Undani wa John Mnyika na John Heche

Undani wa John Mnyika na John Heche

JangalaFalsafa unachokisema ndo kitu nachokihitaji, uko sahihi kabisa, CDM au kambi ya upinzani kwa ujumla wanapaswa kujitathmini kila wakati na kujielekeza katika mambo ya msingi yatakayowaletea heshima kubwa na watanzania walio wengi kuwaamini,wasiwe na papara za kuwalazimisha watanzania kuwaamini, kitendo cha kuaminika hakilazimishwi kitakuja automatically ikiwa wananchi wataridhika na utashi wa kweli katika kuwaletea mabadiliko.

BAVICHA wanaweza wakawa mstari wa mbele katika kuwaunganisha vijana wa Tanzania na kuwaongoza katika harakati za kujiletea kipato, Nguvu ya umma isitumike katika maandamano tu watumie nguvu ya umma katika shughuli za harambee ili kuwajengea uwezo vijana na mwisho wa siku hawa ndo watakichangia chama katika harakati zenu za M4C,au anzisheni utaratibu popote pale katika nchi hii itengwe hata siku moja kila mwisho wa mwezi vijana nchi nzima wafanye shughuli za kijamii, utaratibu huu upo Rwanda, upo Burundi mtakuwa walau positive katika Taifa hili vinginevyo kuna baadhi ya watanzania wataendelea kuwaona ni watu wa fujo fujo hivi, hamna ustaarabu hamna jema katika nchi hii licha ya michango mizuri bungeni kwa bahati mbaya si watu wote wanaweza kufanya tathmini kwa kupitia bunge......

Hili la kutenga siku kwa ajili ya shughuli za kijamii tuko pamoja

Huu ni moja wapo wa mipango tuliyo nayo.
 
Hili la kutenga siku kwa ajili ya shughuli za kijamii tuko pamoja

Huu ni moja wapo wa mipango tuliyo nayo......

Naona hata nyie bado mna ugonjwa ule ule "tuna mpango"....."upembuzi yakinifu"...... "survey"......"design" mpaka lini?

kumbukeni mnafanya siasa sio kujenga madaraja! BAVICHA sijui kama mnafahamu kuwa vijana wa kitanzania hawana common agenda!! na waliowengi hawajitambui, kinahitajika chombo makini cha kuwaweka pamoja bila kujali itikadi zao.

Anzisheni haraka utaratibu wa kazi za harambee za kusaidia jamii, katika hili hata vijana wasio wanachama wenu kama mimi tutashiriki na wengi watajiunga na chama chenu na watanzania watawaamini waliowengi.
 
Naona hata nyie bado mna ugonjwa ule ule "tuna mpango"....."upembuzi yakinifu"...... "survey"......"design" mpaka lini?

kumbukeni mnafanya siasa sio kujenga madaraja! BAVICHA sijui kama mnafahamu kuwa vijana wa kitanzania hawana common agenda!! na waliowengi hawajitambui, kinahitajika chombo makini cha kuwaweka pamoja bila kujali itikadi zao.

Anzisheni haraka utaratibu wa kazi za harambee za kusaidia jamii, katika hili hata vijana wasio wanachama wenu kama mimi tutashiriki na wengi watajiunga na chama chenu na watanzania watawaamini waliowengi.

Mkuu wangu Shibalanga

Hoja ya Msingi kabisa.Umetoa ushauri mzuri sana kwa hawa vijana wa CDM.Ni Imani yangu Mnyika,Heche,Ben na vijana wenzao wameona ushauri huu makini.

Ndiyo maana nasema sikuzote jukwaa hili ni la watu makini wanaoweza kutoa ushauri kwa maslaha mapana ya nchi yetu.

Kwa wale wanaodhani upinzani ni kuporomosha matusi ya nguoni kwa viongozi unaotofautiana nao wajue wanajiaibisha sana.

Mkuu Shibalanga Asante sana.!
 
