Undani wa John Mnyika na John Heche

Undani wa John Mnyika na John Heche

hawezi kupambana na combination ya mboni mhita na sadifa wa Uvccm.Kama ni shule hata sadifa ana masters na wakili Anthoni Mavunde mjumbe wa baraza UVCCM anayo
Ana kazi sana kuongoza bavicha mwakani mbele ya hawa wadomi wa Uvccm.Kwa bahati nzuri mamluki wake paul makonda na akina felician tuliwadhibiti uvccm .hataweza dogo huyo
Mkuu naona bado uko usingizini.

Unawezaje kuilinganisha BAVICHA na UVCCM?

Uwezo wa kamanda Heche ni mkubwa sana kufanya harakati za siasa kuliko mtu yoyote ndani ya CCM.

Kifupi UVCCM ilishakufa tangu mwaka 2007 kwenye uchaguzi wao wa ndani, huu uchaguzi wa juzi juzi ndani ya UVCCM ilikuwa ndio mazishi rasmi.

Yote kwa yote tutapima uwezo wao kwenye marudio ya uchaguzi wa Sumbawanga mjini.
 
Mkuu Ritz kwa mara ya kwanza nikubaliane na wewe.Hata kama umeandika kwa nia mbaya itakuwa ni shauri yako.

Tatizo lenu lenu ndio hilo niandike kwa nia mbaya ili iweje bahati nzuri mie sifichi kitu mtu yoyote namchana tu...Ben ni mtu makini kwangu sija haja ya wewe kukubali wala kukataa.
 
CHADEMA hujiendesha kwa ruzuku toka serikalini, ada na viingilio vya wanachama pamoja na michango mbalimbali ya wapenzi. hivyo Sabodo hata kama yeye CCM ni mpenzi wa CHADEMA kutumia pesa aliyotoa ktk kampen ni sahihi kikatiba. Makeo ni siri yetu
 
Hivi inamsaidia nini mtu kila siku kumtaja mwenzake kwa kuzungumzia mambo yake binafsi?
Mambo binafsi ya mtu, mathalani John Mnyika ama Ben Saanane yana athari gani chanya ama hasi kwa ustawi wa Chadema?
Wasiwasi wangu ni kwamba Ben ameonyesha kupiga hatua kubwa sana kisiasa sasa kuna watu wanamuonea wivu na wanadhani njia ya kumkwamisha ni kuanza kuzungumzia mambo yake binafsi.
Mwanzoni kulikuwa na fununu mitaani kwamba vijana wote waliogombea Bavicha na kuenguliwa wameunda alliance ya kuushambulia uongozi wa Bavicha na Chadema kwa ujumla.
Kwakuwa Ben naye alienguliwa akatajwa kuwemo katika huo ushirika haramu. Kadri siku zinavyokwenda ukweli umebainika kwamba Ben hayuko nao bali amefocus kukijenga chama na si kujenga watu binafsi. Naona hii ndiyo inamletea shida kidogo lakini naona ameshaishinda hiyo vita kwani mwenye macho haambiwi tazama.

Mkuu Mwita,thankyou Comrade.Ume-Add value kubwa sana kwenye mada yangu.Mwita vijana wengine wa CDM wanapaswa kufuata mfano wako jinsi unavyojadili mada zako hapa JF kwa hekima kubwa.Ninazidi kuziona hazina za kina Mnyika.
 
Last edited by a moderator:
inaonekana kuna watu hawafurahii maendeleo ya chama na hasa wao wanapokuwa mchango wao haujaonekana.mkuu umechambua vizuri na huo ndo ukweli wenyewe.na hawa wanaotawaliwa na fikra za udini,ukabila n.k ni akina nani hasa?je ni kwanini mtu mmoja anaachwa achezee chama atakavyo?mimi siamini kama kuna mwanachama ama kiongozi mwenye hati miliki ya chama.lazima wote tuwe na nia ya pamoja,malengo ya pamoja,falsafa moja,itikadi moja ktk chama.mh.mnyika na ndg.heche are the best in demostration,kwanini wengine wanajipa uhalali wa kuleta chuki pasi ya sababu je ndiyo njia ya kuyapata madaraka?

Thankyou Mgaya.Nimefurahi Mods wamefuta post za watu ambao tayari walishajipanga kuchafua hii mada.Ukiona mtu anajadili Udini na Ukabila leo ni wa kuhurumiwa tu.
 
