Bila shaka mkuu wangu, bila kukusau wewe ni jembe na ndio maana nikapendekeza sana jina lako wewe ktk uongozi maana unaonyesha nia njema sana ktk ujenzi hapa JF..Kila siku unapoandika hoja ni Positive, mawazo yanayojenga badala ya kubomoa..nakutakia kila la kheri nategemea sana tutakuja kutana siku moja tubadilishane mawazo.Hivi inamsaidia nini mtu kila siku kumtaja mwenzake kwa kuzungumzia mambo yake binafsi?
Mambo binafsi ya mtu, mathalani John Mnyika ama Ben Saanane yana athari gani chanya ama hasi kwa ustawi wa Chadema?
Wasiwasi wangu ni kwamba Ben ameonyesha kupiga hatua kubwa sana kisiasa sasa kuna watu wanamuonea wivu na wanadhani njia ya kumkwamisha ni kuanza kuzungumzia mambo yake binafsi.
Mwanzoni kulikuwa na fununu mitaani kwamba vijana wote waliogombea Bavicha na kuenguliwa wameunda alliance ya kuushambulia uongozi wa Bavicha na Chadema kwa ujumla.
Kwakuwa Ben naye alienguliwa akatajwa kuwemo katika huo ushirika haramu. Kadri siku zinavyokwenda ukweli umebainika kwamba Ben hayuko nao bali amefocus kukijenga chama na si kujenga watu binafsi. Naona hii ndiyo inamletea shida kidogo lakini naona ameshaishinda hiyo vita kwani mwenye macho haambiwi tazama.
Mkuu Mwita Maranya
Kuna maandiko fulani yanasema acha magugu na ngano vikue pamoja shambani na wakati wa mavuno magugu yatatengwa mbali na ngano.Na kazi itakuwa moja tu kuyakusanya magugu na kuyachoma moto huku ngano ikiwekwa ghalani.Na ndivyo sasa inavyoonekana.Tayari magugu yanaonekana na ngano imeonekana.Tunasubiri tu siku ya mavuno.
Endelea kupigania chama chako Kamanda Ben.
hivi Greyson Nyakarungu na Habib Mchange wanavyomtukana Heche na Slaa tanuruni ni Sawa au ni wanachama wa CHAMA gani?
Jamani nitakuwa tofauti kidogo hapa juu ya Ben Saanane.Natambua kuwa ni Kamanda na ni hazina ya Taifa, lakini mpaka leo sijajua ni kwanini alienguliwa katika ushindani BAVICHA?Hivi alliance yake na Nyakarungu/Mwampamba ndiyo ilimtoa ama RUSHWA?
Najua CDM ni chama makini na mpaka kufikia vijana hawa kuwekwa pembeni ni lazima uchunguzi wa kina ulifanyika na kamati kujiridhisha kuwa vijana hawa HAWAFAI.Kama hii ndivyo ilivyo, ubora ama usafi wa Ben uko wapi?Je! Amewahi kukiri na kutubu? Ama ndo hivyo ukishasoma mchezo, unaingia dimbani kucheza kama mchezo utakavyo.
Ben naomba majibu juu ya hayo.Niko tayari kukosolewa kwa yote.
Bila shaka mkuu wangu, bila kukusau wewe ni jembe na ndio maana nikapendekeza sana jina lako wewe ktk uongozi maana unaonyesha nia njema sana ktk ujenzi hapa JF..Kila siku unapoandika hoja ni Positive, mawazo yanayojenga badala ya kubomoa..nakutakia kila la kheri nategemea sana tutakuja kutana siku moja tubadilishane mawazo.
naamini hakuandika kwa nia mbaya, kuna wakati RitzMkuu Ritz kwa mara ya kwanza nikubaliane na wewe.Hata kama umeandika kwa nia mbaya itakuwa ni shauri yako.
safi sana. Hongera zao.wanajf,
mara ya mwisho kuzungumzia undani wa wanasiasa ilikuwa mwezi january mwaka huu kwa kuwazungumzia wanasiasa mashuhuri tanzania freeman mbowe na dr wilbroad slaa.niliahidi nitarudi tena na mada hii hii kuwajadili wanasiasa wengine.na nitakuwa nikifanya hivyo mara kwa mara nipatapo nafasi bila kubagua wanasiasa kwa itikadi zao.
Leo nitaomba kuwajadili wanasiasa wengine mashuhuri katika anga la tanzania.wanasiasa hao ni john mnyika-mbunge wa jimbo la ubungo na john heche-mwenyekiti wa bavicha taifa.nimewachanganya pamoja kwa sababu wanashabihiana kwa mambo mengi lakini lamsingi likiwa itikadi yao na misimamo yao kuhusu mambo ya msingi.
Mafanikio misimamo yao:
-kwanza wote hawa ni vijana na wamekuwa kama role model kwa vijana wengi si kwa vijana wa cdm tu bali kwa vijana wa itikadi zote.
