Undani wa John Mnyika na John Heche

Undani wa John Mnyika na John Heche

Hapo ndipo napoanza kuamini wote ni wababaishaji tu si chama kilichoko madarakani wala vyama vya upinzani, Kama hakuna chama cha upinzani kitakachothubutu kuonyesha njia kwa vitendo,vitakuwa na umaarufu lakini haviwezi kuaminika kwa wanyonge hata siku moja, siwezi kushawishika kwamba CDM hawana uwezo wa kuonyesha utendaji kwa kuchagua mambo muhimu yanayowagusa wanyonge waliowengi na kuwasaidia, eti mpaka wasubiri waingie Ikulu wakusanye Kodi, haya ni mawazo ya Utopia!! UNAPOKUTANA NA MTU ANALIA KWA USTAARABU TU WA KAWAIDA KABISA UNATOA KITAMBAA CHAKO CHA MFUKONI UNAMPATIA AFUTE MACHOZI.." sio unamsaidia kulia.

Kwa kiwango chochote wanachopata CDM ikiwa ni ruzuku, misaada kutoka kwa chama rafiki,michango ya wanachama,harambee, michango ya wabunge na "fundrising" yote hiyo wanapaswa waanze taratibu kuchagua mambo muhimu wasaidie wananchi, wanajiandaaje kuongoza nchi hawajui kuwahudumia wananchi? Napata taabu sana kutahmini ikiwa kuna watu makini Tanzania wenye nia ya dhati na utashi wa kuwatumikia watanzania ikiwa kuna watu bado wana fikra kama zako!!

Kitendo cha kuwa shupavu na mahiri katika kulalamika na kueleza udhaifu wa chama, serikali ama mtu mwingine sio dalili ya kuwa na nia safi ama utashi wa kuwatumikia watanzania, tutahitaji tujiridhishe kwa historia yako katika kuwasaidia watanzania,na watanzania wa leo wamechoka kusikia Blah....blah....blah! ikiwa watanzania wamekata tamaa basi wewe uanayejinasibu kuwa mkombozi wao utembee katika maneno yako!! ''SIO KUHUBIRI MAJI KISHA WEWE UNAKUNYWA MAZIWA'' ni unafiki mkubwa na kamwe huwezi kuaminika hata kidogo.

Lengo la chama cha upinzani ni kukosoa na kutoa mawazo mbadala na kuonyesha wao wakichukua dola watafanya nini kizuri zaidi

Si malengo ya chama cha upinzani kubeba majukumu ya serikali inayokusanya kodi.Lengo la upinzani kuonyesha sera na mipango sahihi zaidi itakayoleta tija kwa wananchi wake

Harakati za CHADEMA hazina tofauti na harakati za TANU kumuondoa mkoloni aliyeko madarakani.Ni harakati za kumuondoa mtawala aliyebweteka na kutumia jasho la wananchi kwa maslahi ya wachache

CHADEMA kama ilivyokua TANU kina jukumu la kuwaamsha wanyonge na kuunganisha nguvu dhidi ya mfumo mbovu unaosimamiwa na watawala wasiojali raia wake kama ilivyokua kwa TANU ambayo ilikua haikusanyi kodi lakini iliunganisha nguvu kuongoza mabadiliko

TANU haikua na viongozi wenye uzoefu serikalini lakini walichukua uhuru na kuunda serikali kwa kutumia watumishi waadilifu waliokuwa wakiitumikia serikali ya kikoloni hivyo walisimamia sera na mipango chini ya serikali ya Nyerere.

Pia hoja ya uzoefu inazidi kuchuja.Chama cha The Dream huko Georgia kilianzishwa mwezi May lakini mwezi Oktoba kimechukua madaraka.Wananchi wamekiamini kutokana na elimu ya uraia

Pia hoja ya CHADEMA kupata ufadhili kutoka kwa Marafiki,kwani hujaona mradi wa maji wa Sabodo ambao CHADEMA iliombwa ipeleke mchanganuo?

Pia CHADEMA tunakoongoza halmashauri tunawaonyesha wananchi kile ambacho tutafanya tukiwa madarakani kutokana na mipango mizuri zaidi

Kazi ya CHADEMA bungeni inaeleweka na sijui kwanini unataka CHADEMA labda ijenge barabara ilihali unajua haikusanyi kodi
 
Ben hata mimi nampongeza sana mkuu kwa kushinda hiyo vita ya kuunganishwa na kina Habibu Mchange na Mwampamba, Huyu jamaa amedhihirisha usomi wake kwamba ni wa maana na Huyu jamaa ni lulu kwa taifa siyo tu kwa chama wakuu

Mkuu Lomayann

Na hapo ndipo unapoweza kugundua kama mtu aliyeenda shule elimu yake imemsaidia au La.Ndiyo maana siku zote nasema vijana wasomi wajiepushe na mambo ya hovyo ya kutukana na kukashifu watu kama wendawazimu.

Ben Saanane ameweza kufaulu mtihani huo.Ben angeingia nae mkumbo wa kuwatukana viongozi wakuu wa chama chake kupitia JF,Tanuru ama FB heshima anayomwagiwa kwenye mjadala huu isingekuwepo.

Ukisoma maandiko matakatifu ya Kiislam na Kikristo yote yanazungumzia heshima kwa wazazi,wazee na watu waliokuzidi umri.Sasa leo anapoibuka kijana mdogo kabisa na kuanza kuwatukana kila aina ya matusi na kashfa wazee ndani ya chama kisa tu wametofautiana kimtizamo ni aibu kubwa kwa hao vijana na Taifa kwa ujumla.Na dhambi ya namna hiyo haiwezi kupita hivihivi.
 
WanaJF,
Mara ya mwisho kuzungumzia undani wa wanasiasa ilikuwa mwezi January mwaka huu kwa kuwazungumzia wanasiasa mashuhuri Tanzania Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.Niliahidi nitarudi tena na mada hii hii kuwajadili wanasiasa wengine.Na nitakuwa nikifanya hivyo mara kwa mara nipatapo nafasi bila kubagua wanasiasa kwa itikadi zao.

Leo nitaomba kuwajadili wanasiasa wengine mashuhuri katika anga la Tanzania.Wanasiasa hao ni John Mnyika-Mbunge wa Jimbo la Ubungo na John Heche-Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa.Nimewachanganya Pamoja kwa sababu wanashabihiana kwa mambo mengi lakini lamsingi likiwa Itikadi yao na misimamo yao kuhusu mambo ya msingi.

Mafanikio Misimamo yao:

-Kwanza wote hawa ni vijana na wamekuwa kama Role model kwa vijana wengi si kwa vijana wa CDM tu bali kwa vijana wa Itikadi zote.
-Ni vijana wenye misimamo isiyoyumba na wanakitetea kwa nguvu kile wanachokiamini bila kuogopa vitisho kutoka kwa yeyote.
-Kutokana na Karama za kiuongozi walizo nazo wamefanikiwa kufika nafasi za juu kabisa za uongozi kwa umri wao.John Mnyika mbali ya kuwa mbunge anayeongoza jimbo kubwa kabisa la Ubungo pia yeye ndiye msemaji mkuu wa chama chake cha CDM.John Heche ni kiongozi wa BAVICHA Taifa na mjumbe wa Kamati kuu ya chama chake CDM,chombo cha ngazi ya juu kabisa ndani ya chama chake.
-Vijana hawa wamekuwa wakifanya kazi kubwa ndani ya chama chao hasa kuimarisha chama vijijini na kukipigania chama.Mafanikio yoyote ndani ya CDM huwezi kuwakosa hawa vijana.
-Ni vijana ambao hawaamini katika siasa za makundi.Sikuzote wanaamini katika CDM Imara.Huwezi kuwakuta wakishabikia majina ya watu ndani ya chama chao bali wanashabikia sera na Itikadi ya CDM.
-Ni wanyenyekevu,watiifu na wanapenda kukosolewa.
-Vijana hawa wana heshima kubwa kwa viongozi wao ndani ya Chama na huheshimu siku zote busara za wazee.Lau wakikosoa basi hukosoa kwa staha kubwa.

Changamoto zao:

-John Heche na John Mnyika pamoja na sifa zote zilizotajwa juu bado wanachangamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwafikia vijana wengi zaidi hasa wa vijijini na kuwapa somo la Uraia hususan umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura kwani inaonekana vijana wengi ni wafuasi sugu wa CDM lakini hawajiandikishi wala kupiga kura.
-Kutokana na umaarufu wao wamejitokeza vijana wengine wenye chuki na mafanikio yao na kuwaandama kwa matusi na maneno ya uongo hasa kupitia mitandao ya kijamii.Hata hivyo bado vijana hawa wameonyesha subira kubwa kwa mashambulizi hayo.Hawajakata tamaa bali wanasonga mbele.

Kwa Viongozi wakuu wa CHADEMA.

-Kutokana na yote niliyoandika juu viongozi wakuu wa CDM wanapaswa kuwatia moyo vijana hawa ili wasonge mbele zaidi na wasikatishwe tamaa na maadui wa CDM.
-CDM kama chama wanapaswa kuandaa vijana wasomi wanaofuata nyayo za kina Mnyika na Heche.Hata hivyo nafarijika kuona wapo vijana ndani ya CDM wenye uwezo wa kufuata nyayo hizi.Kwa mfano yupo kijana anayeitwa Ben Saanane,kwa wanaofuatilia siasa zake watagundua kwamba ni kijana anayeonyesha uvumilivu wa hali ya juu.Ben Saanane amewahi kupata misukosuko ya kisiasa lakini alisimama imara kutetea anchoamini.Hakuwahi kukashifu viongozi wake wa chama katika uficho au kwa uwazi.Ben anaamini CDM kama taasisi imara na siyo makundi ya watu.Ninaweza kusema Ben Saanane ni matunda ya kazi nzuri za kina Mnyika na wenzake.Hata hivyo chama kiandae vijana wengi zaidi wa kufuata nyayo za kina Mnyika na Heche na siyo Ben Saanane tu...

WanaJF Karibuni kwa mjadala!

Wanabodi

Nimekuwa nikifuatilia sana jukwaa hili kama Guest lakini sasa nimeona nijisajili rasmi baada ya kuona Fmpiganaji ameleta mada iliyonifurahisha.

Kwa kweli hawa vijana John Mnyika na John Heche wananifurahisha sana kwa utendaji wao.Ni watu waliosababisha nianze kupenda na kufuatilia wanasiasa.
Kama huyu Ben Saanane anafuata nyayo zao basi itakuwa vema sana.
 
Hii ni thread ambayo imeshawishi mgeni kujisajili.ustaarabu na staha kwa kuleta hata mahasimu.Nyota ya Ben kisiasa inaonekana ni nzuri.Hii ni thread ya mwaka
 
Lengo la chama cha upinzani ni kukosoa na kutoa mawazo mbadala na kuonyesha wao wakichukua dola watafanya nini kizuri zaidi

Si malengo ya chama cha upinzani kubeba majukumu ya serikali inayokusanya kodi.Lengo la upinzani kuonyesha sera na mipango sahihi zaidi itakayoleta tija kwa wananchi wake

Harakati za CHADEMA hazina tofauti na harakati za TANU kumuondoa mkoloni aliyeko madarakani.Ni harakati za kumuondoa mtawala aliyebweteka na kutumia jasho la wananchi kwa maslahi ya wachache

CHADEMA kama ilivyokua TANU kina jukumu la kuwaamsha wanyonge na kuunganisha nguvu dhidi ya mfumo mbovu unaosimamiwa na watawala wasiojali raia wake kama ilivyokua kwa TANU ambayo ilikua haikusanyi kodi lakini iliunganisha nguvu kuongoza mabadiliko

TANU haikua na viongozi wenye uzoefu serikalini lakini walichukua uhuru na kuunda serikali kwa kutumia watumishi waadilifu waliokuwa wakiitumikia serikali ya kikoloni hivyo walisimamia sera na mipango chini ya serikali ya Nyerere.

Pia hoja ya uzoefu inazidi kuchuja.Chama cha The Dream huko Georgia kilianzishwa mwezi May lakini mwezi Oktoba kimechukua madaraka.Wananchi wamekiamini kutokana na elimu ya uraia

Pia hoja ya CHADEMA kupata ufadhili kutoka kwa Marafiki,kwani hujaona mradi wa maji wa Sabodo ambao CHADEMA iliombwa ipeleke mchanganuo?

Pia CHADEMA tunakoongoza halmashauri tunawaonyesha wananchi kile ambacho tutafanya tukiwa madarakani kutokana na mipango mizuri zaidi

Kazi ya CHADEMA bungeni inaeleweka na sijui kwanini unataka CHADEMA labda ijenge barabara ilihali unajua haikusanyi kodi

Good.umemaliza kaka.Kweli Jembe
 
Mnyika

Ni kijana mwenye akili nyingi sana na kama kweli wako na Ben saanane sambamba basi ni hatua nzuri kwa kuwa Ben na Mnyika ni wanasiasa vijana wenye uwezo wa kujenga hoja na wakaeleweka ingawa kidogo Ben naona anafanya siasa za hatari hasa kuunda alliance na watu ambao wana historia mbaya kwenye chama.Huwa anajiamini kupita kiasi

Halikadhalika John Mnyika atamkomaza zaidi Ben huko tuendako na kama watafanya kazi karibu wataongeza ngivu katika safu ya vijana