Kweli kabisa mkuu vichwa vyao ni vya kufugia nywele, Hawa vijana nawashangaa sana mda wote wanajifikilia kutukana ukitaka kuwajua waangalie hata tanuruni utawajua ndo wenyewe

Anyway tusonge mbela achana nao nawe upo Juu sana hata mapendekezo uliyoyatoa kwa Heche kumrithi Zitto Unaibu ni kutokana na uwezo mkubwa alionao na ni analysis nzuri kama ya Fmpiganaji
 
Mnyika

Ni kijana mwenye akili nyingi sana na kama kweli wako na Ben saanane sambamba basi ni hatua nzuri kwa kuwa Ben na Mnyika ni wanasiasa vijana wenye uwezo wa kujenga hoja na wakaeleweka ingawa kidogo Ben naona anafanya siasa za hatari hasa kuunda alliance na watu ambao wana historia mbaya kwenye chama.Huwa anajiamini kupita kiasi

Halikadhalika John Mnyika atamkomaza zaidi Ben huko tuendako na kama watafanya kazi karibu wataongeza ngivu katika safu ya vijana

Mnyika ameweza kuongeza haiba ya vijana

JOHN HECHE

Ni kiongozi mzuri.Nilihofia kama aliweza kuvumilia mikimiki ya vurugu za alliance ya akina Ben Saanane na lile kundi na hasa mkakati wa kumpiga vita na kumpindua
Ameweza kwenda vijijini
Naona ni jambo la kumshukuru Mungu kama hawa wameweza kukaa pamoja
Sasa naona hata vita ya Heche na makamu wake shonza itakosa nguvu.Ukimwondoa ben hapo akina mchange hawatakua na nguvu

Ben Saanane
Kosa lake kubwa ni kutulia.Bado anastahili kwenda sana vijijini.Hata ukiongea nae ana kwa ana utavutiwa nae
Pia haya maswala yake na wasichana wanatakiwa waache mara moja na hata Mnyika.Wanasiasa wakubwa na Bright wamejumiwa mara nyingi na kupenda kwao watoto.Vinginevyo hizi colabo hapa zimetulia mno.Nitafurahi siku moja nikiwaona heche,ben na Mnyika jukwaani au wakienda vijijini pamoja

Mkuu Jibril Asante kwa kukoleza hii mada.Ninaamini CDM imara itajengwa na vijana wenye nia njema kama hawa watatu juu.Hivi mtu anayeshindwa hata kuheshimu viongozi wake wenye umri sawa na baba yake utasema ana akili kweli?
 
si ni ukweli lakini?mtu amefanya utafiti ili ashabikie kitu cha kweli.naunga mkono huu utafiti

Mkuu Lamusumo nakushukuru sana kuunga mkono hoja hii.Kamwe katika tafiti zangu sipendelei mtu na ninaakisi kile nilichokipata.Watu wengine wanaamini katika kujipendekeza kitu ambacho hakiwezi kutoa tathmini sahihi.
 
Ben Saanane,
Kwa kweli ana sifa za kuwa kiongozi namkubali sana kuna kipindi cha miaka ya nyuma alikuwa anatukanwa sana humu JF watu wanabandika picha zake na za wadada wanamdhalilisha lakini mwenyewe alikuwa anajibu kwa hoja bila kashfa wala kejeli...Jamaa anatisha.

Mkubwa Ritz ninaamini kwamba umetendea haki Jukwaa.Asante sana.
 
Last edited by a moderator:
Mnyika

Ni kijana mwenye akili nyingi sana na kama kweli wako na Ben saanane sambamba basi ni hatua nzuri kwa kuwa Ben na Mnyika ni wanasiasa vijana wenye uwezo wa kujenga hoja na wakaeleweka ingawa kidogo Ben naona anafanya siasa za hatari hasa kuunda alliance na watu ambao wana historia mbaya kwenye chama.Huwa anajiamini kupita kiasi

Halikadhalika John Mnyika atamkomaza zaidi Ben huko tuendako na kama watafanya kazi karibu wataongeza ngivu katika safu ya vijana

Mnyika ameweza kuongeza haiba ya vijana

JOHN HECHE

Ni kiongozi mzuri.Nilihofia kama aliweza kuvumilia mikimiki ya vurugu za alliance ya akina Ben Saanane na lile kundi na hasa mkakati wa kumpiga vita na kumpindua
Ameweza kwenda vijijini
Naona ni jambo la kumshukuru Mungu kama hawa wameweza kukaa pamoja
Sasa naona hata vita ya Heche na makamu wake shonza itakosa nguvu.Ukimwondoa ben hapo akina mchange hawatakua na nguvu