-ni vijana wenye misimamo isiyoyumba na wanakitetea kwa nguvu kile wanachokiamini bila kuogopa vitisho kutoka kwa yeyote.
-kutokana na karama za kiuongozi walizo nazo wamefanikiwa kufika nafasi za juu kabisa za uongozi kwa umri wao.john mnyika mbali ya kuwa mbunge anayeongoza jimbo kubwa kabisa la ubungo pia yeye ndiye msemaji mkuu wa chama chake cha cdm.john heche ni kiongozi wa bavicha taifa na mjumbe wa kamati kuu ya chama chake cdm,chombo cha ngazi ya juu kabisa ndani ya chama chake.
-vijana hawa wamekuwa wakifanya kazi kubwa ndani ya chama chao hasa kuimarisha chama vijijini na kukipigania chama.mafanikio yoyote ndani ya cdm huwezi kuwakosa hawa vijana.
-ni vijana ambao hawaamini katika siasa za makundi.sikuzote wanaamini katika cdm imara.huwezi kuwakuta wakishabikia majina ya watu ndani ya chama chao bali wanashabikia sera na itikadi ya cdm.
-ni wanyenyekevu,watiifu na wanapenda kukosolewa.
-vijana hawa wana heshima kubwa kwa viongozi wao ndani ya chama na huheshimu siku zote busara za wazee.lau wakikosoa basi hukosoa kwa staha kubwa.
Changamoto zao:
-john heche na john mnyika pamoja na sifa zote zilizotajwa juu bado wanachangamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwafikia vijana wengi zaidi hasa wa vijijini na kuwapa somo la uraia hususan umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura kwani inaonekana vijana wengi ni wafuasi sugu wa cdm lakini hawajiandikishi wala kupiga kura.
-kutokana na umaarufu wao wamejitokeza vijana wengine wenye chuki na mafanikio yao na kuwaandama kwa matusi na maneno ya uongo hasa kupitia mitandao ya kijamii.hata hivyo bado vijana hawa wameonyesha subira kubwa kwa mashambulizi hayo.hawajakata tamaa bali wanasonga mbele.
Kwa viongozi wakuu wa chadema.
-kutokana na yote niliyoandika juu viongozi wakuu wa cdm wanapaswa kuwatia moyo vijana hawa ili wasonge mbele zaidi na wasikatishwe tamaa na maadui wa cdm.
-cdm kama chama wanapaswa kuandaa vijana wasomi wanaofuata nyayo za kina mnyika na heche.hata hivyo nafarijika kuona wapo vijana ndani ya cdm wenye uwezo wa kufuata nyayo hizi.kwa mfano yupo kijana anayeitwa ben saanane,kwa wanaofuatilia siasa zake watagundua kwamba ni kijana anayeonyesha uvumilivu wa hali ya juu.ben saanane amewahi kupata misukosuko ya kisiasa lakini alisimama imara kutetea anchoamini.hakuwahi kukashifu viongozi wake wa chama katika uficho au kwa uwazi.ben anaamini cdm kama taasisi imara na siyo makundi ya watu.ninaweza kusema ben saanane ni matunda ya kazi nzuri za kina mnyika na wenzake.hata hivyo chama kiandae vijana wengi zaidi wa kufuata nyayo za kina mnyika na heche na siyo ben saanane tu...
Wanajf karibuni kwa mjadala!
Bila shaka tukijaaliwa.Nakushukuru sana Kaka mkuu kwa comment yako. Utakumbuka niliwahi kukuandikia mahali fulani kwamba wewe ni mmoja kati ya wakongwe wachache ninaowaheshimu sana hapa JF.
Ninazisoma sana comments zako hapa JF.
Nadhani utakumbuka jana nilistuka kidogo kwa comment yako kule kwenye thread ya Mchange kumpigia debe Zitto.
Mkuu nitafarijika sana kukutana nawe tubadilishane mawazo, nakumbuka uliniambia makazi yako hapa nyumbani yako Ukonga ambapo ndio uwanja wangu wa nyumbani.
Ben Saanane,
Kwa kweli ana sifa za kuwa kiongozi namkubali sana kuna kipindi cha miaka ya nyuma alikuwa anatukanwa sana humu JF watu wanabandika picha zake na za wadada wanamdhalilisha lakini mwenyewe alikuwa anajibu kwa hoja bila kashfa wala kejeli...Jamaa anatisha.
Hakika nikiwaondoa hawa walotajwa hapo juu, ktk vijana wa Chadema wanaonitia moyo na wanaoandika vitu vya maana hapa JF ni Ben Saanane, huyu ananipa hamu, nguvu na matumaini makubwa juu ya vijana wetu.
Mkuu Ritz.
Nimeupenda sana mchango wako kuhusu Ben ambao kwa hakika umeonyesha jinsi binadamu tulivyo pendelewa kwa kujaliwa utashi wa kung'amua na mwenyezi mungu.
