Undani wa John Mnyika na John Heche

Undani wa John Mnyika na John Heche

Ritz kama utaendelea kujadili issues hapa JF ukiwa objective hivi litakuwa jambo la kheri sana. Kama ni kukubaliana tunakubaliana kwa hoja na kama tunapingana basi inakuwa ni kwa hoja.

Sasa ''ukianzaga'' yale mambo yako ya udini na ukabila ndo huwa unanichefua kabisa hata nisitake kukusoma.

Mkuu Mwita.
Ritz leo amenikuna sana kwa mchango wake, naamini hii yote ni kuelekea mabadiliko ya kuuona ukweli, naamini hata hayo mengine uliyoyasema atakuwa akiyajengea hoja kwa busara na hekima kubwa. Mkuu Ritz! Siku yangu ya leo umeifanya kuwa ya furaha na amani sana kwa aina ya michango iliyo jaa yale mafundisho ya kipenzi chetu (Muhammad S. A. W), sisi wote ni ndugu, tunapishana style na milango ya kumuombea Mwenyezi Mungu tu.
 
Last edited by a moderator:
Mkimaliza kujadili hii,mje mtuambie kwanini katika uchaguzi uliopita wa madiwani mmeambulia kata 5 tu!,ingawa mmefanya kampeni kubwa sana kila sehemu husika,kwa kutumia fedha za mzee sabodo.

View attachment 70318mfano hapa tunamwona HECHE akiwa huko ludewa katani tena hakuna hata umeme anaonekana katika kikao cha ndani usiku akiwa na kombat yake sio bar wala hotel hii ulitaka CHADEMA ifanye kampeni zipi hivi hujui kuwa chama kinazidi kufanikiwa hichi?
 
Heche nae ni kijana kweli maajabu yapo Chadema.Halafu wote hao uliowataja ni wapeleka maji bafuni wa mwenyekiti
Mitusi tuu!! weye unatumia kinywa kunanhiii?
unatia kinyaa kishenzi yaani!! umesomea kata gani?
 
Hii ni moja ya thread chache ambazo watu wengi wamejikita kwenye uchambuzi basi BEN atakuwa na kitu special I do wish him well in political life
 
Karibu tena mkuu,
Nimependa namna ulivyojitolea kuwaelezea hawa Vijana wawili wa kisiasa ndnai ya CHADEMA.
Namimi nakuunga mkono mkuu kwamba wanatakiwa kutiwa moyo na kupewa nafasi zaidi ili wakieneze chama kwa mapana zaidi.
LAKINI MKUU,KATIKA UCHAMBUZI WAKO UMEAINISHA MAFANIKIO,CHANGA MOTO NA RAI YAKO KWA VIONGOZI WA CHADEMA.
Naomba niongeze hili katika uchambuzi wako,kwamba hawa vijana wawili wanaoonekana kushabihiana
WANAMAPUNGUFU HAYA HAPA,AMBAYO NI MUHIMU WAKAYAFANYIA KAZI

1.John Mnyika anafanya vizuri ndani ya JImbo lake kwa kiasi flani.lakini ili aweze kufanikiwa zaidi basi ni Muhimu akajitenga na siasa za kuattack watendaji wa serikali na kuwatolea amri iliwatimize shughuli za maendeleo ya jimboni mwake.
Kwa mfano>alipotoa masaa 48 maji yawe yanatoka jimboni kwake kwa watendaji wa DAWASCO hakuwa angalia kwamba yeye ni mwnasiasa na anowambia ni watendaji wa serikali.
Kwa maksudi wanaweza kumuangusha katika kufanikisha kile alicholenga kukifanya.
Pia mnyika anapaswa kuangalia namna anavyowaweka viongozi wake wa juu katika upeona upokeo wa kimatendo na kiushirikiano.Yeye ni mwanasiasa kijana sana na muda mrefu kwenye ulingo huu,basi kwa nafasi yake inatakiwa aangalie namna navyowatreat kinidhamu na kiutendaji kazi hawa viongozi wajuu wa chama.Hizi kelele tunazosikia nyuma ya pazia kwamba anatumika,au anamkubali sana mtu flani si jambo jema kwa ustawi wa chama.