Ben Saanane
Kosa lake kubwa ni kutulia.Bado anastahili kwenda sana vijijini.Hata ukiongea nae ana kwa ana utavutiwa nae
Pia haya maswala yake na wasichana wanatakiwa waache mara moja na hata Mnyika.Wanasiasa wakubwa na Bright wamejumiwa mara nyingi na kupenda kwao watoto.Vinginevyo hizi colabo hapa zimetulia mno.Nitafurahi siku moja nikiwaona heche,ben na Mnyika jukwaani au wakienda vijijini pamoja


JIBRIL,
Asante sana.Ni kweli vijana wengi wanapenda kutuona tukishirikiana zaidi

Uchaguzi ulifanyika ukapita.Tunachostahili ni kujenga Baraza na chama kwa kila namna

Mnyika tunashirikiana kwa karibu na mambo mengi huwa ananishauri.Tumekua marafiki tangu nikiwa masomoni na nilikua nikiwasiliana nae kwa karibu tangu kipindi hicho.Hata niliporudi,nilikua nimepanga kwenda jimboni lakini nikawa nimechelewa.Tulishirikiana sana kuhusu jimbo la Ubungo na nilijifunza mengi kutoka kwake kama rafiki na kiongozi wangu ndani ya Chama


Kuna makosa kadhaa ya kisiasa nilishafanya kama mwanadamu na kama mwanasiasa yeyote lakini mara zote alinishauri na kunipa Moyo


Jibril,Umezungumzia suala la kwenda vijijini.Hili ni sahihi kabisa.Tuna programme ya M4C kwa sasa na ratiba itakapokua imekaa sawa ndani ya chama soon tutakua vijijini tena.

Kuhusu suala la alliance,hili limekua darasa kwangu na kama mwanasiasa kijana limenikomaza.Naomba niseme kama ni political testing ni bora uanze kuizoea mapema kabla hujachukua majukumu nyeti zaidi.Ipo siku nitatoa ufafanuzi wa kina

Again,Asanteni JF kwa kunikosoa na kunishauri.Nakaribia mwaka wa 7 sasa nakula Nondo za JF.Asanteni kwa kunijenga
 
  • Thanks
Reactions: awp
fmpiganaji,

Shukrani sana post yako.Kwa kweli inatia moyo sana sana.

Ni kweli tumekua na changamoto za hapa na pale lakini kadiri siku zinavyosonga mbele Vijana ndani ya CHADEMA tunazidi kuimarika

Ni kweli vijana wengi ambao ni wafuasi wa CHADEMA wanafurahi kutuona tukisimama kwa umoja kumuelekezea silaha zetu (Hoja/Fikra Mbadala) adui yetu(Mpinzani) ambaye ni CCM na mfumo adui kwa ustawi wa kundi la vijana na Taifa kwa ujumla

Tunaweza tusikubaliane mambo kadhaa kama ilivyo kawaida kwa taasisi yoyote yenye watu wengi wenye uwezo katika mazingira ya kidemokrasia bila kuathiri malengo ya pamoja na uwajibikaji.

Kama tunakipenda chama ni lazima tukilinde.Hakuna mtu anayestahili kukilinda chama hiki kama si mimi,wewe na wengine

Naamini BAVICHA imara ndiyo itakayobeba na kushawashi ajenda bora kwa vijana Tanzania.Kazi inaendelea kufanyika

Kukosoana ni lazima kuwe na tija na mara nyingi nomekua nikisizitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiama kuhakikisha fan base tuliyo nayo inapiga kura.Mikakati mingine sitaitaja hapa ila tutashirikiana na baraza la vijana kwa karibu zaidi

Ukiona Ben Saanane anapiga hatua kubwa kiasi hiki ujue familia yangu ya Jamii Forums imechangia kwa kiasi kikubwa,wale wanaoniunga mkono,wanaonikosoa na wale wanaotoa kebehi.

Ben
Nashukuru umeiona Post yangu na umekuja kutoa mchango wako.Nimefurahi pia kuthamini malezi ya Jukwaa letu la JF.
Ninachokushauri endelea kujenga chama chako bila kutazama watu wanaongea nini.Endelea kushauri viongozi wako wakuu wa chama katika namna bora ya kuimarisha chama.Wagongee hata usiku wape mawazo yako.Ninaamini kina Dr.Slaa na Mbowe ni wasikivu na wanashaurika alimradi washauriwe kwa hekima na busara.
Pia kama wadau wengine walivyosema hakikisheni mnaenda zaidi vijijini.Nimesikia katika uchaguzi wa Vijiji leo USA River CDM imeshinda mitaa 6 na CCM imepata 3.Na CDM itaongoza halmashauri ya mji mdogo wa USA.Sasa mimi nataka mchukulie huu kama mfano mkajikite zaidi vijijini.