Mnyika ameweza kuongeza haiba ya vijana

JOHN HECHE

Ni kiongozi mzuri.Nilihofia kama aliweza kuvumilia mikimiki ya vurugu za alliance ya akina Ben Saanane na lile kundi na hasa mkakati wa kumpiga vita na kumpindua
Ameweza kwenda vijijini
Naona ni jambo la kumshukuru Mungu kama hawa wameweza kukaa pamoja
Sasa naona hata vita ya Heche na makamu wake shonza itakosa nguvu.Ukimwondoa ben hapo akina mchange hawatakua na nguvu

Ben Saanane
Kosa lake kubwa ni kutulia.Bado anastahili kwenda sana vijijini.Hata ukiongea nae ana kwa ana utavutiwa nae
Pia haya maswala yake na wasichana wanatakiwa waache mara moja na hata Mnyika.Wanasiasa wakubwa na Bright wamejumiwa mara nyingi na kupenda kwao watoto.Vinginevyo hizi colabo hapa zimetulia mno.Nitafurahi siku moja nikiwaona heche,ben na Mnyika jukwaani au wakienda vijijini pamoja
wajanja wawili hawachimbi shimo. Angalia Julius Nyerere na Kambona, Nyerere na Mtei. Kila mmoja hapo(Mnyika, Heche na Ben) wasifanye kazi pamoja abadani watagombana tu.
 
Lengo la chama cha upinzani ni kukosoa na kutoa mawazo mbadala na kuonyesha wao wakichukua dola watafanya nini kizuri zaidi

Si malengo ya chama cha upinzani kubeba majukumu ya serikali inayokusanya kodi.Lengo la upinzani kuonyesha sera na mipango sahihi zaidi itakayoleta tija kwa wananchi wake

Harakati za CHADEMA hazina tofauti na harakati za TANU kumuondoa mkoloni aliyeko madarakani.Ni harakati za kumuondoa mtawala aliyebweteka na kutumia jasho la wananchi kwa maslahi ya wachache

CHADEMA kama ilivyokua TANU kina jukumu la kuwaamsha wanyonge na kuunganisha nguvu dhidi ya mfumo mbovu unaosimamiwa na watawala wasiojali raia wake kama ilivyokua kwa TANU ambayo ilikua haikusanyi kodi lakini iliunganisha nguvu kuongoza mabadiliko

TANU haikua na viongozi wenye uzoefu serikalini lakini walichukua uhuru na kuunda serikali kwa kutumia watumishi waadilifu waliokuwa wakiitumikia serikali ya kikoloni hivyo walisimamia sera na mipango chini ya serikali ya Nyerere.

Pia hoja ya uzoefu inazidi kuchuja.Chama cha The Dream huko Georgia kilianzishwa mwezi May lakini mwezi Oktoba kimechukua madaraka.Wananchi wamekiamini kutokana na elimu ya uraia

Pia hoja ya CHADEMA kupata ufadhili kutoka kwa Marafiki,kwani hujaona mradi wa maji wa Sabodo ambao CHADEMA iliombwa ipeleke mchanganuo?

Pia CHADEMA tunakoongoza halmashauri tunawaonyesha wananchi kile ambacho tutafanya tukiwa madarakani kutokana na mipango mizuri zaidi

Kazi ya CHADEMA bungeni inaeleweka na sijui kwanini unataka CHADEMA labda ijenge barabara ilihali unajua haikusanyi kodi

Bwana Ben ninachokisema kiko wazi kabisa wala hakihitaji elimu ya uraia kukielewa, kile kitendo cha wanachadema waliokwenda na greda kupanua mto msimbazi hakikuhitaji muingie madarakani mkusanye kodi kwanza ndipo mkakodi greda kufanya jambo zuri kwa wananchi kama lile, sasa kwa utaratibu ule ndo mimi nataka mfanye zaidi hata kwa mambo mengine msaidie wananchi, usinipe mfano wa TANU kumtoa mkoloni,mindset za watanzania wa leo haziko kwenye kumuondoa mkoloni na ndio maana unaona pamoja na kusema kila uchaguzi mnaibiwa kura lakini ukweli ni kwamba bado kuna kundi kubwa la watanzania halijawaamini CHADEMA na zaidi ni kundi lisilokuwa na chama chochote kama mimi hapa.

Unawezaje kutoa mfano wa halimashauri mnazoziongoza CDM wakati mnaziongoza kwa kutumia ilani ya CCM? Pengine labda pale mtakapotekeleza ilani hiyo kwa uaminifu pasiwepo na mislocation of funds kama ilivyokuwa imezoeleka.Sidhani kama CDM kusaidia wananchi ni kubeba majukumu ya serikali au basi ni lini mliongoza walau wananchi kuchangia fedha kwa ajili ya kufanya jambo fulani kwa manufaa ya wanyonge; ikiwa ni zahati ya kijiji, shule ama visima vya maji? sijawahi kusikia zaidi ya kuwasikia mkizing'ong'a shule na zahati za mahasimu wenu wa kisiasa CCM, Bw. Saanane CDM, wapo vijana wachapa kazi na wasomi lakini hiki kitu huwa nakishangaa sana kwanini huwa hamjawahi kufikiri hili, maana mpaka mnaonekana ni watu wa kusubiri scandals ili mzunguke Tanzania nzima kuzifafanua,je mnafikiri hivyo ndiyo kutafuta kuaminika kwa watanzania?

Hakuna asiyejua kuwa watanzania walio wengi ni wavivu, hawafanyi kazi na kama wanafanya kazi ni kwa saa chache sana zinazobaki ni Blah...blah...blah! na starehe kwa sana, ni lini na mkutano gani mliwaeleza wanachama wenu, wapiga kura wenu kuhusu wajibu huu muhimu kwa maendeleo ya nchi yao na hasa kuwa mahiri katika kutekeleza majukumu yao kwa ngazi mbalimbali za kijamii? au hamjui kwa mvivu akishindwa jambo hutafuta visingizio? au pengine nyie mkiingia madarakani mnadhani watakuja watanzania tofauti na hawa mliowazoeza kulalamika tu hata kwa mambo muhimu wanayopaswa kuyatekeleza wao kama wao katika familia zao?

Sifurahishwi na mambo mengi yanayofanywa na serikali ya CCM lakini vilevile bado sioni chama chenye utashi wa kweli wa kuwakomboa watanzania, vyama vyenu vimeingiwa na mdudu mbaya wa makundi kila kukicha, kila mtu kwenye chama anataka awe maarufu, kila mtu kwenye chama ni msemaji wa chama sasa unashindwa kuelewa kama hawa watu nia yao ni moja ama kila mmoja ana maslahi yake binafsi. Pamoja na kueneza elimu ya uraia ipo kazi kubwa ya kuwafanya watanzania wawaamini maana nyie wenyewe kwanza aidha hamwaminiki au hamwaminiani, mambo ni vululuvulu!!!!!
 
mkuu tuntemeke swala la CHASO ni muhimu kwa ajili ya kuvuna vijana wapigania mabadiliko ya kweli hapo nakuunga mkono
lakini huyu binti yetu SHONZA ameamua mwenyewe na wote tunamwona akijiandaa kusumbua baraza lao labda tumfanyie maombezi aepukane na siasa za shibuda
Asante mkuu kwa kutambua umuhimu wa CHASO kwa ustawi wa chadema imara ya yakisasa.
 
wajanja wawili hawachimbi shimo. Angalia Julius Nyerere na Kambona, Nyerere na Mtei. Kila mmoja hapo(Mnyika, Heche na Ben) wasifanye kazi pamoja abadani watagombana tu.

Labda JAMII FORUMS AU MEMBER YEYOTE aanzishe kura ya maoni safu ya Chadema mwakani itakayopambana na CCM

-Opinion Poll

-MWENYEKITI:

ZITTO KABWE
FREEMAN MBOWE

-JUMUIYA YA WANAWAKE

RACHEL MASHISHANGA
ESTHER WASIRA
HALIMA MDEE

-BAVICHA
Habibu Mchange
Sharifa Mohamed
Ben Saanane
Deo Munis

WAZEE
Mabere Marando
John Shibuda
Profesa Abdallah Safari

KATIBU MKUU
DR.SLAA
MNYIKA
MKUMBO
 
Wanabodi

Nimekuwa nikifuatilia sana jukwaa hili kama Guest lakini sasa nimeona nijisajili rasmi baada ya kuona Fmpiganaji ameleta mada iliyonifurahisha.

Kwa kweli hawa vijana John Mnyika na John Heche wananifurahisha sana kwa utendaji wao.Ni watu waliosababisha nianze kupenda na kufuatilia wanasiasa.
Kama huyu Ben Saanane anafuata nyayo zao basi itakuwa vema sana.

Mkuu Greenwhich.

Kwanza nakushukuru sana na Karibu sana jamvini.Ninajisikia Fahari kuona nimekuwa Source ya wewe kujisajili JF.