Kila jema na lenye kheri lisikuponyoke ustadhi wangu. Mwenyezi Mungu azidi kukujalia hekima na busara na jicho ang'avu linalo uona ukweli.
JIBRIL,
Asante sana.Ni kweli vijana wengi wanapenda kutuona tukishirikiana zaidi
Uchaguzi ulifanyika ukapita.Tunachostahili ni kujenga Baraza na chama kwa kila namna
Mnyika tunashirikiana kwa karibu na mambo mengi huwa ananishauri.Tumekua marafiki tangu nikiwa masomoni na nilikua nikiwasiliana nae kwa karibu tangu kipindi hicho.Hata niliporudi,nilikua nimepanga kwenda jimboni lakini nikawa nimechelewa.Tulishirikiana sana kuhusu jimbo la Ubungo na nilijifunza mengi kutoka kwake kama rafiki na kiongozi wangu ndani ya Chama
Kuna makosa kadhaa ya kisiasa nilishafanya kama mwanadamu na kama mwanasiasa yeyote lakini mara zote alinishauri na kunipa Moyo
Jibril,Umezungumzia suala la kwenda vijijini.Hili ni sahihi kabisa.Tuna programme ya M4C kwa sasa na ratiba itakapokua imekaa sawa ndani ya chama soon tutakua vijijini tena.
Kuhusu suala la alliance,hili limekua darasa kwangu na kama mwanasiasa kijana limenikomaza.Naomba niseme kama ni political testing ni bora uanze kuizoea mapema kabla hujachukua majukumu nyeti zaidi.Ipo siku nitatoa ufafanuzi wa kina
Again,Asanteni JF kwa kunikosoa na kunishauri.Nakaribia mwaka wa 7 sasa nakula Nondo za JF.Asanteni kwa kunijenga
Mohamedi Mtoi,
Mungu atujalie sote tuwe na busara na heri tele.
kaka sasa unaweza sema uko tayari kabisa kumuunga heche mkono katika vita aliyonayo ya kupambana na CCM na kweli utaacha vile vya vikao vya pale (kapuni) ambavyo agenda kuu huwa ni kumdhoofisha huyu bwana mdogo wa chama cgenu kupitia vijana HECHE kwa kweli sisi humu asilimia 100 hatupendezwi na siasa za uvunguni anazofanya mwenzako,nyakarungu, mwampamba, mchange, unasemaje kuhusu mienendo hii na swali langu la utayari wako naomba nipate jibu maana tunapenda kuwaona field na HEche sio humu mitandaoni kwa majina mbalimbalifmpiganaji,
Shukrani sana post yako.Kwa kweli inatia moyo sana sana.
Ni kweli tumekua na changamoto za hapa na pale lakini kadiri siku zinavyosonga mbele Vijana ndani ya CHADEMA tunazidi kuimarika
Ni kweli vijana wengi ambao ni wafuasi wa CHADEMA wanafurahi kutuona tukisimama kwa umoja kumuelekezea silaha zetu (Hoja/Fikra Mbadala) adui yetu(Mpinzani) ambaye ni CCM na mfumo adui kwa ustawi wa kundi la vijana na Taifa kwa ujumla
Tunaweza tusikubaliane mambo kadhaa kama ilivyo kawaida kwa taasisi yoyote yenye watu wengi wenye uwezo katika mazingira ya kidemokrasia bila kuathiri malengo ya pamoja na uwajibikaji.
Kama tunakipenda chama ni lazima tukilinde.Hakuna mtu anayestahili kukilinda chama hiki kama si mimi,wewe na wengine
Naamini BAVICHA imara ndiyo itakayobeba na kushawashi ajenda bora kwa vijana Tanzania.Kazi inaendelea kufanyika
Kukosoana ni lazima kuwe na tija na mara nyingi nomekua nikisizitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiama kuhakikisha fan base tuliyo nayo inapiga kura.Mikakati mingine sitaitaja hapa ila tutashirikiana na baraza la vijana kwa karibu zaidi
Ukiona Ben Saanane anapiga hatua kubwa kiasi hiki ujue familia yangu ya Jamii Forums imechangia kwa kiasi kikubwa,wale wanaoniunga mkono,wanaonikosoa na wale wanaotoa kebehi.
mkuu unaelekekea kujibu hoja zangu kaza buti mambo si mabayaApolycaprito,
Sikuenguliwa BAVICHA kwa tuhuma za Rushwa.
Nilishawahi kutoa ufafanuzi hapa JF siku moja baada ya Uchaguzi ule yaani Tarehe 29.05.2011.
Nilieleza juu ya tuhuma za kuunda alliance ambayo kamati ya wazee iliona technically si fair katika uchaguzi ule.Ni kweli niliunda alliance.Mchakato wa uchaguzi una kanuni zake.Na ili Demokrasia ishamiri ni lazima kanuni hizo zifuatwe.Nilijifunza zaidi kupitia nafasi ile na baada ya hapo niliahidi nitashirikiana kukijenga chama changu.BAVICHA ni kubwa kuliko sisi sote