Ungamo la kishetani!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ungamo la kishetani!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dark City, Aug 18, 2011.

1. Dark City

Dark City JF-Expert Member

#1
Aug 18, 2011
Joined: Oct 18, 2008
Messages: 16,277
Likes Received: 241
Trophy Points: 160
Can this be really? To me, ni ungamo la kiibirisi!!  KAMA WEWE NDIO MUMEO UNAFANYAJE??
Mke wangu mpendwa!
Nimekuwa nikiandamwa na msongo wa mawazo siku za karibuni kwa kuwa sasa nadhani nimefikia mwisho sina budi kukueleza aina ya mume uliyekubali kuwa naye hadi mungu atakapo tutenganisha. Najua wewe ni mpole na mvumilivu lakini ninayokwenda kuyasema ni mazito sana kwa moyo wa mwanadamu hivyo usinionee huruma kwa uamuzi utakao uchukua kwani tayari nimeukubali kabla sijaujua. Sijajua kosa ulilolifanya hadi kupewa adhabu ya mume kama mimi ila ninaamini aliyekuadhibu akiyasikia haya basi atakuandalia pepo yako mbinguni kwa kuwa umekwisha onja kiama hapa duniani, mke wangu:-

1. Yule mtoto wa shangazi yako ninayemsomesha sifanyi hayo kwa mapenzi yangu kwako bali ninaficha ubaya tunaokufanyia, nimekuwa na uhusiano usiofaa na binti huyu tangu alipovunja ungo, miaka nane iliyopita.
2. Msichana wa kazi uliyemfukuza kwa kuwa na ujauzito tukagombana sana na nilikuita majina yote mabaya ni kwa kuwa nilikuwa najaribu kumlinda kwa kuwa sikuwa na uhakika kama hiyo mimba hainihusu kwa kuwa nimetembea naye miezi ile miwili uliyokwenda mafunzo south africa.
3. Nyumba unayoisifia sana aliyopanga shoga yako Suzzy wa Sinza, ninalipia mimi kodi na nimekuwa na uhusiano wa siri na rafiki yako Suzzy tangu mkiwa pamoja chuo kikuu.
4. Ugomvi mara kwa mara ndani ya nyumba yetu mara zote huwa naupanga ili kuficha maovu yangu.
5. Mke wangu sijawaji kukumbuka birthday yako hata siku moja ila ninaambiwa na rafiki yako Suzzy.
6. Hata tabia ya kwenda Bar si kwa sababu ya kukutana na marafiki bali ni tabia yangu mbaya ya kupenda kuwashika shika makalio na matiti ma bar maid.
7. Kinachonipeleka salon kufanya scrub si usafi mke wangu bali ni tamaa ya kushikwa shikwa na kutekenywa na wasichana wadogo wa salon, hii ndio sababu mara zote unaponunu dawa za scrub nyumbani nazipoteza au nasingizia zinanitoa chunusi.
8. Mke wangu mimi sio shabiki kabisa wa mpira bali huwa nasingizia kupenda ili nilpate uhuru wa kutumia muda mwingi nje ya nyumbani.
9. Mke wangu yule personal trainer wa gym nilimuajiri pia kukuangalia, kukuchunguza na pia kukujaribu ili nipate visingizio vya kukuacha tangu miaka miwili iliyopita lakini sikufanikiwa na alichoniambia ndicho kimenifikisha kwenye ungamo hili.
10. Mke wangu pete yangu ya harusi haikupotea bali niliigawa kwa rafiki yako Suzzy

2. bht

bht JF-Expert Member

#2
Aug 18, 2011
Joined: May 14, 2009
Messages: 10,341
Likes Received: 209
Trophy Points: 160
It can't be!
ndo pa kuparalaizi mwili na roho hapo....

3. Bujibuji

Bujibuji JF-Expert Member

#3
Aug 18, 2011
Joined: Feb 4, 2009
Messages: 35,396
Likes Received: 22,273
Trophy Points: 280
Atakujibu nakupenda mume wangu.
Endelea tu na tabia zako.

4. bht

bht JF-Expert Member

#4
Aug 18, 2011
Joined: May 14, 2009
Messages: 10,341
Likes Received: 209
Trophy Points: 160

Umenikumbusha wimbo wa Lady Jay Dee....mume anaungama yooote, mke anasema anampenda...

5. Henge

Henge JF-Expert Member

#5
Aug 18, 2011
Joined: May 14, 2009
Messages: 6,767
Likes Received: 78
Trophy Points: 145
duuuu aiseee hii kali lakini kwa kuwa alivumilia wakati hujaungama kwa nini asikuvumilie sasa!
TENA UTAZIDISHA UPENDO WAKE KWAKO!

