Ungepewa milioni 12 uwekeze, ungefanya uwekezaji gani? Wafanyabishara waheshimiwe, ajira ni bora zaidi ya biashara

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,675
Wafanyabishara wote, na wapambanaji wote walioweza kutoka chini, bila kitu na wakafanikiwa kuona Mwanga, aisee ukimpita mtu wa hivyo jaribu kumheshimu sana maana hustling zake sio za kitoto.

Nimeelewa kwanini Baba yangu alikuwa ananikazania nisome, biashara sio kwa ajili ya watu dhaifu, ila ajira ndio wamejaa watu dhaifu zaidi, kwanini nimesema hivyo?

Kusoma kuajiriwa na kulipwa mshahara hakuna maajabu zaidi maana unauza ujuzi unabadilishana na pesa, kwahiyo pesa zinaflow tu bila hata ya kuumiza kichwa, pesa za wizi, n.k lakini biashara unaweza umiza kichwa mara kumi na usitoboe.

Brother wangu, anataka kunikopa mtaji wa million 12 na kanipa miezi 6 ya kupambana, baada ya miezi sita ikishapita inabidi kila mwezi nimtumie laki 5 mpaka hela yake yote itimie.

Sasa hizi hela za ndugu ni za lawama aisee na sitaki kumdissapoint kabisa, Dar es Salaam siwezi enda maana niliingia kichwa kichwa nikapigwa za uso nikatoka nduki sitaki kurudi tena.

Nipo Kigoma maeneo ya Kasulu hapa, kichwa kinawaka moto kweli, nawaza niingie vijijini nikanunue maharage nikaweke stoo, lakini naona kama risk ni kubwa na faida kidogo, nikawaza niende Mpanda huko wakati wa mavuno ya mpunga nikatupie hela huko wakati naendelea kuwaza niifanyie nini.

Hivi wazee ungekuwa wewe umepewa hiyo hela ungeitumbukiza sehemu gani ikupe faida?.
 
Nilipoona umeandika ajira ni bora zaidi ya biashara nimekushangaa sana.

Unamaanisha hizi ajira za mishahara ya 585,000 na 765,000 au 1.3m hadi 3.3m ni bora?

Akili kama hizi kutoboa ni ndoto
Soma tena mkuu, shida ni kukuza hela mfano upewe million 20 then uambiwe baada ya mwaka nataka milioni 25, hapo ndio lazima kichwa kipate moto.
 
Tunanunulia wapi na kuuzia wapi mkuu? Details muhimu
Kwa hio hela yako tununulie tu Dakawa Morogoro kuepusha gharama kubwa za usafiri, Mbuzi kama 70 hivi za 50-65, hio hela ita double chap kwa haraka.

Me nakushauri, wewe kaa kwanza na hela yako, uje uwe kama saidia mtu anayefanya hizo biashara kwa gharama zako kwa muda wa hata miezi miwili, then ndo uanze.

Kuna vitu unatakiwa ujifunze kwanza kabla hujaanza kufanya, mathalani uchaguzi wa mbuzi mzuri na bei zake uzijue kulingana na ukubwa wa mbuzi.
 
Kwa hio hela yako tununulie tu Dakawa Morogoro kuepusha gharama kubwa za usafiri, Mbuzi kama 70 hivi za 50-65, hio hela ita double chap kwa haraka.
Me nakushauri, wewe kaa kwanza na hela yako, uje uwe kama saidia mtu anayefanya hizo biashara kwa gharama zako kwa muda wa hata miezi miwili, then ndo uanze. Kuna vitu unatakiwa ujifunze kwanza kabla hujaanza kufanya, mathalani uchaguzi wa mbuzi mzuri na bei zake uzijue kulingana na ukubwa wa mbuzi.
Ni kweli, kila kitu kinaanzia kwenye elimu fasaha
 
Ni kweli, kila kitu kinaanzia kwenye elimu fasaha
Yes, knowledge ndo kila kitu kwenye biashara na mentors wazuri mzee. Maana kuna muda market haieleweki ila kama una mentor mzuri anakuokoa kabisa una clear stock kwa wakati. Ufugaji unalipa sana yaani, ingekuwa anakupa free hizo 12M ni zako, hakuna cha marejesho, ningekwambia ufuge na broilers na kuku wa mayai layers. Utajiri nje nje mwanangu. Anyways, soma maoni ya wadau alafu utaona mwenyewe where to invest yourself. Ukumbuke tu kwamba hakuna biashara ambayo haina hasara, uvumilivu na juhudi ku minimize vitu vinavyokutia hasara ndo key to success.
 
Wafanyabishara wote, na wapambanaji wote walioweza kutoka chini, bila kitu na wakafanikiwa kuona Mwanga, aisee ukimpita mtu wa hivyo jaribu kumheshimu sana maana hustling zake sio za kitoto.

Nimeelewa kwanini Baba angu alikua ananikazania nisome, biashara sio kwa ajili ya watu dhaifu, ila ajira ndio wamejaa watu dhaifu zaidi, kwanini nimesema hivyo?

Kusoma kuajiriwa na kulipwa mshahara hakuna maajabu zaidi maana unauza ujuzi unabadilishana na pesa, kwahiyo pesa zinaflow tu bila hata ya kuumiza kichwa, pesa za wizi, n.k lakini biashara unaweza umiza kichwa mara kumi na usitoboe.

Brother wangu, anataka kunikopa mtaji wa million 12 na kanipa miezi 6 ya kupambana, baada ya miezi sita ikishapita inabidi kila mwezi nimtumie laki 5 mpaka hela yake yote itimie.

Sasa hizi hela za ndugu ni za lawama aisee na sitaki kumdissapoint kabisa, daresalam siwezi enda maana niliingia kichwa kichwa nikapigwa za uso nikatoka nduki sitaki kurudi tena.

Nipo kigoma maeneo ya kasulu hapa, kichwa kinawaka moto kweli, nawaza niingie vijijini nikanunie maharage nikaweke stoo, lakini naona kama risk ni kubwa na faida kidogo, nikawaza niende Mpanda huko wakati wa mavuno ya mpunga nikatupie hela huko wakati naendelea kuwaza niifanyie nini.

Hivi wazee ungekua wewe umepewa hiyo hela ungeitumbukiza sehemu gani ikupe faida?.
Endelea kutafuta ajira uajiriwe na achana na biashara maana ushaweka negativity so imekuakaa akilini kuwa biashara ni ngumu na hautakuja kufanikiwa...it seems unataka mafanikio ya haraka and maybe ndo mana mara ya kwanza ulikula za uso
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom