Sina uhakika sana ikiwa utafiti wako hapo juu una ithibati, lakini naona nina hoja ya kuchangia,nitachepuka kidogo isipokuwa binafsi nitawachambua hao vijana kwa kujadili taasisi waliyopo (CHADEMA)
CDM kama chama kikuu cha upinzani hapa Tanzania kwa vyovyote vile lazima kikutane na changamoto lukuki katika harakati zake za kuingia ikulu, mara kadhaa nimekuwa nikimsikia Dr. Slaa akiwajibu mahasimu wake wa kisiasa (CCM) pale wanapolalama kwamba CMD muda wote wapo kuangalia mapungufu tu na kuyasema bila kutaja hata mazuri ya CCM, lakini yeye bila kumung'unya maneno alitoka na kusema wao CHADEMA hawapo kwa ajili ya kusifia mazuri ya CCM, maana kama ni mazuri hawaoni haja ya kuyataja.
Sasa kwa msingi huu, binafsi naona udhaifu mkubwa sana wa CDM kama sio wa Dr. Slaa, nafikiri huo ndo msimamo wa chama, hivyo BAVICHA ya kina Heche na wenzake wameendelea kulalamika kila kukicha kiasi kwamba kama utakuwa unafuatilia vizuri mikutano yao muda wote wanaeleza Rais kafanya nini....waziri kafanya nini..... wakati mwingine unaweza hata kubashiri mambo ambayo atakayoongea mara tu akianza.
My take: Siasa hizi zimepitwa na wakati, watanzania wamechoka kusikiliza watu wakilalamika tuuuuu! inapaswa sasa kwa uwezo mdogo walionao CDM waonyeshe kwa mfano; kama wanasema shule za kata hazina viwango, zitawaangukia wanafunzi hebu wajenge hata shule moja na wajinadi kwa kusema "Ikiwa tutaingia madarakani hizi ndo shule zenye viwango tutajenga" waseme na kutenda hivyo hivyo hata kwenye mambo kama visima vya maji, barabara za vijijini,zahati, ofisi za mitaa n.k
Kiukweli wananchi wamechoka kukusanyika kwenye mikutano wanapewa faraja ama machungu wanaporudi nyumbani kero ziko pale pale kwanza mkutano umewakawiza kwenda kutafuta kuni, kuchota maji maana ni ya shida, kwenda kutafuta vipimo zahati ya mbali,Inawezekana wanachoelezwa ni cha kweli lakini mwisho wa siku hawana jinsi zaidi ya kusubiri kipindi kingine cha uchaguzi waweze kufanya mabadiliko lakini pengine imebaki miaka 3 ndo uchaguzi mwingine sasa ndo kusema CDM wao watakuwa wakizunguka kulalamika tuuu! mi nadhani sio sahihi hebu watoke wafanye kwa mfano ndo njia peke itayowajengea imani na heshima kubwa kwa wapiga kula.
CHADEMA naweza kusema wamepanda mbegu mbaya sana kwa vijana wa kitanzania na watanzania kwa ujumla, Tabia ya kulalamika tuuuu na wengine sasa hata ukimuuliza kile acholalamika kwa kiasi gani ameona au anatambua athari zake, hajui chachote isipokuwa aliwahi kuwasikia viongozi wake wakilalamika, hii mbegu sio nzuri hata kidogo kuna wengine kabisa tunafahamu ugumu wa maisha yake sababu ni yeye mwenyewe lakini naye analalamika vijana au watu wa namna hii wapo kila kona ya nchi hii lakini ni lini hivi vyama vya upinzani vilisimama vikakemea vijana waache tabia ya kufanyiwa kila kitu? waache kukaa masikani na kusubiri maendeleo?
Kina Heche na Mnyika wamekuwa katika mkururo huo huo wa kulalamika tu kuonyesha madhaifu tu ya CCM na kusahau kuwaonyesha kwa mfano watanzania ni kipi wamefanya,najua watakuja watu wahoji juu ya fedha, lakini mi nasema wanaweza wakiamua, ujue CDM mpaka kimejipambanua kuwa ni chama kinachojengwa na matukio ni kweli kabisa!
Nilifarijika walau kwa mara ya kwanza kuona uongozi wa CDM( sikumbuki walikuwa ni wa wapi lakini sio makao makuu) walitoka na Greda kwenda kupanua nadhani mto msimbazi ili kusaidia wananchi waishio bonde la mto msimbazi wasipatwe maafa ya mafuriko, kitu kile ndo nataka iwe msimamo wa CDM Taifa na kila kiwango cha chama, mambo hayo ndo yatakayowajengea heshima kubwa na kuaminika zaidi kuliko kulalamika tu kila kukicha,mnawafundisha kitu kibaya sana watanzania kujipambanua nyie ni malaika siku ikitokea mkachukua nchi mbegu mlioipanda itawwatesa hata nyie wenyewe maana ndo mazoea! AKSANTENI.