Kila la kheri!
 
Ben Saanane,
Kwa kweli ana sifa za kuwa kiongozi namkubali sana kuna kipindi cha miaka ya nyuma alikuwa anatukanwa sana humu JF watu wanabandika picha zake na za wadada wanamdhalilisha lakini mwenyewe alikuwa anajibu kwa hoja bila kashfa wala kejeli...Jamaa anatisha.

Mkuu Ritz,

Shukrani sana.Changamoto zako hasa kwa post zangu zimekuwa zikiniimarisha zaidi.JF haiwezi kuwa kisima cha fikra bila kupingana.

Asante sana Kaka
 
Last edited by a moderator:
Huu ni mshangao wa Mwaka.unamkubali kada wa chadema?
Ritz unamkubali ben aliyeshabikiwa na molemo tena?mbona molemo hapendi ushabikie watu huko chadema kama zitto na wengine?

Mkuu tuachane na kuweka mipaka kwenye mijadala hapa JF.Ritz asihukumiwe kwa kusema ya moyoni mwake.
 
Ritz
Mkuu naona umeanza kupona
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana Mkuu kwa Analysis nzuri

Hawa vijana ni makini sana katika kazi zao na Heche kwa cku za karibuni ameenda vijijini zaidi ili kuwafikia vijana wengi sana kuwaelimisha na nakumbuka mawazo yako yanafanana sana na Melemo kwani alishawahi kuona uwezo wa HECHE na hata kutoa pendekezo la kumrithi Zitto Unaibu

Thankyou Comrade igwa.Nashukuru kwa kuongeza nyama kwenye mada yangu.
 
Jamani nitakuwa tofauti kidogo hapa juu ya Ben Saanane.Natambua kuwa ni Kamanda na ni hazina ya Taifa, lakini mpaka leo sijajua ni kwanini alienguliwa katika ushindani BAVICHA?Hivi alliance yake na Nyakarungu/Mwampamba ndiyo ilimtoa ama RUSHWA?

Najua CDM ni chama makini na mpaka kufikia vijana hawa kuwekwa pembeni ni lazima uchunguzi wa kina ulifanyika na kamati kujiridhisha kuwa vijana hawa HAWAFAI.Kama hii ndivyo ilivyo, ubora ama usafi wa Ben uko wapi?Je! Amewahi kukiri na kutubu? Ama ndo hivyo ukishasoma mchezo, unaingia dimbani kucheza kama mchezo utakavyo.

Ben naomba majibu juu ya hayo.Niko tayari kukosolewa kwa yote.
 
WanaJF,
Mara ya mwisho kuzungumzia undani wa wanasiasa ilikuwa mwezi January mwaka huu kwa kuwazungumzia wanasiasa mashuhuri Tanzania Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.Niliahidi nitarudi tena na mada hii hii kuwajadili wanasiasa wengine.Na nitakuwa nikifanya hivyo mara kwa mara nipatapo nafasi bila kubagua wanasiasa kwa itikadi zao.

Leo nitaomba kuwajadili wanasiasa wengine mashuhuri katika anga la Tanzania.Wanasiasa hao ni John Mnyika-Mbunge wa Jimbo la Ubungo na John Heche-Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa.Nimewachanganya Pamoja kwa sababu wanashabihiana kwa mambo mengi lakini lamsingi likiwa Itikadi yao na misimamo yao kuhusu mambo ya msingi.

Mafanikio Misimamo yao:

-Kwanza wote hawa ni vijana na wamekuwa kama Role model kwa vijana wengi si kwa vijana wa CDM tu bali kwa vijana wa Itikadi zote.
-Ni vijana wenye misimamo isiyoyumba na wanakitetea kwa nguvu kile wanachokiamini bila kuogopa vitisho kutoka kwa yeyote.
-Kutokana na Karama za kiuongozi walizo nazo wamefanikiwa kufika nafasi za juu kabisa za uongozi kwa umri wao.John Mnyika mbali ya kuwa mbunge anayeongoza jimbo kubwa kabisa la Ubungo pia yeye ndiye msemaji mkuu wa chama chake cha CDM.John Heche ni kiongozi wa BAVICHA Taifa na mjumbe wa Kamati kuu ya chama chake CDM,chombo cha ngazi ya juu kabisa ndani ya chama chake.
-Vijana hawa wamekuwa wakifanya kazi kubwa ndani ya chama chao hasa kuimarisha chama vijijini na kukipigania chama.Mafanikio yoyote ndani ya CDM huwezi kuwakosa hawa vijana.
-Ni vijana ambao hawaamini katika siasa za makundi.Sikuzote wanaamini katika CDM Imara.Huwezi kuwakuta wakishabikia majina ya watu ndani ya chama chao bali wanashabikia sera na Itikadi ya CDM.
-Ni wanyenyekevu,watiifu na wanapenda kukosolewa.
-Vijana hawa wana heshima kubwa kwa viongozi wao ndani ya Chama na huheshimu siku zote busara za wazee.Lau wakikosoa basi hukosoa kwa staha kubwa.

