Karibu tena mkuu,
Nimependa namna ulivyojitolea kuwaelezea hawa Vijana wawili wa kisiasa ndnai ya CHADEMA.
Namimi nakuunga mkono mkuu kwamba wanatakiwa kutiwa moyo na kupewa nafasi zaidi ili wakieneze chama kwa mapana zaidi.
LAKINI MKUU,KATIKA UCHAMBUZI WAKO UMEAINISHA MAFANIKIO,CHANGA MOTO NA RAI YAKO KWA VIONGOZI WA CHADEMA.
Naomba niongeze hili katika uchambuzi wako,kwamba hawa vijana wawili wanaoonekana kushabihiana
WANAMAPUNGUFU HAYA HAPA,AMBAYO NI MUHIMU WAKAYAFANYIA KAZI
1.John Mnyika anafanya vizuri ndani ya JImbo lake kwa kiasi flani.lakini ili aweze kufanikiwa zaidi basi ni Muhimu akajitenga na siasa za kuattack watendaji wa serikali na kuwatolea amri iliwatimize shughuli za maendeleo ya jimboni mwake.
Kwa mfano>alipotoa masaa 48 maji yawe yanatoka jimboni kwake kwa watendaji wa DAWASCO hakuwa angalia kwamba yeye ni mwnasiasa na anowambia ni watendaji wa serikali.
Kwa maksudi wanaweza kumuangusha katika kufanikisha kile alicholenga kukifanya.
Pia mnyika anapaswa kuangalia namna anavyowaweka viongozi wake wa juu katika upeona upokeo wa kimatendo na kiushirikiano.Yeye ni mwanasiasa kijana sana na muda mrefu kwenye ulingo huu,basi kwa nafasi yake inatakiwa aangalie namna navyowatreat kinidhamu na kiutendaji kazi hawa viongozi wajuu wa chama.Hizi kelele tunazosikia nyuma ya pazia kwamba anatumika,au anamkubali sana mtu flani si jambo jema kwa ustawi wa chama.
2.John Heche akiwa kama wenyekiti wa BAVICHA bila kusuasua napenda kusema kunambo mengi ndani ya Baraza lake yamekwenda kombo.
John heche anatakiwa achukue hatua kuhakikisha yeye na makamu wake wanakuwa kitu kimoja.Hivi sasa nakili wazi viongozi hawa wawili wanaongea na kucheka kama binadamu lakini mioyoni mwao wanatofauti/mpasuko kubwa sana ya kiutendaji.
Heche anakambi yake(sitaki kuitaja) naye makamu mwenyekiti anawatu wake.Hii kwa uhai wa Baraza ni hatari sana,lazima Heche ajitambue kwamba yeye ni kiongozi mkubwa basi hana cha kusubiri zaidi ya kuhakikisha mambo yana kaa sawa.
Pia Heche tangu aingie madarakani kunajambo amabalo sijajua ama maksudi au kwa bahati mbaya ameamua kulitupa,kuliacha,kulitelekeza na kuto litupia macho kabisa ili hali ndio muhimili wa Vijana wasomi ndani ya chadema,Ndio shamba la kuvuna vijana wasomi wa chadema,Ndio chuo cha kuzalisha viongozi wa somi ndani ya chadema...Swala hilo ni CHASO.
CHASO-CHADEMA STUDENT ORGANIZATION imetelekezwa,haipo pamoja,inajikongoja.Karibia vyo vyote vya juu vya elimu ya kati vina vijana wa chadema ambao wamejikusanya kwa jitihada zao,wanajiongoza wanakiu ya ukombozi kupita maelezo.
Lakini baraza la vijana la chadema chini ya John Heche limeshindwa kuwaunganisha vijana hawa.hakuna uongozi wa CHASO kitaifa,Hakuna anayetambua viongozi wa chaso wanaomaliza muda wake wanakenda wapi?Heche hajui yawezekana hata idadi ya matawi ya chaso ndani ya chadema.
JOhn heche hatembelei kufungua matawi ya chaso,Heche hatembelei kuangalia Vijana hawa wa chasso kwenye matawi yao wanakabiliwa na matatizo gani.
John heche jitizame kama umekamilika kuhusu hili,CCM wanalia kuna vijana wanaharakati na wanamapinduzi wasomi wote wanakimbilia CHASO.Vijana wa chaso wanatikisa chaguzi mbalimbali za Urais vyuoni mwao.Lakini je wanaandaliwa mazingira gani ya kukua kisiasa ndani ya baraza la Vijana?
Lakini mwisho,John heche naomba tumie akili yako na ya wenzako,Kuna haja gani ya kendekeza makundi ndani ya barza la vijana?kwanini kwenye mikutano yako hutoi nafasi kwa vijana flaniflani ambao wanaonekana hawapo upande unaouamini ndani ya chama?Weweni kiongozi hutakiwi kuegamia upande wowote..Lakini kesi za kugoma kutoa maiki za kuhutubia mikutanoni kwa vijana flani zimekuwa nyingi sana.
Je kuwanyima maiki ndio suruhisho la mogogoro wako na wao?Je BAVICHA inaundwa na vijana wa upande mmoja?
asanteni.
Ni hayo tu
Mkuu tuntemeke hivi ndivyo twajenga chama kwa hoja za kutambua udhaifu na how to fix.nakupa pongezi kwa mawazo yako ya kujenga chama na kiukombozi.