Undani wa John Mnyika na John Heche

Undani wa John Mnyika na John Heche

Kumbe huo ndo undani wao? Duh!! inabidi utuambie ulitumia nyenzo gani kufanya utafiti kama huu unaoonyesha umahiri wa mnyika na henche hasa wakiwa ni wapiga POROJO wakuu wa chadema. Ujasiri na umahiri wa mtu si kelele na maneno mengi bali ni utendaji wao wa kazi za kuwaletea wananchi maendeleo. Njoo na hoja za msingi utuambie hadi sasa mnyika amewatetea na kuwasaidia vipi wananchi wake wa jimbo la Ubungo? Bado hatujaona mafanikio yao, inabidi warudi tena kwenye kile cha cha kikristo cha ujerumani (CDU) wakajifunze tena namna nzuri ya kuwabatiza watanzania.

Mkuu wangu Lali

Mtu yeyote mstaarabu akisoma hoja yako atakupuuza tu kwa sababu umeonekana ni mtupu kichwani.

Binafsi ninaogopa kukuonyesha mazuri aliyofanya Mnyika kwa sababu tayari umeshajitanabaisha wewe ni mbaguzi wa hali ya juu ambaye Mwl Nyerere tayari alishatuonya tuwaogope watu wa aina yako kama Ukoma.

Kwa mtu mwenye akili timamu kabisakabisa huwezi kusema kina Mnyika wakasomee Kubatiza watu.Mungu akusaidie upone huo ugonjwa ulio nao wa ubaguzi wa kidini.
 
hapo umeongea ukweli nakupa big up xana CDM NDO TEGEMEO JIPYA KWA WATANZANIA
 
Toka kwa mara ya kwanza nimemuona kamanda heche akigombea udiwani kata ya tarime mjini nilitegemea kuona matunda yake kwa taifa letu,alimpigania charles nyanguru aliyekisaliti chama na kumuwezesha kuwa mbunge,heche ni kamanda wa makamanda hana hoja wala agenda tofauti na kuleta mabadiliko kwa watanzania,hakika Heche ni jembe sana tena sana,i wish kama vijana tungeungana wote bila itikadi zetu kuwatambua vijana wanaotambua kazi na majukumu yao kwa taifa letu mgando.

Comrade Apex

Hakika umeongeza jambo jingine kwenye mada yangu kumhusu John Heche.

John Heche ni mvumilivu sana.Nitafafanua kidogo.Kwenye uchaguzi mkuu uliopita John Heche alitaka kugombea ubunge Jimbo la Tarime lakini akashindwa kwenye kura za maoni na Mwita Mwikabe Waitara.Mwingine aliyeshindwa kwenye kura za maoni ni aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Charles Mwera.Kutokana na uroho wa madaraka Charles Mwera akakimbilia CUF ili apate nafasi ya kugombea.

Lakini tunaona John Heche baada ya kushindwa kwenye kura za maoni hakuhama chama chake.Alikubali kushindwa na akaendelea kupigania chama chake.Tena kwa kujitoa zaidi na kuzunguka nchi nzima na mgombea urais Dr Wilbroad Slaa.

Isitoshe John Heche hakutukana viongozi wake kwenye mitandao ya kijamii kwa vile eti hakupitishwa kugombea ubunge.Wala John Heche hakuanzisha kundi la kumuunga mkono kisiri kuhujumu chama.Uvumilivu wa John Heche ndiyo umemfanya ale mbivu leo kwa kuwa kiongozi mkuu wa Bavicha nchini.Na ndiyo maana leo wengine tunasimama hadharani kupongeza vijana mfano wa Ben Saanane kwamba hakupata nafasi ya kuwa Mkiti wa Bavicha lakini ameendelea kuheshimu chama na viongozi wake.Ben ameonyesha wazi kushindwa kupata nafasi ya uongozi suluhu siyo kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii na kujisajili kwa ID feki kwa lengo moja tu la kuwatukana matusi ya nguoni viongozi wakuu na kuelezea maisha yao binafsi tena ya unyumba kana kwamba wao ni malaika.

John Heche ametoa somo kubwa kwa vijana wenzake kwamba hakuna jambo bora kama SUBIRA.Nafasi za uongozi zipo nyingi sana kwamba ukikosa nafasi hii leo kesho utapata nyingine.Vijana wetu wajifunze somo hili na wakielewe.

Nakushukuru sana Comrade Apex.
 
Hawa ni VICHWA na ni MAJEMBE huwezi kuwalinganisha na hao wa upande mwingine

Mkuu swrc

Mkuu wangu umeongeza jambo moja la wazi kabisa.Kwamba ni kweli hata ukifuatilia sana bunge ukilinganisha hoja za vijana wa vyama mbalimbali halafu ukalinganisha na hoja za John Mnyika utagundua tofauti kubwa kati yao.

Ama unaweza kuangalia wenyeviti wa vijana wa vyama vyote halafu ukamlinganisha John Heche pia utagundua tofauti kubwa kati yao.

Ama fuatilia hoja za Ben Saanane hapa jamvini halafu linganisha na hoja za makada wa vyama vingine hapa jamvini utagundua pia tofauti kubwa kati yao.Unaweza kudhani CDM ina chuo maalum cha kufundisha makamanda wake kwa ustadi wa kujenga hoja wa Ben.

Niseme tu CDM wana bahati kubwa ya kupendwa na vijana makini na machachari.CDM izidi kuwapika na kuwaimarisha vijana hawa kwa mustakabali wa chama na Taifa kwa ujumla.

Comrade swrc nakushukuru sana!
 
Kwa muda muafaka, tunayoyaona leo yalishasemwa tangu zamani.
Hakika mkuu... But kiukweli heche anajiamini mno.... Ndio mana napata wasiwasi na waitara kama kwel ni mkurya original
 
Back
Top Bottom