6. Mr Rocky

Mr Rocky JF-Expert Member

#6
Aug 18, 2011
Joined: Oct 10, 2007
Messages: 15,186
Likes Received: 570
Trophy Points: 280
Mhhh hapo ahhh sidhani kama mke atakuw ana guts za kuendelea na ndoa hiyo

7. Smile

Smile JF-Expert Member

#7
Aug 18, 2011
Joined: Jul 18, 2011
Messages: 15,427
Likes Received: 194
Trophy Points: 160
Uupuuzi

8. Mr Rocky

Mr Rocky JF-Expert Member

#8
Aug 18, 2011
Joined: Oct 10, 2007
Messages: 15,186
Likes Received: 570
Trophy Points: 280
Bebii mekumiss
unaona eeehhh haya mambo ya kijinga kabisa hayo

9. IGWE

IGWE JF-Expert Member

#9
Aug 18, 2011
Joined: Feb 3, 2011
Messages: 7,753
Likes Received: 1,326
Trophy Points: 280
wimbo mzuri sana ule....mwanamke ana mapenzi hata shetani angeogopa....'hawajui'

10. Lizzy

Lizzy JF-Expert Member

#10
Aug 18, 2011
Joined: May 25, 2009
Messages: 22,224
Likes Received: 244
Trophy Points: 160
Sasa hiyo ni ndoa au circus?‘

11. Vin Diesel

Vin Diesel JF Gold Member

#11
Aug 18, 2011
Joined: Mar 1, 2011
Messages: 8,402
Likes Received: 738
Trophy Points: 280
hapo ngoma itanoga na yeye akikushushia list ndefu uliyoshiba kuliko yako.

12. Mr Rocky

Mr Rocky JF-Expert Member

#12
Aug 18, 2011
Joined: Oct 10, 2007
Messages: 15,186
Likes Received: 570
Trophy Points: 280
Wanafanya act ya movie ya kuonyesha walimwengu

13. bht

bht JF-Expert Member

#13
Aug 18, 2011
Joined: May 14, 2009
Messages: 10,341
Likes Received: 209
Trophy Points: 160

Kumbe 'hawajui' ndo jina la wimbo eeh? Ngoja niusikilize

14. PakaJimmy

PakaJimmy JF-Expert Member

#14
Aug 18, 2011
Joined: Apr 29, 2009
Messages: 16,236
Likes Received: 309
Trophy Points: 180
Haya ndiyo yanayoendelea kwenye familia zetu nyingi sana, japo hapa tunafanya kama kushangaa!
Tena pengine tunafanya mazito zaid ya haya!
Imagine vitendo kama mfano abortion tunazofanya au kusaidia kuzifanya, kufukuzisha kazi wenzetu kwa makusudi, kugombanisha ndoa za marafiki etc!

Bora huyo jamaa ameamua kuweka hadharani aliyoyafanya, nadhani amedhamiria kuyaacha jumla.
Personally nachukulia hili kama ungamo la DHATI!
NAWASILISHA.

15. First Born

First Born JF-Expert Member

#15
Aug 18, 2011
Joined: Jul 11, 2011
Messages: 5,315
Likes Received: 96
Trophy Points: 145

si ndo ulichonipendea?

16. H

Hardwood JF-Expert Member

#16
Aug 18, 2011
Joined: Sep 21, 2010
Messages: 854
Likes Received: 481
Trophy Points: 80
Subiri kwanza yakukute ndio utajua ni upuuzi au laa!!!!

17. Gugwe

Gugwe Senior Member

#17
Aug 18, 2011
Joined: Jul 25, 2011
Messages: 126
Likes Received: 9
Trophy Points: 35
Lakini nahisi kuna maungamo mengi katika hayo yanatugusa wengi tu, lakini hatujakaa na kutafakari katika muelekeo wa maungamo

18. Chauro

Chauro JF-Expert Member

#18
Aug 18, 2011
Joined: Aug 20, 2010
Messages: 2,969
Likes Received: 16
Trophy Points: 135
Asante PJ kwa kusema ukweli huwa siwaelewi binadamu utafikiri huwa kuna viumbe wanatoka sayari nyingine kuja kufanya huu ushetani .

19. Mwendabure

Mwendabure JF-Expert Member

#19
Aug 18, 2011
Joined: Mar 10, 2011
Messages: 2,056
Likes Received: 300
Trophy Points: 180
Huyo mume atakuwa na anasumbuliwa na ugonjwa unaojulikana kitaalamu kama... Kitombicssana ambao unasababishwa na vijidudu wajulikanao kitaalamu kama Nyegelundopacs. Ugonjwa huo unashambulia sana wanaume wenye umri na kipato cha kati na kipato cha juu. Hasa wale wenye elimu zao, nyumba zao, wake zao (tena wenye kazi/kipato) na pesa zao ndo zinawapa jeuri.
Kapuku ni nadra kuugua ugonjwa huu.

Dk. Mwendabure!

20. Dena Amsi

Dena Amsi R I P

#20
Aug 18, 2011
Joined: Aug 17, 2010
Messages: 13,137
Likes Received: 255
Trophy Points: 160
Dah mie naweza zimia we DC wewe dah ngoja kwanza nivute pumzi halafu nirudi kukwambia ningejibu

Loading...