Changamoto zao:

-John Heche na John Mnyika pamoja na sifa zote zilizotajwa juu bado wanachangamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwafikia vijana wengi zaidi hasa wa vijijini na kuwapa somo la Uraia hususan umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura kwani inaonekana vijana wengi ni wafuasi sugu wa CDM lakini hawajiandikishi wala kupiga kura.
-Kutokana na umaarufu wao wamejitokeza vijana wengine wenye chuki na mafanikio yao na kuwaandama kwa matusi na maneno ya uongo hasa kupitia mitandao ya kijamii.Hata hivyo bado vijana hawa wameonyesha subira kubwa kwa mashambulizi hayo.Hawajakata tamaa bali wanasonga mbele.

Kwa Viongozi wakuu wa CHADEMA.

-Kutokana na yote niliyoandika juu viongozi wakuu wa CDM wanapaswa kuwatia moyo vijana hawa ili wasonge mbele zaidi na wasikatishwe tamaa na maadui wa CDM.
-CDM kama chama wanapaswa kuandaa vijana wasomi wanaofuata nyayo za kina Mnyika na Heche.Hata hivyo nafarijika kuona wapo vijana ndani ya CDM wenye uwezo wa kufuata nyayo hizi.Kwa mfano yupo kijana anayeitwa Ben Saanane,kwa wanaofuatilia siasa zake watagundua kwamba ni kijana anayeonyesha uvumilivu wa hali ya juu.Ben Saanane amewahi kupata misukosuko ya kisiasa lakini alisimama imara kutetea anchoamini.Hakuwahi kukashifu viongozi wake wa chama katika uficho au kwa uwazi.Ben anaamini CDM kama taasisi imara na siyo makundi ya watu.Ninaweza kusema Ben Saanane ni matunda ya kazi nzuri za kina Mnyika na wenzake.Hata hivyo chama kiandae vijana wengi zaidi wa kufuata nyayo za kina Mnyika na Heche na siyo Ben Saanane tu...

WanaJF Karibuni kwa mjadala!


Kuhusu John Mnyika siwezi kupingana na wewe mtoa mada hata kidogo,ila nina tatizo na mashaka kwa bwana John Heche kwani nimeanza kumfahamu na kuwa nae karibu toka mwaka 2006 - 2009 tukiwa chuo cha mtakatifu Augustino Mwanza na ntapingana na wewe kutokana na sababu zifuatazo:-

1.Uwezo wake wa kufikiri. Natilia shaka sana credit ulizompa John Heche kwa sababu alipokua mwaka wa kwanza katika chuo cha Mtakatifu Augustino counter book yake kwa juu alikua kaandika Pum...u University.

2.Ni msaliti na hana msimamo. Mwaka 2008 kulikua na Uchaguzi wa kumchagua Rais wa serikali ya wanafunzi SAUT,na bwana John Heche aliamua kumgeuka Mgombea aliyekua anasoma nae darasa moja Education na kuamua kumsupport mgombea aliyekua aliyekua anasoma Sociology,hii ilisababisha members wa darasa lake kumuijia juu na hivyo ikamfanya abdilishe uamzi wake na swala hili hadi leo liliteta uhasama kati yake na Bwana Mnyeti ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Misungwi (Mawe matatu).Pili alisaliti wenzake katika harakati za kuanzisha mgomo kwa watu wa Education mwaka 2008 pale walipoamua kwenda katika ofisi ya Makam mkuu wa chuo yeye kama mhamasishaji siku ilipofika alipanda bus na kwenda Tarime hivyo kuwaachana wenzake wakiandamana hivyo kuambulia kupewa barua za onyo na wengine kusimamishwa chuo wakati yeye kama kiongozi akitokomea mbali.

Asanteni.
1.
 
Back
Top Bottom