Ningependa wanasiasa vijana waone unapofanya siasa za kistaarabu na za heshima unakuwa katika mioyo ya watu.Kwamba huyu Greenwhich ameipenda siasa kwa sababu ya hawa vijana.Hiyo ni heshima kubwa na Mnyika,Heche,Ben na wenzao wanapaswa kuendeleza siasa hizi za kistaarabu ili kuwavutia watu wasiopenda siasa.

Lakini pia ninaamini huyu Greenwhich amevutiwa kujisajili kutokana na jinsi huu mjadala unavyojadiliwa kistaarabu.Huu ni mfano wa mjadala unavyopaswa kuwa hapa JF.Moderators na Wanajamvi hongereni sana kwa hilo.
 
Asante mkuu kwa kutambua umuhimu wa CHASO kwa ustawi wa chadema imara ya yakisasa.
Tuntemeke wataleta udini kama kawa.Demokrasia huko hamna.hebu weka opinion poll hapo juu nashindwa kuanza uzi.jf administrators watamodify
 
Hii ni thread ambayo imeshawishi mgeni kujisajili.ustaarabu na staha kwa kuleta hata mahasimu.Nyota ya Ben kisiasa inaonekana ni nzuri.Hii ni thread ya mwaka

Comrade Jibril

Kwa mara nyingine nasema tena Asante sana.

Dhahabu ni Dhahabu tu hata ikifichwa kwenye matakataka au kwenye udongo,haimati itachukua muda gani lakini lzima itafichuliwa tu.

Hii ndiyo JF tuitakayo.!
 
wajanja wawili hawachimbi shimo. Angalia Julius Nyerere na Kambona, Nyerere na Mtei. Kila mmoja hapo(Mnyika, Heche na Ben) wasifanye kazi pamoja abadani watagombana tu.

hao wote watataka kufunikana.na wote ni waroho wa madaraka kama maalim seif au odinga
 
Labda JAMII FORUMS AU MEMBER YEYOTE aanzishe kura ya maoni safu ya Chadema mwakani itakayopambana na CCM

-Opinion Poll

-MWENYEKITI:

ZITTO KABWE
FREEMAN MBOWE

-JUMUIYA YA WANAWAKE

RACHEL MASHISHANGA
ESTHER WASIRA
HALIMA MDEE

-BAVICHA
Habibu Mchange
Sharifa Mohamed
Ben Saanane
Deo Munis

WAZEE
Mabere Marando
John Shibuda
Profesa Abdallah Safari

KATIBU MKUU
DR.SLAA
MNYIKA
MKUMBO

Ndugu yangu naona kwa makusudi umeamua kuja kuharibu huu mjadala.Kwanini usianzishe mada yako kuliko kuja kuvuruga mada ya mwenzako?
 
Tuntemeke wataleta udini kama kawa.Demokrasia huko hamna.hebu weka opinion poll hapo juu nashindwa kuanza uzi.jf administrators watamodify

Mkuu wangu mbona mleta mada hajaongelea mambo ya udini? Kwanini umeamua kuja kuvuruga mjadala wa kistaarabu?
 
Mkuu kiribo

Niseme kidogo kuhusu huyu Binti Shonza,huyu binti ni mzuri sana kiuongozi kwani namfahamu vyema tangu akiwa mwaka wa kwanza chuoni.
Tatizo lake moja tu ni kudanganywa na akadanganyika.

Unajua nilisoma siku moja makala ya Dr Kitila niliipenda sana.Dr Kitila alisema hawa vijana wanapochaguliwa nafasi za uongozi wanapaswa kupata semina za maadili ya uongozi.Wanapaswa kujua miiko ya Uongozi.

Sasa kitendo cha Shonza kwenda kwenye vyombo vya habari kumpinga Mkiti wake ilikuwa ni mbaya sana kwake.Na hii itamgharimu Shonza kisiasa maisha yake yote.

Kwa ninavyomjua Shonza naamini kuna vijana walimuingiza kwenye mtego naye akaingia mkenge.Ni vigumu sana viongozi wenzake kumuamini kwa sasa.Kwani kulikuwa na hasara gani Shonza kusubiri vikao ndipo amshambulie Mkiti wake?

