elimu ya juu
----Huku Ulaya utakuta mtoto anazaliwa na mzazi anafikiria mwanangu ataendaje chuo kwahiyo wanaanza savings kwa ajili ya kitu kama hicho, huku kwetu wat wengi watasingizia umaskini lakini ukweli ni kwamba ndio maskini wapo lakini kuna sehemu kubwa tu jamii wanaofanya mambo ambayo sio lazima (mfano baba kila siku lazima apitie kilabuni na kupata fegi moja mbili) ambapo kama angekuwa na mipango na marengo bora ya kusomesha mwanae engepunguza vitu visivyo lazima. Ni jukumu letu kama wazazi kuanza kujipoanga mapema, wale wanaoshindwa kabisa watakuwepo na hawakosi katika kila jamii. Kwahiyo wenye uwezo wakiweza kutafuta vyao ndio tutapata nafasi ya kuwa identify na kuwasaidia wasio nauwezo. Tatizo lililopo sasa hivi wakati wa mgomo wote wanajiita watoto wa wakulima lkn ukiangalia maisha wanyoishi wakiwa na fedha utakuta 10% au zaidi ndo wanaishi kama watoto wa wakulima walio vyuo vikuu.

Kwasasa ni hayo tu mzee

Wapo wazai ambao wanawasomesh watoto wao katika shule za sekondari binafsi ambazo viwango vyake vya ada vinazidi hiyo asilimia ambayo wanatakiwa kulipa elimu ya juu. Ajabu ni kuwa kama walimudu sekondari, umasikini wao umeanza lini kiasi kwamba wanashindwa kulipa elimu ya juu?
Hapa ina maana kuwa tatizo hili linaweza kusa si tu ni la wanafunzi, bali linaanza kwa wazazi na wanafunzi wanatumwa na wazazi wao kugoma kwa sababu wao (wanafunzi) sio wanaolipa ada hiyo
 
Unaombwa utoe ushauri wa jinsi ya kutatua matatizo ya elimu ya Juu nchini ili hatimaye:

a. Migomo isiyo ya lazima isitokee
b. Elimu ya Juu inapatikana kwa kila atakaye
c. Familia zinaweza kumudu elimu ya juu
d. Elimu ya Juu inakuwa ni ya kiwango cha juu katika ubora wake na kuandaa wanafunzi katika ushindani wa soko la ajira la kimataifa.
e. Kuwaandaa wanafunzi kuwa watafiti na kuchangia utaalamu wao katika mabadiliko ya jamii yetu.
f. Kujenga nidhamu ya kisomi nchini.

NB: Yawezekana kuna kaubaguzi ka aina fulani hapa kwa kufocus kwenye elimu ya juu tu. Mniwie radhi.[/QUOTE]

KWANI WEWE ULIKUWA NA MAONI GANI?
 
Wapo wazai ambao wanawasomesh watoto wao katika shule za sekondari binafsi ambazo viwango vyake vya ada vinazidi hiyo asilimia ambayo wanatakiwa kulipa elimu ya juu. Ajabu ni kuwa kama walimudu sekondari, umasikini wao umeanza lini kiasi kwamba wanashindwa kulipa elimu ya juu?
Hapa ina maana kuwa tatizo hili linaweza kusa si tu ni la wanafunzi, bali linaanza kwa wazazi na wanafunzi wanatumwa na wazazi wao kugoma kwa sababu wao (wanafunzi) sio wanaolipa ada hiyo

hao hao walioweza kujilipia secondary wengi wao ndo wanaopata ile 80% naomba uelewe kuna wengi sana ambao wazazi wao hawajaweza hata kuwalipia ada ile ya 20,000 unapomwambia alipe 40% ni kama unamtukana hebu fikiria kama una watoto 4 wote wako chuo unawezaje kuwalipia wote au ndo kuanza kubagua aende wa kiume au wa kike! wakati nikiwachuo nilijihusisha sana na maswala ya wanafunzi pale UD na nimejionea mwenyewe watu bila boom kutoka wengi wao wanakuwa hawana hata cent ya kujinunulia chakula kuna mate wangu yeye alikuwa analisha na kusomesha wadogo wake kwa boom sasa ingekuwa kipindi hiki jamani hata chuo asingemaliza sasa hivi ni mtu mkubwa tu ila tungekuwa tumempoteza only kwa 40% issues, Mi nadhani ufuatiliaji wa mikopo ungefuatwa bado wangeweza kuzungusha hizo pesa na kusomesha wengine ni wasomi wangapi wamemaliza na wako willing kurudisha mikopo ili wenzao wasome??? juzijuzi nimeona Taasisi ya mikopo wametuma barua ofisini kwetu na walitoa kwenye gazeti makampuni ambayo hawajatuma majina ya wafanyakazi waliohitimu elimu ya juu watume majina na threats kibao mpaka leo ofisi yangu haijatuma na sijaona hatua yeyote iliyochukuliwa, angalieni background ya wale wenye mikopo ya 80% most of them walikuwa wanasoma shule za ada 1,000,000, na wala wasikatae maana mifano tunayo,
 