2.John Heche akiwa kama wenyekiti wa BAVICHA bila kusuasua napenda kusema kunambo mengi ndani ya Baraza lake yamekwenda kombo.
John heche anatakiwa achukue hatua kuhakikisha yeye na makamu wake wanakuwa kitu kimoja.Hivi sasa nakili wazi viongozi hawa wawili wanaongea na kucheka kama binadamu lakini mioyoni mwao wanatofauti/mpasuko kubwa sana ya kiutendaji.
Heche anakambi yake(sitaki kuitaja) naye makamu mwenyekiti anawatu wake.Hii kwa uhai wa Baraza ni hatari sana,lazima Heche ajitambue kwamba yeye ni kiongozi mkubwa basi hana cha kusubiri zaidi ya kuhakikisha mambo yana kaa sawa.
Pia Heche tangu aingie madarakani kunajambo amabalo sijajua ama maksudi au kwa bahati mbaya ameamua kulitupa,kuliacha,kulitelekeza na kuto litupia macho kabisa ili hali ndio muhimili wa Vijana wasomi ndani ya chadema,Ndio shamba la kuvuna vijana wasomi wa chadema,Ndio chuo cha kuzalisha viongozi wa somi ndani ya chadema...Swala hilo ni CHASO.
CHASO-CHADEMA STUDENT ORGANIZATION imetelekezwa,haipo pamoja,inajikongoja.Karibia vyo vyote vya juu vya elimu ya kati vina vijana wa chadema ambao wamejikusanya kwa jitihada zao,wanajiongoza wanakiu ya ukombozi kupita maelezo.
Lakini baraza la vijana la chadema chini ya John Heche limeshindwa kuwaunganisha vijana hawa.hakuna uongozi wa CHASO kitaifa,Hakuna anayetambua viongozi wa chaso wanaomaliza muda wake wanakenda wapi?Heche hajui yawezekana hata idadi ya matawi ya chaso ndani ya chadema.
JOhn heche hatembelei kufungua matawi ya chaso,Heche hatembelei kuangalia Vijana hawa wa chasso kwenye matawi yao wanakabiliwa na matatizo gani.
John heche jitizame kama umekamilika kuhusu hili,CCM wanalia kuna vijana wanaharakati na wanamapinduzi wasomi wote wanakimbilia CHASO.Vijana wa chaso wanatikisa chaguzi mbalimbali za Urais vyuoni mwao.Lakini je wanaandaliwa mazingira gani ya kukua kisiasa ndani ya baraza la Vijana?
Lakini mwisho,John heche naomba tumie akili yako na ya wenzako,Kuna haja gani ya kendekeza makundi ndani ya barza la vijana?kwanini kwenye mikutano yako hutoi nafasi kwa vijana flaniflani ambao wanaonekana hawapo upande unaouamini ndani ya chama?Weweni kiongozi hutakiwi kuegamia upande wowote..Lakini kesi za kugoma kutoa maiki za kuhutubia mikutanoni kwa vijana flani zimekuwa nyingi sana.
Je kuwanyima maiki ndio suruhisho la mogogoro wako na wao?Je BAVICHA inaundwa na vijana wa upande mmoja?
asanteni.

Ni hayo tu​
 
WanaJF,
Mara ya mwisho kuzungumzia undani wa wanasiasa ilikuwa mwezi January mwaka huu kwa kuwazungumzia wanasiasa mashuhuri Tanzania Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.Niliahidi nitarudi tena na mada hii hii kuwajadili wanasiasa wengine.Na nitakuwa nikifanya hivyo mara kwa mara nipatapo nafasi bila kubagua wanasiasa kwa itikadi zao.

Leo nitaomba kuwajadili wanasiasa wengine mashuhuri katika anga la Tanzania.Wanasiasa hao ni John Mnyika-Mbunge wa Jimbo la Ubungo na John Heche-Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa.Nimewachanganya Pamoja kwa sababu wanashabihiana kwa mambo mengi lakini lamsingi likiwa Itikadi yao na misimamo yao kuhusu mambo ya msingi.

Mafanikio Misimamo yao:

-Kwanza wote hawa ni vijana na wamekuwa kama Role model kwa vijana wengi si kwa vijana wa CDM tu bali kwa vijana wa Itikadi zote.
-Ni vijana wenye misimamo isiyoyumba na wanakitetea kwa nguvu kile wanachokiamini bila kuogopa vitisho kutoka kwa yeyote.
-Kutokana na Karama za kiuongozi walizo nazo wamefanikiwa kufika nafasi za juu kabisa za uongozi kwa umri wao.John Mnyika mbali ya kuwa mbunge anayeongoza jimbo kubwa kabisa la Ubungo pia yeye ndiye msemaji mkuu wa chama chake cha CDM.John Heche ni kiongozi wa BAVICHA Taifa na mjumbe wa Kamati kuu ya chama chake CDM,chombo cha ngazi ya juu kabisa ndani ya chama chake.
-Vijana hawa wamekuwa wakifanya kazi kubwa ndani ya chama chao hasa kuimarisha chama vijijini na kukipigania chama.Mafanikio yoyote ndani ya CDM huwezi kuwakosa hawa vijana.
-Ni vijana ambao hawaamini katika siasa za makundi.Sikuzote wanaamini katika CDM Imara.Huwezi kuwakuta wakishabikia majina ya watu ndani ya chama chao bali wanashabikia sera na Itikadi ya CDM.
-Ni wanyenyekevu,watiifu na wanapenda kukosolewa.
-Vijana hawa wana heshima kubwa kwa viongozi wao ndani ya Chama na huheshimu siku zote busara za wazee.Lau wakikosoa basi hukosoa kwa staha kubwa.

Changamoto zao:

-John Heche na John Mnyika pamoja na sifa zote zilizotajwa juu bado wanachangamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwafikia vijana wengi zaidi hasa wa vijijini na kuwapa somo la Uraia hususan umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura kwani inaonekana vijana wengi ni wafuasi sugu wa CDM lakini hawajiandikishi wala kupiga kura.
-Kutokana na umaarufu wao wamejitokeza vijana wengine wenye chuki na mafanikio yao na kuwaandama kwa matusi na maneno ya uongo hasa kupitia mitandao ya kijamii.Hata hivyo bado vijana hawa wameonyesha subira kubwa kwa mashambulizi hayo.Hawajakata tamaa bali wanasonga mbele.

Kwa Viongozi wakuu wa CHADEMA.

-Kutokana na yote niliyoandika juu viongozi wakuu wa CDM wanapaswa kuwatia moyo vijana hawa ili wasonge mbele zaidi na wasikatishwe tamaa na maadui wa CDM.
-CDM kama chama wanapaswa kuandaa vijana wasomi wanaofuata nyayo za kina Mnyika na Heche.Hata hivyo nafarijika kuona wapo vijana ndani ya CDM wenye uwezo wa kufuata nyayo hizi.Kwa mfano yupo kijana anayeitwa Ben Saanane,kwa wanaofuatilia siasa zake watagundua kwamba ni kijana anayeonyesha uvumilivu wa hali ya juu.Ben Saanane amewahi kupata misukosuko ya kisiasa lakini alisimama imara kutetea anchoamini.Hakuwahi kukashifu viongozi wake wa chama katika uficho au kwa uwazi.Ben anaamini CDM kama taasisi imara na siyo makundi ya watu.Ninaweza kusema Ben Saanane ni matunda ya kazi nzuri za kina Mnyika na wenzake.Hata hivyo chama kiandae vijana wengi zaidi wa kufuata nyayo za kina Mnyika na Heche na siyo Ben Saanane tu...

WanaJF Karibuni kwa mjadala!

Sina uhakika sana ikiwa utafiti wako hapo juu una ithibati, lakini naona nina hoja ya kuchangia,nitachepuka kidogo isipokuwa binafsi nitawachambua hao vijana kwa kujadili taasisi waliyopo (CHADEMA)

CDM kama chama kikuu cha upinzani hapa Tanzania kwa vyovyote vile lazima kikutane na changamoto lukuki katika harakati zake za kuingia ikulu, mara kadhaa nimekuwa nikimsikia Dr. Slaa akiwajibu mahasimu wake wa kisiasa (CCM) pale wanapolalama kwamba CMD muda wote wapo kuangalia mapungufu tu na kuyasema bila kutaja hata mazuri ya CCM, lakini yeye bila kumung'unya maneno alitoka na kusema wao CHADEMA hawapo kwa ajili ya kusifia mazuri ya CCM, maana kama ni mazuri hawaoni haja ya kuyataja.

Sasa kwa msingi huu, binafsi naona udhaifu mkubwa sana wa CDM kama sio wa Dr. Slaa, nafikiri huo ndo msimamo wa chama, hivyo BAVICHA ya kina Heche na wenzake wameendelea kulalamika kila kukicha kiasi kwamba kama utakuwa unafuatilia vizuri mikutano yao muda wote wanaeleza Rais kafanya nini....waziri kafanya nini..... wakati mwingine unaweza hata kubashiri mambo ambayo atakayoongea mara tu akianza.

My take: Siasa hizi zimepitwa na wakati, watanzania wamechoka kusikiliza watu wakilalamika tuuuuu! inapaswa sasa kwa uwezo mdogo walionao CDM waonyeshe kwa mfano; kama wanasema shule za kata hazina viwango, zitawaangukia wanafunzi hebu wajenge hata shule moja na wajinadi kwa kusema "Ikiwa tutaingia madarakani hizi ndo shule zenye viwango tutajenga" waseme na kutenda hivyo hivyo hata kwenye mambo kama visima vya maji, barabara za vijijini,zahati, ofisi za mitaa n.k

Kiukweli wananchi wamechoka kukusanyika kwenye mikutano wanapewa faraja ama machungu wanaporudi nyumbani kero ziko pale pale kwanza mkutano umewakawiza kwenda kutafuta kuni, kuchota maji maana ni ya shida, kwenda kutafuta vipimo zahati ya mbali,Inawezekana wanachoelezwa ni cha kweli lakini mwisho wa siku hawana jinsi zaidi ya kusubiri kipindi kingine cha uchaguzi waweze kufanya mabadiliko lakini pengine imebaki miaka 3 ndo uchaguzi mwingine sasa ndo kusema CDM wao watakuwa wakizunguka kulalamika tuuu! mi nadhani sio sahihi hebu watoke wafanye kwa mfano ndo njia peke itayowajengea imani na heshima kubwa kwa wapiga kula.

CHADEMA naweza kusema wamepanda mbegu mbaya sana kwa vijana wa kitanzania na watanzania kwa ujumla, Tabia ya kulalamika tuuuu na wengine sasa hata ukimuuliza kile acholalamika kwa kiasi gani ameona au anatambua athari zake, hajui chachote isipokuwa aliwahi kuwasikia viongozi wake wakilalamika, hii mbegu sio nzuri hata kidogo kuna wengine kabisa tunafahamu ugumu wa maisha yake sababu ni yeye mwenyewe lakini naye analalamika vijana au watu wa namna hii wapo kila kona ya nchi hii lakini ni lini hivi vyama vya upinzani vilisimama vikakemea vijana waache tabia ya kufanyiwa kila kitu? waache kukaa masikani na kusubiri maendeleo?

Kina Heche na Mnyika wamekuwa katika mkururo huo huo wa kulalamika tu kuonyesha madhaifu tu ya CCM na kusahau kuwaonyesha kwa mfano watanzania ni kipi wamefanya,najua watakuja watu wahoji juu ya fedha, lakini mi nasema wanaweza wakiamua, ujue CDM mpaka kimejipambanua kuwa ni chama kinachojengwa na matukio ni kweli kabisa!

Nilifarijika walau kwa mara ya kwanza kuona uongozi wa CDM( sikumbuki walikuwa ni wa wapi lakini sio makao makuu) walitoka na Greda kwenda kupanua nadhani mto msimbazi ili kusaidia wananchi waishio bonde la mto msimbazi wasipatwe maafa ya mafuriko, kitu kile ndo nataka iwe msimamo wa CDM Taifa na kila kiwango cha chama, mambo hayo ndo yatakayowajengea heshima kubwa na kuaminika zaidi kuliko kulalamika tu kila kukicha,mnawafundisha kitu kibaya sana watanzania kujipambanua nyie ni malaika siku ikitokea mkachukua nchi mbegu mlioipanda itawwatesa hata nyie wenyewe maana ndo mazoea! AKSANTENI.
 
Hii ni moja ya thread chache ambazo watu wengi wamejikita kwenye uchambuzi basi BEN atakuwa na kitu special I do wish him well in political life

Ni kweli ninaona kitu ambacho ni nadra sana
 
Karibu tena mkuu,
Nimependa namna ulivyojitolea kuwaelezea hawa Vijana wawili wa kisiasa ndnai ya CHADEMA.
Namimi nakuunga mkono mkuu kwamba wanatakiwa kutiwa moyo na kupewa nafasi zaidi ili wakieneze chama kwa mapana zaidi.
LAKINI MKUU,KATIKA UCHAMBUZI WAKO UMEAINISHA MAFANIKIO,CHANGA MOTO NA RAI YAKO KWA VIONGOZI WA CHADEMA.
Naomba niongeze hili katika uchambuzi wako,kwamba hawa vijana wawili wanaoonekana kushabihiana
WANAMAPUNGUFU HAYA HAPA,AMBAYO NI MUHIMU WAKAYAFANYIA KAZI

1.John Mnyika anafanya vizuri ndani ya JImbo lake kwa kiasi flani.lakini ili aweze kufanikiwa zaidi basi ni Muhimu akajitenga na siasa za kuattack watendaji wa serikali na kuwatolea amri iliwatimize shughuli za maendeleo ya jimboni mwake.
Kwa mfano>alipotoa masaa 48 maji yawe yanatoka jimboni kwake kwa watendaji wa DAWASCO hakuwa angalia kwamba yeye ni mwnasiasa na anowambia ni watendaji wa serikali.
Kwa maksudi wanaweza kumuangusha katika kufanikisha kile alicholenga kukifanya.
Pia mnyika anapaswa kuangalia namna anavyowaweka viongozi wake wa juu katika upeona upokeo wa kimatendo na kiushirikiano.Yeye ni mwanasiasa kijana sana na muda mrefu kwenye ulingo huu,basi kwa nafasi yake inatakiwa aangalie namna navyowatreat kinidhamu na kiutendaji kazi hawa viongozi wajuu wa chama.Hizi kelele tunazosikia nyuma ya pazia kwamba anatumika,au anamkubali sana mtu flani si jambo jema kwa ustawi wa chama.