Ujana bwana maji ya moto usipokuwa makini utaungua.Hata hivyo naamini Shonza amejifunza kitu.
alianza mienendo ya kuzunguka na wale jamaa wenye ID nyingi humu JF wakampa sumu balaa binti yetu mimi ni mmoja wa watu niliyefanikiwa kuhudhuria graduation yake pale mabibo nilimsikia bwana HECHE ambaye ni mwkt wake akiteta na kuwaondoa hofu ndugu zake shonza kuwa ana mpango wa kumgroom kisiasa huyu binti ili naye awe ni alama ya nini lilikuwa lengo la bavicha lakini badae nilisikitika kumsikia mimi kwa sikio langu mdogo wetu huyu akijitapa kuwa ntamfuta heche kwenye siasa na ntamwaibisha nilichemka mwili wote jamani vijana wetu jaribuni kuwa na subira na muelewe screening ya mambo ni kitu cha ziada
 
Bwana Ben ninachokisema kiko wazi kabisa wala hakihitaji elimu ya uraia kukielewa, kile kitendo cha wanachadema waliokwenda na greda kupanua mto msimbazi hakikuhitaji muingie madarakani mkusanye kodi kwanza ndipo mkakodi greda kufanya jambo zuri kwa wananchi kama lile, sasa kwa utaratibu ule ndo mimi nataka mfanye zaidi hata kwa mambo mengine msaidie wananchi, usinipe mfano wa TANU kumtoa mkoloni,mindset za watanzania wa leo haziko kwenye kumuondoa mkoloni na ndio maana unaona pamoja na kusema kila uchaguzi mnaibiwa kura lakini ukweli ni kwamba bado kuna kundi kubwa la watanzania halijawaamini CHADEMA na zaidi ni kundi lisilokuwa na chama chochote kama mimi hapa.

Unawezaje kutoa mfano wa halimashauri mnazoziongoza CDM wakati mnaziongoza kwa kutumia ilani ya CCM? Pengine labda pale mtakapotekeleza ilani hiyo kwa uaminifu pasiwepo na mislocation of funds kama ilivyokuwa imezoeleka.Sidhani kama CDM kusaidia wananchi ni kubeba majukumu ya serikali au basi ni lini mliongoza walau wananchi kuchangia fedha kwa ajili ya kufanya jambo fulani kwa manufaa ya wanyonge; ikiwa ni zahati ya kijiji, shule ama visima vya maji? sijawahi kusikia zaidi ya kuwasikia mkizing'ong'a shule na zahati za mahasimu wenu wa kisiasa CCM, Bw. Saanane CDM, wapo vijana wachapa kazi na wasomi lakini hiki kitu huwa nakishangaa sana kwanini huwa hamjawahi kufikiri hili, maana mpaka mnaonekana ni watu wa kusubiri scandals ili mzunguke Tanzania nzima kuzifafanua,je mnafikiri hivyo ndiyo kutafuta kuaminika kwa watanzania?

Hakuna asiyejua kuwa watanzania walio wengi ni wavivu, hawafanyi kazi na kama wanafanya kazi ni kwa saa chache sana zinazobaki ni Blah...blah...blah! na starehe kwa sana, ni lini na mkutano gani mliwaeleza wanachama wenu, wapiga kura wenu kuhusu wajibu huu muhimu kwa maendeleo ya nchi yao na hasa kuwa mahiri katika kutekeleza majukumu yao kwa ngazi mbalimbali za kijamii? au hamjui kwa mvivu akishindwa jambo hutafuta visingizio? au pengine nyie mkiingia madarakani mnadhani watakuja watanzania tofauti na hawa mliowazoeza kulalamika tu hata kwa mambo muhimu wanayopaswa kuyatekeleza wao kama wao katika familia zao?

Sifurahishwi na mambo mengi yanayofanywa na serikali ya CCM lakini vilevile bado sioni chama chenye utashi wa kweli wa kuwakomboa watanzania, vyama vyenu vimeingiwa na mdudu mbaya wa makundi kila kukicha, kila mtu kwenye chama anataka awe maarufu, kila mtu kwenye chama ni msemaji wa chama sasa unashindwa kuelewa kama hawa watu nia yao ni moja ama kila mmoja ana maslahi yake binafsi. Pamoja na kueneza elimu ya uraia ipo kazi kubwa ya kuwafanya watanzania wawaamini maana nyie wenyewe kwanza aidha hamwaminiki au hamwaminiani, mambo ni vululuvulu!!!!!

Nashukuru Mkuu, lakini Watz lazima wafumbe macho wapite kimya kimya kwenye post yako, wakidhani wanamkomoa mtu, kumbe wanajikomoa wenyewe!
Nguvu ya UMMA ipo? Why isitumike? Mfano tu, kila tawi la liwaunganishe vijana, tena bila kujali itikadi zao za vyama, wawe na mradi wowote wa maendeleo, hata kufuga kuku, kulima, ama kufyatua tofali, wenyeviti wa Bavicha wawe wanawatembelea na kuwahimiza, miaka miwili kila mwanakikundi ana baiskeli yake, unadhani wangapi wangejenga imani na chama?
UONGOZI ni UBUNIFU! Hata michango ya HARAKATI, ingetoka huko! Mnang'ang'ana tu changieni chama, m4c, n.k hamjui wanazitoa wapi? Wengine wanakaba wapate hela ya kuchangia, inakuwa yaleyale unatoa moja unaweka moja!
Uongozi ni Ubunifu!
Mungu wetu anaita sasa!
 