Kwa mtazamo wangu,
a. Migomo isiyo ya lazima isitokee
-- Sisi kama wazazi tunaangusha watoto wetu hatuwafundishi mentality ya kujitegemea wakati wanakua. Mtoto likizo kazi kuzurura au kukaa tu nyumbani na kusubiri kulipiwa kila kitu. Inabidi mentality ya kijamaa itoke kwenye jamii yetu watu wawe watafutaji (wazazi kwa watoto) ili mtoto hadi anafika chuo kikuu anajua thamani ya elimu anayotafuta na ugumu wa maisha yalivyo hivyo kama haki yake atadai kwa nguvu lakini atajua na waibu wake. Utakuta sehemu kama cafeteria pale wanawahudumu ambao sio wanafunzi sasa nini kinazuia mwanafunz mmoja kuomba kazi hata shift ambayo hana vipindi. Vijana wetu wakifika chuo kikuu status quo inawaharibu utakuta mda wanao wakutosha lkn ukifika mtihani hawajajiandaa kwahiyo wanadesa lkn mi naona yote hii ni kwasababu tu hawakujifunza jinsi ya kutafuta kitu katika life.

-- Wanafunzi wa vyuo vikuu wajue wameenda pale kutafuta maisha sio "Sunday School", so time is of the essence especially to them maana ulimwengu na opertunities havisubiri mtu. Ukiangalia vijana wetu wengi siku hizi wanaona chuoni ni kama sehemu ya kukulia kwahiyo wakipata tatizo tu huwa wana option mbili moja kuongea na uongozi wakikataliwa wanachotaka wanagoma.

b. Elimu ya Juu inapatikana kwa kila atakaye
-- Kila anayetaka awe tayari kuitafuta, kama mtu anajua kuwa mwaka flani mwanangu atakuwa anaingia chuo kikuu na zitahitajika kiasi fulani kwa ajili ya 40% ya mkopo atatafuta. Kwa wale wasio na uwezo wengine watakosa wengine waende kwenye vyuo ambavyo vitawawezesha kujitegemea mapema zaidi. Tatizo la wengi wetu watanzania kujituma na kujitegemea kudogo kila mtu anataka akaajiliwe akitoka chuo kikuu. Familia zifanye strategic planning badala ya kumsomesha mtu diploma ya banking waangalie uwezekano wa yeye kusomea FTC au kitu kama hicho ambacho akitoka hapo anaweza hata kutengeneza vigoda au akajiingiza kwenye shughuli za ujenzi ambazo asilimia kubwa zinafanywa na watu wasio na ujuzi huo kwahiyo atakuwa na advantage huko.

-- Tujidai kuwa wakati tunapata uhuru nchi nzima ilikuwa haina uwezo wa kujisomesha, then serikali ikaja ikasomesha watu, sasa hawa waliosomeshwa tulitarajia wao ndio wawe washauri wazuri wa ndugu zao (watoto, wajomba,shangazi) waliobaki kule kijijini au katika hali ya umaskini. Lakini hamna kitu kama hicho hadi leo wanafunzi wetu wanafikiria kama walivyokuwa wanafikiria wanafunzi wa mwaka 1990, ukiangalia kisa ni umimi. Wale waliosoma hawakuweza kuwashauri wenzao (ambao ni ndugu zao) kwamba nyakit zinabadilika na approach kwenye elimu ibadilike. Ukiangalia vitu walivyogomea watu mwaka 1992 ndio hivyo hivyo wanavyogomea mwaka huu hii inaonyesha watu waliomaliza toka mwaka huo 1992 walipoingia serikalini au makazini walijitoa kuwa wadau waelimu ya juu. Yaani kwasababu wao washapita sio tatizo lao tena maana kama wasingekuwa wa mimi aidha sera zingebadilika au mtazamo wa jamii ungebadilika.