Ni kweli na ukanda upunguzwe , CDM ni ya kaskazini,kusini,mashariki ,magharibi na kanda ya kati,viti maalumu kusini hata kimoja????? ili kuonyesha sura ya kitaifa!!!!!
 
Nashukuru Mkuu, lakini Watz lazima wafumbe macho wapite kimya kimya kwenye post yako, wakidhani wanamkomoa mtu, kumbe wanajikomoa wenyewe!
Nguvu ya UMMA ipo? Why isitumike? Mfano tu, kila tawi la liwaunganishe vijana, tena bila kujali itikadi zao za vyama, wawe na mradi wowote wa maendeleo, hata kufuga kuku, kulima, ama kufyatua tofali, wenyeviti wa Bavicha wawe wanawatembelea na kuwahimiza, miaka miwili kila mwanakikundi ana baiskeli yake, unadhani wangapi wangejenga imani na chama?
UONGOZI ni UBUNIFU! Hata michango ya HARAKATI, ingetoka huko! Mnang'ang'ana tu changieni chama, m4c, n.k hamjui wanazitoa wapi? Wengine wanakaba wapate hela ya kuchangia, inakuwa yaleyale unatoa moja unaweka moja!
Uongozi ni Ubunifu!
Mungu wetu anaita sasa!

Comrade JingalaFalsafa

Haya ndiyo maneno sasa.Akina Mnyika wajue wanapaswa wajue bado wana kazi pevu ili kukamilisha kazi ya ukombozi waliyoamua kuifanya.

Umeongeza Changamoto inayopaswa kufanyiwa kazi tena kwa haraka kwa usitawi wa CDM,Bavicha na Taifa kwa Ujumla.

Hii ni kazi ya kushirikiana vijana wote.Isiwe tu kazi ya Mnyika,Heche na kina Ben.Nawashauri sasa wale vijana waliokuwa wameamua kuingia msituni kwa lengo moja tu la kutukana na kukashifu viongozi wao wajirudi washirikiane na wenzao.Vijana hawa wajue kufikia mafanikio sio kutumia mitandao kuzungumzia maisha binafsi ya viongozi wao tena kwa matusi.

Vijana wote watumie JF,FB,Tanuru na mitandao mingine kuelimisha jamii na kusaka maendeleo ya Taifa lao.Siku zote naamini kijana anayetumia mitandao hii kutukana viongozi wake hana tofauti na kichaa muokota makopo.

Mkuu JingaLafalsafa Asante sana.
 
wote ni wakristo.. Mfumo kristo

Mkuu Black Bat,

Nilitaka nisikujibu lakini nikaona huenda nikifa nikaulizwa kwanini sikukusaidia.

Mkuu wangu kweli mpaka leo upi kwenye Blanketi la udini? Hebu jiulize dini uliyo nayo wewe inakusaidia chochote katika kupata mlo.wako wa kila siku? Yaani nina maana ukienda dukani ukitaja tu dini yako unapewa kila kitu?

Hasha mkuu wangu.Acha kujiaibisha kiasi hiki.Kwa maana nyingine kuwasema hao kwa kuangalia majina yao eti ni mfumo Kristo unamaanisha nini? Kwa maana yako tusema kwa kuangalia majina ya Rais wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Tanzania haraka haraka tuseme ni Mfumo Islam? Looo...Huu ni upofu uliopitiliza.

Mkuu Fanya kazi kwa bidii achana na ujinga na ukichaa wa Udini kwani utakuangamiza wewe mwenyewe.

Pole sana mkuu wangu..!
 
alianza mienendo ya kuzunguka na wale jamaa wenye ID nyingi humu JF wakampa sumu balaa binti yetu mimi ni mmoja wa watu niliyefanikiwa kuhudhuria graduation yake pale mabibo nilimsikia bwana HECHE ambaye ni mwkt wake akiteta na kuwaondoa hofu ndugu zake shonza kuwa ana mpango wa kumgroom kisiasa huyu binti ili naye awe ni alama ya nini lilikuwa lengo la bavicha lakini badae nilisikitika kumsikia mimi kwa sikio langu mdogo wetu huyu akijitapa kuwa ntamfuta heche kwenye siasa na ntamwaibisha nilichemka mwili wote jamani vijana wetu jaribuni kuwa na subira na muelewe screening ya mambo ni kitu cha ziada