JangalaFalsafa unachokisema ndo kitu nachokihitaji, uko sahihi kabisa, CDM au kambi ya upinzani kwa ujumla wanapaswa kujitathmini kila wakati na kujielekeza katika mambo ya msingi yatakayowaletea heshima kubwa na watanzania walio wengi kuwaamini,wasiwe na papara za kuwalazimisha watanzania kuwaamini, kitendo cha kuaminika hakilazimishwi kitakuja automatically ikiwa wananchi wataridhika na utashi wa kweli katika kuwaletea mabadiliko.

BAVICHA wanaweza wakawa mstari wa mbele katika kuwaunganisha vijana wa Tanzania na kuwaongoza katika harakati za kujiletea kipato, Nguvu ya umma isitumike katika maandamano tu watumie nguvu ya umma katika shughuli za harambee ili kuwajengea uwezo vijana na mwisho wa siku hawa ndo watakichangia chama katika harakati zenu za M4C,au anzisheni utaratibu popote pale katika nchi hii itengwe hata siku moja kila mwisho wa mwezi vijana nchi nzima wafanye shughuli za kijamii, utaratibu huu upo Rwanda, upo Burundi mtakuwa walau positive katika Taifa hili vinginevyo kuna baadhi ya watanzania wataendelea kuwaona ni watu wa fujo fujo hivi, hamna ustaarabu hamna jema katika nchi hii licha ya michango mizuri bungeni kwa bahati mbaya si watu wote wanaweza kufanya tathmini kwa kupitia bunge.
 
Nashukuru Mkuu, lakini Watz lazima wafumbe macho wapite kimya kimya kwenye post yako, wakidhani wanamkomoa mtu, kumbe wanajikomoa wenyewe! Nguvu ya UMMA ipo? Why isitumike? Mfano tu, kila tawi la liwaunganishe vijana, tena bila kujali itikadi zao za vyama, wawe na mradi wowote wa maendeleo, hata kufuga kuku, kulima, ama kufyatua tofali, wenyeviti wa Bavicha wawe wanawatembelea na kuwahimiza, miaka miwili kila mwanakikundi ana baiskeli yake, unadhani wangapi wangejenga imani na chama? UONGOZI ni UBUNIFU! Hata michango ya HARAKATI, ingetoka huko! Mnang'ang'ana tu changieni chama, m4c, n.k hamjui wanazitoa wapi? Wengine wanakaba wapate hela ya kuchangia, inakuwa yaleyale unatoa moja unaweka moja! Uongozi ni Ubunifu! Mungu wetu anaita sasa!
JangalaFalsafa unachokisema ndo kitu nachokihitaji, uko sahihi kabisa, CDM au kambi ya upinzani kwa ujumla wanapaswa kujitathmini kila wakati na kujielekeza katika mambo ya msingi yatakayowaletea heshima kubwa na watanzania walio wengi kuwaamini,wasiwe na papara za kuwalazimisha watanzania kuwaamini, kitendo cha kuaminika hakilazimishwi kitakuja automatically ikiwa wananchi wataridhika na utashi wa kweli katika kuwaletea mabadiliko. BAVICHA wanaweza wakawa mstari wa mbele katika kuwaunganisha vijana wa Tanzania na kuwaongoza katika harakati za kujiletea kipato, Nguvu ya umma isitumike katika maandamano tu watumie nguvu ya umma katika shughuli za harambee ili kuwajengea uwezo vijana na mwisho wa siku hawa ndo watakichangia chama katika harakati zenu za M4C,au anzisheni utaratibu popote pale katika nchi hii itengwe hata siku moja kila mwisho wa mwezi vijana nchi nzima wafanye shughuli za kijamii, utaratibu huu upo Rwanda, upo Burundi mtakuwa walau positive katika Taifa hili vinginevyo kuna baadhi ya watanzania wataendelea kuwaona ni watu wa fujo fujo hivi, hamna ustaarabu hamna jema katika nchi hii licha ya michango mizuri bungeni kwa bahati mbaya si watu wote wanaweza kufanya tathmini kwa kupitia bunge.
 
Back
Top Bottom