c. Familia zinaweza kumudu elimu ya juu
----Huku Ulaya utakuta mtoto anazaliwa na mzazi anafikiria mwanangu ataendaje chuo kwahiyo wanaanza savings kwa ajili ya kitu kama hicho, huku kwetu wat wengi watasingizia umaskini lakini ukweli ni kwamba ndio maskini wapo lakini kuna sehemu kubwa tu jamii wanaofanya mambo ambayo sio lazima (mfano baba kila siku lazima apitie kilabuni na kupata fegi moja mbili) ambapo kama angekuwa na mipango na marengo bora ya kusomesha mwanae engepunguza vitu visivyo lazima. Ni jukumu letu kama wazazi kuanza kujipoanga mapema, wale wanaoshindwa kabisa watakuwepo na hawakosi katika kila jamii. Kwahiyo wenye uwezo wakiweza kutafuta vyao ndio tutapata nafasi ya kuwa identify na kuwasaidia wasio nauwezo. Tatizo lililopo sasa hivi wakati wa mgomo wote wanajiita watoto wa wakulima lkn ukiangalia maisha wanyoishi wakiwa na fedha utakuta 10% au zaidi ndo wanaishi kama watoto wa wakulima walio vyuo vikuu.

Kwasasa ni hayo tu mzee

Rudi Tanzania katembelee Vijijini mzee hela ya kula yenyewe hamna unaongelea kumlipia mtu ada,ya shule za msingi ada ilifutwa kwasababu watu walikuwa hawana hela ya kupeleka watoto shule sasa mzazi huyohuo akusanye 40% ya kumpeleka mtoto chuo kikuuu????
 
hao hao walioweza kujilipia secondary wengi wao ndo wanaopata ile 80% naomba uelewe kuna wengi sana ambao wazazi wao hawajaweza hata kuwalipia ada ile ya 20,000 unapomwambia alipe 40% ni kama unamtukana...

Sasa tukiamua kuwa wakweli, ukiangalia katika vyuo vikuu vyetu, ni percentage ngapi ya hao watanzania wasio na uwezo wana watoto wao vyuoni humo?
kama kuna wengine ambao waliweza kulipa sekondari na sasa wanapata 80% kwa nini nao wanagoma?
Anyway, tofauti hiyo ya vipato baina ya watanzanai ndiyo iliyosababisha serikali kuanzisha utaratibu wa means testing ili kila mwanafunzi/mzazi alipe kulingana na uwezo wake. Si kwamba wazazi wote wenye watoto vyuo vikuu ni masikini kama ambavyo wanafunzi waliogoma wanavyotaka tuamini
 
Unaombwa utoe ushauri wa jinsi ya kutatua matatizo ya elimu ya Juu nchini ili hatimaye:

a. Migomo isiyo ya lazima isitokee
b. Elimu ya Juu inapatikana kwa kila atakaye
c. Familia zinaweza kumudu elimu ya juu
d. Elimu ya Juu inakuwa ni ya kiwango cha juu katika ubora wake na kuandaa wanafunzi katika ushindani wa soko la ajira la kimataifa.
e. Kuwaandaa wanafunzi kuwa watafiti na kuchangia utaalamu wao katika mabadiliko ya jamii yetu.
f. Kujenga nidhamu ya kisomi nchini.

NB: Yawezekana kuna kaubaguzi ka aina fulani hapa kwa kufocus kwenye elimu ya juu tu. Mniwie radhi.

Ushauri wangu utalenga kwa wanafunzi.

Mwanafunzi lazima awe na malengo yake ya muda mfupi na muda mrefu na kuwa na mikakati ya kuyafikia.Lengo kuu la mwanafunzi liwe ni kusoma kwa bidii zote na kwa muda unaotakiwa ili kumaliza masomo kwa muda muafaka.Hii itafanikiwa tu kwa kujijengea nidhamu ya hali ya juu, ikiwa ni pamoja na kutambua uwezo wa wazazi na hata serikali kumsaidia afikie lengo kuu.

Kufuatana na majadiliano niliyoyafanya na baadhi ya wanafunzi inaelekea wako wanafunzi wanaoweka lengo kuu pembeni na kujali zaidi malengo ya muda mfupi ambayo si ya lazima sana kwa kipindi cha uanafunzi.Wapo wenye kudhani kuwa wakiwa chuoni wataweza kujipatia mali au vifaa kama magari, TV, kuvaa vizuri na kwenda na wakati ili pale amalizapo masomo awe amekamilika au pia kuwakoga wengine.Hii hupelekea kuanza kujiingiza kwenye vitendo visivyokubalika ambavyo si lazima kuvitaja hapa, lakini kubwa zaidi ni kuingiwa na jazba na hasira kuwa kiasi cha fedha inayotolewa kama mkopo hakitoshi.

Vile vile nimelinganisha na wale waliosoma zamani ( 80s-na kurudi nyuma) ambapo wao wanasema kuwa walisoma kwenye mazingira magumu - mfano UDSM kulikuwa na tatizo kubwa sana la maji, hivyo hali ya usafi kwenye halls of residence ilikuwa ni mbaya, fedha ya kujikimu ilikuwa kidogo mno kiasi kuwa ilikua haichukui hata wiki moja! chakula pia kilikuwa kibaya na mapungufu mengine. Pamoja na matatizo haya hawakuona kama migomo ingewatatulia matatizo yao.Lengo kuu la kumaliza kwa wakati lilikuwa ndio muhimu zaidi na waliweka nidhamu mbele zaidi.

Ni jukumu la mwanafunzi na wazazi kushirikiana ili kumfanya mwanafunzi afikie lengo.Pia kama kuna matatizo, migomo au vurugu hazitaleta ufumbuzi wa haraka bali vitachangia kumuathiri zaidi mwanafunzi hasa anayetoka familia maskini.

Kwa kulalamika na hata kugoma, ni kweli Serikali itakuwa imepata changa moto kuangalia kwa undani tatizo hili lakini hadi hapo ufumbuzi utakapopatikana, hailipi kufanya vurugu.
 
Rudi Tanzania katembelee Vijijini mzee hela ya kula yenyewe hamna unaongelea kumlipia mtu ada,ya shule za msingi ada ilifutwa kwasababu watu walikuwa hawana hela ya kupeleka watoto shule sasa mzazi huyohuo akusanye 40% ya kumpeleka mtoto chuo kikuuu????[/QUOTE]

Hiyo ada kwanza ni kiasi gani KWA MWAKA? Nimeambiwa ni kama 600,000/=( haizidi milioni moja).Tuchukulie kuwa ada ni hiyo kweli kama mtu ( mwanafunzi au mzazi) anapanga vizuri kuhusu masomo ya juu hawezi kuweka akiba ya kama 200,000/=? tuwe realistic jamani!Sikatai kuwa kuna watakaokosa hicho kiasi.Lakini hao ni exception na bado ziko namna za kuwasaidia.Najaribu kuwa objective badala ya kulalamika tu na kulaumu.
Kuna mtu aliwahi kusema " If u think education is expensive, then try ignorance" SAMAHANINI LAKINI!
 
Wapo wazai ambao wanawasomesh watoto wao katika shule za sekondari binafsi ambazo viwango vyake vya ada vinazidi hiyo asilimia ambayo wanatakiwa kulipa elimu ya juu. Ajabu ni kuwa kama walimudu sekondari, umasikini wao umeanza lini kiasi kwamba wanashindwa kulipa elimu ya juu?
Hapa ina maana kuwa tatizo hili linaweza kusa si tu ni la wanafunzi, bali linaanza kwa wazazi na wanafunzi wanatumwa na wazazi wao kugoma kwa sababu wao (wanafunzi) sio wanaolipa ada hiyo

Hapa unanikumbusha ule wakati ambapo serikali ilikuwa inapandisha bei za bidhaaa kwa vile tu wananchi walimudu bei ya kuruka.

Hoja iliyotolewa imeachwa wazi na hivyo kuwa pana ktk kuijadili,mimi nafikiria tuchukue mtanzania ambaye mshahara wake kwa mwezi ni 300,000/= anaishi sehemu yoyote ile ya tanzania mwenye familia ya watoto wawili.je atamudu hizi gharama za maisha.ikiwa ni pamoja na kugharamia masomo ya juu kwa kumlipia huyo mtoto mmoja hapo chuo kikuu.

Kwa upande wangu matatizo mengi yanachangiwa na utawala wa vyuo na ubinafusi wa watawala wetu kwa kuto kujua au kuto kujiamini ktk maamuzi yanayo husu jamii.
 