2.John Heche akiwa kama wenyekiti wa BAVICHA bila kusuasua napenda kusema kunambo mengi ndani ya Baraza lake yamekwenda kombo.
John heche anatakiwa achukue hatua kuhakikisha yeye na makamu wake wanakuwa kitu kimoja.Hivi sasa nakili wazi viongozi hawa wawili wanaongea na kucheka kama binadamu lakini mioyoni mwao wanatofauti/mpasuko kubwa sana ya kiutendaji.
Heche anakambi yake(sitaki kuitaja) naye makamu mwenyekiti anawatu wake.Hii kwa uhai wa Baraza ni hatari sana,lazima Heche ajitambue kwamba yeye ni kiongozi mkubwa basi hana cha kusubiri zaidi ya kuhakikisha mambo yana kaa sawa.
Pia Heche tangu aingie madarakani kunajambo amabalo sijajua ama maksudi au kwa bahati mbaya ameamua kulitupa,kuliacha,kulitelekeza na kuto litupia macho kabisa ili hali ndio muhimili wa Vijana wasomi ndani ya chadema,Ndio shamba la kuvuna vijana wasomi wa chadema,Ndio chuo cha kuzalisha viongozi wa somi ndani ya chadema...Swala hilo ni CHASO.
CHASO-CHADEMA STUDENT ORGANIZATION imetelekezwa,haipo pamoja,inajikongoja.Karibia vyo vyote vya juu vya elimu ya kati vina vijana wa chadema ambao wamejikusanya kwa jitihada zao,wanajiongoza wanakiu ya ukombozi kupita maelezo.
Lakini baraza la vijana la chadema chini ya John Heche limeshindwa kuwaunganisha vijana hawa.hakuna uongozi wa CHASO kitaifa,Hakuna anayetambua viongozi wa chaso wanaomaliza muda wake wanakenda wapi?Heche hajui yawezekana hata idadi ya matawi ya chaso ndani ya chadema.
JOhn heche hatembelei kufungua matawi ya chaso,Heche hatembelei kuangalia Vijana hawa wa chasso kwenye matawi yao wanakabiliwa na matatizo gani.
John heche jitizame kama umekamilika kuhusu hili,CCM wanalia kuna vijana wanaharakati na wanamapinduzi wasomi wote wanakimbilia CHASO.Vijana wa chaso wanatikisa chaguzi mbalimbali za Urais vyuoni mwao.Lakini je wanaandaliwa mazingira gani ya kukua kisiasa ndani ya baraza la Vijana?
Lakini mwisho,John heche naomba tumie akili yako na ya wenzako,Kuna haja gani ya kendekeza makundi ndani ya barza la vijana?kwanini kwenye mikutano yako hutoi nafasi kwa vijana flaniflani ambao wanaonekana hawapo upande unaouamini ndani ya chama?Weweni kiongozi hutakiwi kuegamia upande wowote..Lakini kesi za kugoma kutoa maiki za kuhutubia mikutanoni kwa vijana flani zimekuwa nyingi sana.
Je kuwanyima maiki ndio suruhisho la mogogoro wako na wao?Je BAVICHA inaundwa na vijana wa upande mmoja?
asanteni.

Ni hayo tu​

Ha ha hahaaaaaaaaaaaaa.watu bana.umeona jinsi hawa jamaa uliokua ukiwatukana kila siku walivyojadiliwa kwa ustaarabu ukashindwa kuvumilia

Hongera kwa kuandika busara leo.
Moderators walikuumbua juzi kwa kuunganisha ID uliyotumia kumtukana Ben,Mnyika na Heche matusi ya nguoni kwa ID ya Libasket
 
Mkuu Tuntemeke
Thankyou very much.You have made my day.Kwa heshima nitaanza na hii post yako kwa jinsi ulivyochangia mada hii yangu.Hakika ulichofanya ni Positive Critisism.
Kama kweli vijana wa CDM mtataka kusaidia chama chenu basi michango yenu iwe kama huu uliotoa.Mkuu watu wengi ndani ya JF walikuwa wanakushambulia awali kwa sababu ya Personal attacks zako kwa baadhi ya watu.Natamani viongozi wa CDM wasome mchango wako huu wa leo.

John Heche-Popote ulipo nakushauri jisajili JF kama verified user,hii itakusadia kujibu hoja hasa zenye mawazo chanya.Haina haja ya kuhofia kwa sababu bado naamini umefanya kazi kubwa sana ndani ya chama chako kama wachangiaji wanavyoonyesha kwenye mjadala huu

Again Thankyou Tuntemeke.
 
Kuhusu John Mnyika siwezi kupingana na wewe mtoa mada hata kidogo,ila nina tatizo na mashaka kwa bwana John Heche kwani nimeanza kumfahamu na kuwa nae karibu toka mwaka 2006 - 2009 tukiwa chuo cha mtakatifu Augustino Mwanza na ntapingana na wewe kutokana na sababu zifuatazo:-

1.Uwezo wake wa kufikiri. Natilia shaka sana credit ulizompa John Heche kwa sababu alipokua mwaka wa kwanza katika chuo cha Mtakatifu Augustino counter book yake kwa juu alikua kaandika Pum...u University.

2.Ni msaliti na hana msimamo. Mwaka 2008 kulikua na Uchaguzi wa kumchagua Rais wa serikali ya wanafunzi SAUT,na bwana John Heche aliamua kumgeuka Mgombea aliyekua anasoma nae darasa moja Education na kuamua kumsupport mgombea aliyekua aliyekua anasoma Sociology,hii ilisababisha members wa darasa lake kumuijia juu na hivyo ikamfanya abdilishe uamzi wake na swala hili hadi leo liliteta uhasama kati yake na Bwana Mnyeti ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Misungwi (Mawe matatu).Pili alisaliti wenzake katika harakati za kuanzisha mgomo kwa watu wa Education mwaka 2008 pale walipoamua kwenda katika ofisi ya Makam mkuu wa chuo yeye kama mhamasishaji siku ilipofika alipanda bus na kwenda Tarime hivyo kuwaachana wenzake wakiandamana hivyo kuambulia kupewa barua za onyo na wengine kusimamishwa chuo wakati yeye kama kiongozi akitokomea mbali.