Kiribo

Kama kweli ulichoandika ni sahihi basi ninaanza kuamini ule usemi usemao 'KUNGURU HAFUGIKI'
 
JangalaFalsafa unachokisema ndo kitu nachokihitaji, uko sahihi kabisa, CDM au kambi ya upinzani kwa ujumla wanapaswa kujitathmini kila wakati na kujielekeza katika mambo ya msingi yatakayowaletea heshima kubwa na watanzania walio wengi kuwaamini,wasiwe na papara za kuwalazimisha watanzania kuwaamini, kitendo cha kuaminika hakilazimishwi kitakuja automatically ikiwa wananchi wataridhika na utashi wa kweli katika kuwaletea mabadiliko. BAVICHA wanaweza wakawa mstari wa mbele katika kuwaunganisha vijana wa Tanzania na kuwaongoza katika harakati za kujiletea kipato, Nguvu ya umma isitumike katika maandamano tu watumie nguvu ya umma katika shughuli za harambee ili kuwajengea uwezo vijana na mwisho wa siku hawa ndo watakichangia chama katika harakati zenu za M4C,au anzisheni utaratibu popote pale katika nchi hii itengwe hata siku moja kila mwisho wa mwezi vijana nchi nzima wafanye shughuli za kijamii, utaratibu huu upo Rwanda, upo Burundi mtakuwa walau positive katika Taifa hili vinginevyo kuna baadhi ya watanzania wataendelea kuwaona ni watu wa fujo fujo hivi, hamna ustaarabu hamna jema katika nchi hii licha ya michango mizuri bungeni kwa bahati mbaya si watu wote wanaweza kufanya tathmini kwa kupitia bunge.

Shibalanga

Umetoa mchango mkubwa sana wa mawazo.Ni imani yangu wakuu wa Chama na Bavicha wataufanyia kazi ushauri wako.Hakika JF ni kisima cha Hekima.
 
Asante mkuu kwa kutambua umuhimu wa CHASO kwa ustawi wa chadema imara ya yakisasa.

...........

Tuntemeke

Kwa mara nyingine nikushukuru tena kwa kuendelea kuongeza nyama kwenye mada yangu.

Mimi ni muumini mkubwa wa siasa za CDM za kujijenga kwa wasomi.Ukiangalia wabunge wengi wa CDM utagundua kazi ya kuwashika vijana wasomi iliasisiwa siku nyingi huko nyuma na viongozi hawa wa CDM.Hakika kina Mbowe walifanya kazi kubwa.

Hata ukiangalia vijana hawa wanaojadiliwa leo kwenye mada hii Mnyika,Heche na Ben utagundua ni kwa sababu ya kazi kubwa iliyokwishafanywa kujikita kwa wasomi vyuoni.Tujiulize leo mbona vijana hawa wasomi hawakwenda chama kingine?

Mkuu wangu nikuunge mkono asilimia mia moja kwamba CHASO inapaswa kuimarishwa sana sasa hivi kulingana na mahitaji yalivyo.CDM inahitaji vijana hawa kwenda kugombea udiwani,ubunge na uongozi wa vijiji na mitaa.

Tukitaka ukombozi wa kweli ni lazima tuanze kuwashawishi vijana hawa waanze kugombea nafasi za chini za uongozi na siyo kukimbilia za juu tu.

Asubuhi hii nimesoma taarifa kwenye mtandao wa gazeti la Mwananchi haikunifurahisha sana kwamba wanachama wa CHASO Tawi la chuo kikuu Mbeya-TEKU wanalalamika kwamba tangia Tawi lao lizinduliwe na M/kiti Mbowe mwaka jana hakuna kiongozi yeyote ambaye amewahi hata kuwatembelea na kuwatia moyo.

Viongozi wenyewe wanaolalamikiwa na wa mkoa na wilaya.Sasa hii aibu ni lazima iondoke kwamba kama viongozi wa wilaya na mikoa wanashindwa hata kuwatembelea wanachama wanasubiri mpaka Mbowe na Dr Slaa afanye ziara ni ajabu.Hali hii inapaswa idhibitiwe mara moja.

Mkuu wangu Tuntemeke,pia tukitaka kuwajenga vijana kupitia CHASO ni lazima BAVICHA Taifa na CDM makao makuu pia waandae semina mara kwa mara kwa vijana hawa kuwajenga.

Vijana wanapaswa kufundishwa Skills za Uongozi.Wanapaswa kujua siasa za kushinda na kushindwa.Wanapaswa kuelekezwa maadili ya uongozi yakoje.

Vijana waambiwe wazi ni mwiko kuenguliwa kwenye kugombea nafasi fulani halafu mnaanza makundi ya fitina ya kuwatukana na kuwakashifu viongozi wa chama.Huwa dunia haina siri kijana anayefanya hivyo ni lazima mwishowe ajulikane tu.

Tuntemeke kama ulivyosema bado hii ni changamoto kubwa.Tunajua kazi nyingi walizo nazo viongozi wa Taifa.Lakini walau kazi hii ianze kusimamiwaa na vijana wenyewe.

Jogn Mnyika,John Heche,Ben Saanane na vijana wenzenu wenye maadili ya kweli imarisheni CHASO kwa mageuzi ya kweli katika Taifa.

Mkuu Tuntemeke nasema tena Asante sana.CHASO IMARA NDIYI BAVICHA IMARA NA NDIYO CDM IMARA.
 
Kumlinga john na heche ni kitu usichokiju kabisa. John mnyika ni bora zaidi mara mia moja mbele labda unalinganisha majina yao ya mwanzo nimefanya kazi na hawa watu kwa karibu sana hivyo ninachoongea nakijua ukitaka nikusibitishe ubora wa mnyika na ujinga wa heche.
 
Kumlinga john na heche ni kitu usichokiju kabisa. John mnyika ni bora zaidi mara mia moja mbele labda unalinganisha majina yao ya mwanzo nimefanya kazi na hawa watu kwa karibu sana hivyo ninachoongea nakijua ukitaka nikusibitishe ubora wa mnyika na ujinga wa heche.

Ndugu yangu Rehani.

Hujamwelewa mleta mada.Mleta mada hakuwa na lengo la kuwalinganisha na kuangalia ni nani bora kati yao.Bali mleta mada alitaka watanzania waone kuna kitu fulani kiko ndani ya hawa vijana.Fahamu kila mtu ana kipaji chake alichojaaliwa na Muumba na si lazima vipaji vya watu wote vifanane.
 
Ben saanane ni kada wa membe anawazuga cdm..heche msanii na mropokaji...apo kiongoz ni mnyika basi..
 
Ben saanane ni kada wa membe anawazuga cdm..heche msanii na mropokaji...apo kiongoz ni mnyika basi..

Mkuu Young Tanzanian,

Ingawa wenyewe wanaweza kujibu madai yako lakini niseme kitu kimoja.Jukwaa hili ni la GT.Unapotoa tuhuma nzito kama hizi ni lazima uweke ushahidi usiotiliwa shaka la sivyo tutaita ni yaleyale mambo ya unafiki na ufitini.

Tuonyeshe wazi ni tangu lini Ben ni kada wa Membe? Au ni kwa vile majina yao ya mwanzo yanafanana? Je na mimi nikisema Membe ni kada wa Saanane bila kuleta ushahidi utaafiki? Na je usanii wa Heche uko wapi? Mbona CDM hawaoni huo usanii wake na uropokaji? Kinachoshuhudiwa ni Heche kujikita vijijini kufungua mashina na matawi.Kinachoshuhudiwa ni Heche kuongeza idadi kubwa ya wanachama wa CDM.Kinachoshuhudiwa ni Heche kuwatia ujasiri vijana nchi nzima.Kama haya anayofanya ni uropokaji na usanii basi sifa hizi ni nzuri sana sana.

Tuache majungu na Fitina.
 
Ben saanane ni kada wa membe anawazuga cdm..heche msanii na mropokaji...apo kiongoz ni mnyika basi.......

Young Tanzanian,
Una haki ya kutoa maoni.Lakini huna haki ya kupotosha kiasi hiki

Hebu njoo na uthibitisho wa uliyoandika.

Kama Molemo,Alivyosema hapo juu nadhani unalinganisha ufanano wa majina yetu ya Mwanzo

Membe by professional ana Shahada ya Uzamili katika siasa za kimataifa/uhusiano wa kimataifa na Diplomasia sawa na taaluma yangu.Nimekua nikifuatilia jinsi anavyoitumia taaluma hiyo kwa weledi isipokua yuko in a wrong platform na nimekua nikimpongeza na kumkosoa vikali ninapojua hapa amekosea.Kama hili linanifanya kada wake basi neno kada lina tafsiri nyingi
 
Ben saanane ni kada wa membe anawazuga cdm..heche msanii na mropokaji...apo kiongoz ni mnyika basi......

Young Tanzanian,
Una haki ya kutoa maoni.Lakini huna haki ya kupotosha kiasi hiki

Hebu njoo na uthibitisho wa uliyoandika.

Kama Molemo,Alivyosema hapo juu nadhani unalinganisha ufanano wa majina yetu ya Mwanzo

Membe by professional ana Shahada ya Uzamili katika siasa za kimataifa/uhusiano wa kimataifa na Diplomasia sawa na taaluma yangu.

Nimekua nikifuatilia jinsi anavyoitumia taaluma hiyo kwa weledi isipokua yuko in a wrong platform na nimekua nikimpongeza na kumkosoa vikali ninapojua hapa amekosea.Kama hili linanifanya kada wake basi neno kada lina tafsiri nyingi.
 
WanaJF,
Mara ya mwisho kuzungumzia undani wa wanasiasa ilikuwa mwezi January mwaka huu kwa kuwazungumzia wanasiasa mashuhuri Tanzania Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.Niliahidi nitarudi tena na mada hii hii kuwajadili wanasiasa wengine.Na nitakuwa nikifanya hivyo mara kwa mara nipatapo nafasi bila kubagua wanasiasa kwa itikadi zao.

Leo nitaomba kuwajadili wanasiasa wengine mashuhuri katika anga la Tanzania.Wanasiasa hao ni John Mnyika-Mbunge wa Jimbo la Ubungo na John Heche-Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa.Nimewachanganya Pamoja kwa sababu wanashabihiana kwa mambo mengi lakini lamsingi likiwa Itikadi yao na misimamo yao kuhusu mambo ya msingi.

Mafanikio Misimamo yao:

-Kwanza wote hawa ni vijana na wamekuwa kama Role model kwa vijana wengi si kwa vijana wa CDM tu bali kwa vijana wa Itikadi zote.
-Ni vijana wenye misimamo isiyoyumba na wanakitetea kwa nguvu kile wanachokiamini bila kuogopa vitisho kutoka kwa yeyote.
-Kutokana na Karama za kiuongozi walizo nazo wamefanikiwa kufika nafasi za juu kabisa za uongozi kwa umri wao.John Mnyika mbali ya kuwa mbunge anayeongoza jimbo kubwa kabisa la Ubungo pia yeye ndiye msemaji mkuu wa chama chake cha CDM.John Heche ni kiongozi wa BAVICHA Taifa na mjumbe wa Kamati kuu ya chama chake CDM,chombo cha ngazi ya juu kabisa ndani ya chama chake.
-Vijana hawa wamekuwa wakifanya kazi kubwa ndani ya chama chao hasa kuimarisha chama vijijini na kukipigania chama.Mafanikio yoyote ndani ya CDM huwezi kuwakosa hawa vijana.
-Ni vijana ambao hawaamini katika siasa za makundi.Sikuzote wanaamini katika CDM Imara.Huwezi kuwakuta wakishabikia majina ya watu ndani ya chama chao bali wanashabikia sera na Itikadi ya CDM.
-Ni wanyenyekevu,watiifu na wanapenda kukosolewa.
-Vijana hawa wana heshima kubwa kwa viongozi wao ndani ya Chama na huheshimu siku zote busara za wazee.Lau wakikosoa basi hukosoa kwa staha kubwa.

Changamoto zao:

-John Heche na John Mnyika pamoja na sifa zote zilizotajwa juu bado wanachangamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwafikia vijana wengi zaidi hasa wa vijijini na kuwapa somo la Uraia hususan umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura kwani inaonekana vijana wengi ni wafuasi sugu wa CDM lakini hawajiandikishi wala kupiga kura.
-Kutokana na umaarufu wao wamejitokeza vijana wengine wenye chuki na mafanikio yao na kuwaandama kwa matusi na maneno ya uongo hasa kupitia mitandao ya kijamii.Hata hivyo bado vijana hawa wameonyesha subira kubwa kwa mashambulizi hayo.Hawajakata tamaa bali wanasonga mbele.

Kwa Viongozi wakuu wa CHADEMA.

-Kutokana na yote niliyoandika juu viongozi wakuu wa CDM wanapaswa kuwatia moyo vijana hawa ili wasonge mbele zaidi na wasikatishwe tamaa na maadui wa CDM.
-CDM kama chama wanapaswa kuandaa vijana wasomi wanaofuata nyayo za kina Mnyika na Heche.Hata hivyo nafarijika kuona wapo vijana ndani ya CDM wenye uwezo wa kufuata nyayo hizi.Kwa mfano yupo kijana anayeitwa Ben Saanane,kwa wanaofuatilia siasa zake watagundua kwamba ni kijana anayeonyesha uvumilivu wa hali ya juu.Ben Saanane amewahi kupata misukosuko ya kisiasa lakini alisimama imara kutetea anchoamini.Hakuwahi kukashifu viongozi wake wa chama katika uficho au kwa uwazi.Ben anaamini CDM kama taasisi imara na siyo makundi ya watu.Ninaweza kusema Ben Saanane ni matunda ya kazi nzuri za kina Mnyika na wenzake.Hata hivyo chama kiandae vijana wengi zaidi wa kufuata nyayo za kina Mnyika na Heche na siyo Ben Saanane tu...

WanaJF Karibuni kwa mjadala!

Kumbe huo ndo undani wao? Duh!! inabidi utuambie ulitumia nyenzo gani kufanya utafiti kama huu unaoonyesha umahiri wa mnyika na henche hasa wakiwa ni wapiga POROJO wakuu wa chadema. Ujasiri na umahiri wa mtu si kelele na maneno mengi bali ni utendaji wao wa kazi za kuwaletea wananchi maendeleo. Njoo na hoja za msingi utuambie hadi sasa mnyika amewatetea na kuwasaidia vipi wananchi wake wa jimbo la Ubungo? Bado hatujaona mafanikio yao, inabidi warudi tena kwenye kile cha cha kikristo cha ujerumani (CDU) wakajifunze tena namna nzuri ya kuwabatiza watanzania.
 
Toka kwa mara ya kwanza nimemuona kamanda heche akigombea udiwani kata ya tarime mjini nilitegemea kuona matunda yake kwa taifa letu,alimpigania charles nyanguru aliyekisaliti chama na kumuwezesha kuwa mbunge,heche ni kamanda wa makamanda hana hoja wala agenda tofauti na kuleta mabadiliko kwa watanzania,hakika Heche ni jembe sana tena sana,i wish kama vijana tungeungana wote bila itikadi zetu kuwatambua vijana wanaotambua kazi na majukumu yao kwa taifa letu mgando.
 
Hawa ni VICHWA na ni MAJEMBE huwezi kuwalinganisha na hao wa upande mwingine
 
kuwa na masters ni jambo moja na kuweza kufiri na kutenda ni jambo jingine
 
Back
Top Bottom