Sasa tukiamua kuwa wakweli, ukiangalia katika vyuo vikuu vyetu, ni percentage ngapi ya hao watanzania wasio na uwezo wana watoto wao vyuoni humo?
kama kuna wengine ambao waliweza kulipa sekondari na sasa wanapata 80% kwa nini nao wanagoma?
Anyway, tofauti hiyo ya vipato baina ya watanzanai ndiyo iliyosababisha serikali kuanzisha utaratibu wa means testing ili kila mwanafunzi/mzazi alipe kulingana na uwezo wake. Si kwamba wazazi wote wenye watoto vyuo vikuu ni masikini kama ambavyo wanafunzi waliogoma wanavyotaka tuamini

Mkuu tatizo la kimsingi hapo ni kwamba means testing haifanyiki inavyotakiwa na hamna data zinazoamua nani apate asilimia ngapi. Zinazoletwa ni estimates tu na vilevile kuna dalili kwamba huenda wanaostimates wanainfluence katika maamuzi. Kwa mfano kuna familia ina watoto wawili auu watatu waliopo either kwenye chuo kimoja au tofauti unakuta mmoja anapewa 80% na mwingine anapewa 20% mwingine 60% sasa kwa akili ya kawaida unaweza kuamini kwamba information zilitafutwa?

Kuna double standards nyingi sana kwenye implementation za mipango yetu mingi sana nchi hii. Kila mpango au mradi unapoanza watu watakaoimplement wanaangalia nini watapata na wapi kuna udhaifu na wanapoona kila mtu anatumia kwa level yake ya utandaji.

Hao maafisa wakubwa ambao ndio wanatakiwa kuchangia zaidi utakuta wanapata either 100% au 80% hapo ndipo malalamiko yanapoanza na hatimaye migogoro inafuata.

Kungekuwa na data za kila mtu au familia then haya mambo yasingesumbua, malalamiko yakitokea watekelezaji wanatoa maelezo ya jinsi zoezi lilivyokwenda na waliostahili kupata walichopata principles na regulations zilifuatwa. Malalamiko ya watanzania siku zote ni jinsi wanavyopuuzwa na serikali yao kila jambo linafanyika bila kuhusishwa wanaletewa tu limeamuliwa wao watekeleze na utekelezaji unakuja kupindwa tena.

Mambo mengi tu! Imefikia hatua rais wao anaamua tu eti fungu la pesa za umma hizi peleka huku na hizi peleka kule bila hata kupitia kwenye bajeti. (eg EPA, TRL, safari ya mawaziri kutetea bajeti ya kifisadi etc)
 
hao hao walioweza kujilipia secondary wengi wao ndo wanaopata ile 80% naomba uelewe kuna wengi sana ambao wazazi wao hawajaweza hata kuwalipia ada ile ya 20,000 unapomwambia alipe 40% ni kama unamtukana hebu fikiria kama una watoto 4 wote wako chuo unawezaje kuwalipia wote au ndo kuanza kubagua aende wa kiume au wa kike! wakati nikiwachuo nilijihusisha sana na maswala ya wanafunzi pale UD na nimejionea mwenyewe watu bila boom kutoka wengi wao wanakuwa hawana hata cent ya kujinunulia chakula kuna mate wangu yeye alikuwa analisha na kusomesha wadogo wake kwa boom sasa ingekuwa kipindi hiki jamani hata chuo asingemaliza sasa hivi ni mtu mkubwa tu ila tungekuwa tumempoteza only kwa 40% issues, Mi nadhani ufuatiliaji wa mikopo ungefuatwa bado wangeweza kuzungusha hizo pesa na kusomesha wengine ni wasomi wangapi wamemaliza na wako willing kurudisha mikopo ili wenzao wasome??? juzijuzi nimeona Taasisi ya mikopo wametuma barua ofisini kwetu na walitoa kwenye gazeti makampuni ambayo hawajatuma majina ya wafanyakazi waliohitimu elimu ya juu watume majina na threats kibao mpaka leo ofisi yangu haijatuma na sijaona hatua yeyote iliyochukuliwa, angalieni background ya wale wenye mikopo ya 80% most of them walikuwa wanasoma shule za ada 1,000,000, na wala wasikatae maana mifano tunayo,

Mkuu mchago wako umenigusa sana. Mimi nilisoma sekondari za serikali (form 1-4 day; form 5-6 boarding) na mzazi wangu alishindwa kunilipia ada sh 70,000 (form 5-6) . Hiyo ada nilikuja kilipa mimi mwenyewe baada ya kumaliza chuo na kupata ajira. Fikiria mtoto wa mkulima (80%ya watanzania) nauli ya kwenda shule tu mzazi alikuwa anauza mbuzi! Je yule asiyekuwa hata na mbuzi wa kuuza inakuwaje? Inatia uchungu sana jamani.
Viongozi wengi waliopo madarakani sasa ni watoto wa wakulima na wamesomeshwa bure ila hawataki kuona na kuambiwa ukweli! Kama sio juhudi za mwalimu Nyerere, viongozi wengi wasingekuwepo hapo walipo. Hili swala la kuchangia gharama za elimu ya juu inabidi litazamwe upya vinginevyo watoto wa masikini wataendelea kuwa makondakta, housegirls/boys, vibaka,n.k.
 
Ni aibu leo kwenye blog ya Michuzi au kwingineko mtu akiweka picha ya mhitimu wa udaktari wa filosofia atatukwana na kubezwa na pengine kupongezwa na watu wawili tu. Lakini weka picha ya atokaye Big brother Africa au mrembo anayerudi kutoka katika mashindano ya urembo utaona hata Mawaziri na Maofisa wetu wa serikali wanavyokuwa wa kwanza kuwapokea watu wa namna hiyo kuanzia Airport!

Tukiwa na alau vichwa vichache vya aina hii nchi yetu itasogea. Thanks mkuu!
 
katika haya mapendekezo mnayosema ni yapi tunaweza kuyaweka katika sheria? Je bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu bado iendelee kuwa kama ilivyo au inahitaji mabadiliko ya aina fulani kuendana na mapendekezo ambayo mnayatoa?
 
Niseme kaneno kuhusu hili:

Ni aibu leo kwenye blog ya Michuzi au kwingineko mtu akiweka picha ya mhitimu wa udaktari wa filosofia atatukwana na kubezwa na pengine kupongezwa na watu wawili tu. Lakini weka picha ya atokaye Big brother Africa au mrembo anayerudi kutoka katika mashindano ya urembo utaona hata Mawaziri na Maofisa wetu wa serikali wanavyokuwa wa kwanza kuwapokea watu wa namna hiyo kuanzia Airport!

Ifike mahala tujenge utamaduni wa kuwatuza kwa nguvu wanaotaka kufanya tafiti na pengine kumpongeza rasmi kiserikali kila mtu anayehitimu kwenye level hiyo ya PhD na Thesis zao zipatikane na kutafsiriwa kwa kiswahili na kupitiwa kwa minajili ya kupokea mapendekezo kutokana na matokeo ya chambuzi hizo za tafiti za kisayansi katika idara/wizara husika. Unajua wazazi na hata vijana huona wapi kuna msukumo na mvuto na wakaelekea huko. The push & pull factors zikiwa ni katika ndombolo kama ilivyo kuwa Zaire (enzi zile) kila mtoto aliota siku moja kuimba au kucheza mziki katika kadamnasi na sio kusoma!

Kuanzia sasa tutilie mkazo uanzishwaji na uendelezaji wa Taasisi za utafiti na vyuo vikuu vya sayansi asilia (natural sciences) na teknolojia na siyo kukimbilia tu vile vyenye vitivo vya Arts, humanities etc

On top of that:
Ni rahisi kwa Mtanzania yeyote kuchangia Harusi Birthday au Kitchen Party kuliko kuchangia juhudi zozote zile za kumpeleka Binamu yake kidato cha kwanza,kidato cha tano au University.

Mtanzania anaweza na yuko tayari kuchangia 100,000.00 na kujitolea muda wake kufanikisha Kitchen party hata mara 4 kwa mwaka.
Lakini ni mtanzania huyo huyo akiombwa achangie 30,000.00 mara moja kwa mwaka kusaidia mpwa wake aende kidato cha tano yuko tayari hata kula wembe na kujikata ulimi kuliko kusaidia juhudi zozote za kumwelimisha kinda huyu.

Utasikia akisema hivi huku akisonya kwa hasira na uchungu,

"Eti nichangie 30,000! Wanawazimu kweli hawa, kazi kuzaana kama mipanya buku tu halafu sisi wengine tuumie kuchangia bila faida".
"Watakoma kulinga"

Lakini Mtanzania huyu huyu anayekataa kumchangia mpwa wake 30,000 tu ili aende High School yuko tayari kuchangia harusi ya mpwa wake huyohuyo jumla ya 100,000, mbuzi wawili na kujitolea mkweche wake siku nzima ya harusi.

Kifupi ni kwamba Watanzania tuna Priority za ajabu sana, hata ibilisi huko kuzimu anatushangaa. Mniwie radhi.
 
Back
Top Bottom