Asanteni.
1.

Mkuu Lobapula,
Nakushukuru kuchangia mada hii.

Nafurahishwa na mchango wako na comments zako kuhusu John Heche.Hata hivyo bado naamini John Heche ni Star ndani ya chama chake.Amefanya kazi kubwa na anaendelea kufanya kazi.Hata hivyo haimaanishi kwamba John Heche ni malaika na hana mapungufu.La hasha.

Hata hivyo mkuu sioni muunganiko wowote na hayo uliyoyataja juu na utendaji kazi wake ndani ya Bavicha.Mengine nawza kusema ni ya kibinafsi sana.

Hata hivyo bado nasisitiza umuhimu wa John Heche kujisajili JF kama verified user ili kujibu straight hoja kama hizi.

Again Thankyou Lobapula
 
Hii thread ni nzuri sana yani watu wanajibu kwa hoja pasipo kejeli.
Big up fmpiganaji na mods.

Mkuu Promi demana.
Asante sana.Ninawashukuru sana wanaJF kwa jinsi wanavyochangia thread hii.Hakika tukiendelea kufanya hivi kwa thread hii na nyinginezo heshima ya JF itazidi kupanda.
Tupingane kwa hoja na siyo kufanya mashambulizi kwa watu binafsi na matusi.

Big up JF members!
 
Hii ni moja ya thread chache ambazo watu wengi wamejikita kwenye uchambuzi basi BEN atakuwa na kitu special I do wish him well in political life

Mak89
Thankyou for noted this.Lets us assist them to do more!
 
kaka sasa unaweza sema uko tayari kabisa kumuunga heche mkono katika vita aliyonayo ya kupambana na CCM na kweli utaacha vile vya vikao vya pale (kapuni) ambavyo agenda kuu huwa ni kumdhoofisha huyu bwana mdogo wa chama cgenu kupitia vijana HECHE kwa kweli sisi humu asilimia 100 hatupendezwi na siasa za uvunguni anazofanya mwenzako,nyakarungu, mwampamba, mchange, unasemaje kuhusu mienendo hii na swali langu la utayari wako naomba nipate jibu maana tunapenda kuwaona field na HEche sio humu mitandaoni kwa majina mbalimbali

Ustaadh,

Asante sana.Siku zote BAVICHA ni kubwa kuliko Ben Saanane na Heche.Sote tunaongozwa na dhamira ya Chama kuchukua Dola na kusimamia mchakato wa mabadiliko.Sote tuna common Enemy.Ni lazima tukabiliane naye kwa umoja

Ni muda muafaka zaidi kwetu kubadili mtazamo na kukumbatia siasa za mazoea,hatutaki siasa za kugombani fito na kuachana na ajenda ya ujenzi.Hatutaki kumpa faida adui wa mabadiliko .Tukifanya hivyo tutakua tumejidhoofisha sisi,tumewakatisha tamaa vijana na kumpa nguvu adui yetu

Kuhusu watu wengine,Sitawajadili
 
Ha ha hahaaaaaaaaaaaaa.watu bana.umeona jinsi hawa jamaa uliokua ukiwatukana kila siku walivyojadiliwa kwa ustaarabu ukashindwa kuvumilia

Hongera kwa kuandika busara leo.
Moderators walikuumbua juzi kwa kuunganisha ID uliyotumia kumtukana Ben,Mnyika na Heche matusi ya nguoni kwa ID ya Libasket
Mods naoniwatu kama mimi na wewe,nimeripoti Tatizo langu kwao.Nategemea wanalishughulikia.
Mbali na hapo asante kwa kutambua mchango wangu
 
Ben Saanane,
Kwa kweli ana sifa za kuwa kiongozi namkubali sana kuna kipindi cha miaka ya nyuma alikuwa anatukanwa sana humu JF watu wanabandika picha zake na za wadada wanamdhalilisha lakini mwenyewe alikuwa anajibu kwa hoja bila kashfa wala kejeli...Jamaa anatisha.

Mkuu Ritz nimeamini mchango wako kwenye hii thread una niya njema.Hongera sana na tupo pamoja.
 
Last edited by a moderator:
Ustaadh,

Asante sana.Siku zote BAVICHA ni kubwa kuliko Ben Saanane na Heche.Sote tunaongozwa na dhamira ya Chama kuchukua Dola na kusimamia mchakato wa mabadiliko.Sote tuna common Enemy.Ni lazima tukabiliane naye kwa umoja

Ni muda muafaka zaidi kwetu kubadili mtazamo na kukumbatia siasa za mazoea,hatutaki siasa za kugombani fito na kuachana na ajenda ya ujenzi.Hatutaki kumpa faida adui wa mabadiliko .Tukifanya hivyo tutakua tumejidhoofisha sisi,tumewakatisha tamaa vijana na kumpa nguvu adui yetu

Kuhusu watu wengine,Sitawajadili

Kwa Uvccm hii mjipange sana.vipaji vyenu vya propaganda mvinoe la sivyo uvccm haikamatiki.vua gwanda
 
Karibu tena mkuu,
Nimependa namna ulivyojitolea kuwaelezea hawa Vijana wawili wa kisiasa ndnai ya CHADEMA.
Namimi nakuunga mkono mkuu kwamba wanatakiwa kutiwa moyo na kupewa nafasi zaidi ili wakieneze chama kwa mapana zaidi.
LAKINI MKUU,KATIKA UCHAMBUZI WAKO UMEAINISHA MAFANIKIO,CHANGA MOTO NA RAI YAKO KWA VIONGOZI WA CHADEMA.
Naomba niongeze hili katika uchambuzi wako,kwamba hawa vijana wawili wanaoonekana kushabihiana
WANAMAPUNGUFU HAYA HAPA,AMBAYO NI MUHIMU WAKAYAFANYIA KAZI

1.John Mnyika anafanya vizuri ndani ya JImbo lake kwa kiasi flani.lakini ili aweze kufanikiwa zaidi basi ni Muhimu akajitenga na siasa za kuattack watendaji wa serikali na kuwatolea amri iliwatimize shughuli za maendeleo ya jimboni mwake.
Kwa mfano>alipotoa masaa 48 maji yawe yanatoka jimboni kwake kwa watendaji wa DAWASCO hakuwa angalia kwamba yeye ni mwnasiasa na anowambia ni watendaji wa serikali.
Kwa maksudi wanaweza kumuangusha katika kufanikisha kile alicholenga kukifanya.
Pia mnyika anapaswa kuangalia namna anavyowaweka viongozi wake wa juu katika upeona upokeo wa kimatendo na kiushirikiano.Yeye ni mwanasiasa kijana sana na muda mrefu kwenye ulingo huu,basi kwa nafasi yake inatakiwa aangalie namna navyowatreat kinidhamu na kiutendaji kazi hawa viongozi wajuu wa chama.Hizi kelele tunazosikia nyuma ya pazia kwamba anatumika,au anamkubali sana mtu flani si jambo jema kwa ustawi wa chama.

2.John Heche akiwa kama wenyekiti wa BAVICHA bila kusuasua napenda kusema kunambo mengi ndani ya Baraza lake yamekwenda kombo.
John heche anatakiwa achukue hatua kuhakikisha yeye na makamu wake wanakuwa kitu kimoja.Hivi sasa nakili wazi viongozi hawa wawili wanaongea na kucheka kama binadamu lakini mioyoni mwao wanatofauti/mpasuko kubwa sana ya kiutendaji.
Heche anakambi yake(sitaki kuitaja) naye makamu mwenyekiti anawatu wake.Hii kwa uhai wa Baraza ni hatari sana,lazima Heche ajitambue kwamba yeye ni kiongozi mkubwa basi hana cha kusubiri zaidi ya kuhakikisha mambo yana kaa sawa.
Pia Heche tangu aingie madarakani kunajambo amabalo sijajua ama maksudi au kwa bahati mbaya ameamua kulitupa,kuliacha,kulitelekeza na kuto litupia macho kabisa ili hali ndio muhimili wa Vijana wasomi ndani ya chadema,Ndio shamba la kuvuna vijana wasomi wa chadema,Ndio chuo cha kuzalisha viongozi wa somi ndani ya chadema...Swala hilo ni CHASO.
CHASO-CHADEMA STUDENT ORGANIZATION imetelekezwa,haipo pamoja,inajikongoja.Karibia vyo vyote vya juu vya elimu ya kati vina vijana wa chadema ambao wamejikusanya kwa jitihada zao,wanajiongoza wanakiu ya ukombozi kupita maelezo.
Lakini baraza la vijana la chadema chini ya John Heche limeshindwa kuwaunganisha vijana hawa.hakuna uongozi wa CHASO kitaifa,Hakuna anayetambua viongozi wa chaso wanaomaliza muda wake wanakenda wapi?Heche hajui yawezekana hata idadi ya matawi ya chaso ndani ya chadema.
JOhn heche hatembelei kufungua matawi ya chaso,Heche hatembelei kuangalia Vijana hawa wa chasso kwenye matawi yao wanakabiliwa na matatizo gani.
John heche jitizame kama umekamilika kuhusu hili,CCM wanalia kuna vijana wanaharakati na wanamapinduzi wasomi wote wanakimbilia CHASO.Vijana wa chaso wanatikisa chaguzi mbalimbali za Urais vyuoni mwao.Lakini je wanaandaliwa mazingira gani ya kukua kisiasa ndani ya baraza la Vijana?
Lakini mwisho,John heche naomba tumie akili yako na ya wenzako,Kuna haja gani ya kendekeza makundi ndani ya barza la vijana?kwanini kwenye mikutano yako hutoi nafasi kwa vijana flaniflani ambao wanaonekana hawapo upande unaouamini ndani ya chama?Weweni kiongozi hutakiwi kuegamia upande wowote..Lakini kesi za kugoma kutoa maiki za kuhutubia mikutanoni kwa vijana flani zimekuwa nyingi sana.
Je kuwanyima maiki ndio suruhisho la mogogoro wako na wao?Je BAVICHA inaundwa na vijana wa upande mmoja?
asanteni.

Ni hayo tu​

Mkuu Tuntemeke.
Nimeisoma hii Post yako mara tatu.Najua unafahamu mimi na wewe tunatofautiana sana hapa jamvini.Lakini kwa leo naomba nikupongeze kwa mchango wako.
Sisi wengine hatukatai viongozi kukosolewa,tunachokipinga ni matusi na ukosefu wa adabu na kujadili maisha binafsi ya watu.
Mkuu Tuntemeke Kila la kheri.
 
hawezi kupambana na combination ya mboni mhita na sadifa wa Uvccm.Kama ni shule hata sadifa ana masters na wakili Anthoni Mavunde mjumbe wa baraza UVCCM anayo
Ana kazi sana kuongoza bavicha mwakani mbele ya hawa wadomi wa Uvccm.Kwa bahati nzuri mamluki wake paul makonda na akina felician tuliwadhibiti uvccm .hataweza dogo huyo

Captain Green,

Sikutaka kujibu hizi post zako lakini unazidi kupotosha.

Sikuwahi kuingilia uchaguzi wenu.Kuna wagombea huko ambao walikua marafiki zangu wa Kawaida kama Felician na wengine.

Vijana tuache siasa hizi za uadui na kupanfikiziana chuki pasipo sababu

Nakushangaa unapojisifu kwamba BAVICHA haiwezi kupambana na UVCCM ya hao uliowataja bila kugusia ushiriki wako katika kugakikisha wanapita kwa Rushwa

BAVICHA ni nguzo muhimu kwa chama katika kupambana na ufisadi.Uongozi huo ni matokeo ya ufisadi utaweza vipi kusimama mbele ya vijana pale Machinga Complex na kuwahubiria vijana wajunge na UVCCM? Uongozi huo mpya ambao wewe umesimamia mchakato wa rushwa kuhakikisha wanashinda utaweza vipi kuwakemea vigogo wauza madawa ya kulevya wanaowatumia vijana? Je,hao wasomi wanaolalamikiwa na wenzao kutumika watashindwa vipi kutumika katika utungaji au utekelezaji wa sera na miradi ya kifisadi?

Je,wataweza vipi kusimamia sera ya kuwa na Baraza huruvla vijana la Taifa ambalo litakua mwiba kwa wakandamizaji wa vijana katika sekta zote?

Je,watawezaje kukosoa au kushauri sera inayopingana na utekelezaji wa kilimo kwanza kitakachowafanya vijana kuwa manamba kwenye mashamba makubwa?

Je,kipindi hiki ambacho tumegundua nishati ya Gesi,hivi kweli uongozi uliopatikana hivi utaweza kuwa objective katika utungaji wa sera ya gesi kwa manufaa ya vijana wa sasa na watoto wetu?

No,kwa maoni yangu naona vijana wa aina hii hawana ajenda za vijana bali wana ajenda za wazee wao waliolifikisha taifa hapa.

Vijana hao wamethibitisha jinsi wanavyokomazwa na Rushwa ndani ya chama chao kwa ushirikiano wa karibu kutoka kwa kaka zao na wazee ndani ya hicho chama

Ni jukumu la BAVICHA kuwaokoa vijana na hata hao vijana wa UVCCM ambao wapo ndani ya hicho chama kwa maslahi tu,tutawakomboa kifikra.Hata wewe mkuu siku moja utakuja tu CHADEMA.Tutakukomboa hata wewe kifikra
 
Mkuu Tuntemeke.
Nimeisoma hii Post yako mara tatu.Najua unafahamu mimi na wewe tunatofautiana sana hapa jamvini.Lakini kwa leo naomba nikupongeze kwa mchango wako.
Sisi wengine hatukatai viongozi kukosolewa,tunachokipinga ni matusi na ukosefu wa adabu na kujadili maisha binafsi ya watu.
Mkuu Tuntemeke Kila la kheri.

Mkuu,
Kwenye red hapo ndipo msimamo wangu ulipo kwamba,Kila kiongozi anamakosa yake tena hawa wa kisiasa ndio kabisaa wanamakosa mengi sana.Hivyo basi tuwakosoe kwa hoja,tuwakosoe bila kujali itikadi ya chama,maslahi ndani ya chama,Umaarufu wake kwa taifa hili.
Hapo kwenye blue nakuunga mkono matusi si fungu jema katika kusimamia jambo lolote,na sheria za JF haziruhusu.
Napinga matusi,naunga mkono hoja kwa hoja.
 
Back
Top Bottom