Unbeaten hii maana yake Yanga siyo ya ligi hii ya NBC

Ni upungufu wa maarifa kujisifu kuwa una rekodi bora ndani, wakati huo huo ukienda nje unapakatwa .
Kaka kunywa mtori bila wasiwasi nyama utazikuta chini ya bakuli. Yanga tangu ianzishwe 1935 haijawahi kupata viongozi vijana na wasomi kama ilivyo sasa, mshindo msolla ana PhD na Eng. Hersi na timu yake ni wasomi kwelikweli wasioamini kwenye uchawi kama akina Mangungu, Kaduguda na wenzake. Yanga inasajili wanachama wengi kwa usahihi na Yanga inasajili wachezaji kwa usahihi, Yanga ina wadhamini wa uhakika tofauti na akina Gulamali rip na wengine. Yanga hii itakuwa ya kwanza kuleta kombe la caf Tanzania, hifadhi maneno yangu mahala penye usalama. Yanga hii ya sasa haiwezi tena kufanya usajili wa mchezaji aliye chini ya hawa waliopo sasa wanaoipata Yanga unbeaten 49, haiwezi kuleta kocha mwenye uwezi chini ya Nabi na kaze, Yanga hii haiwezi kuwa Rais ambae ni chini ya Hersi. yanga hii inakwenda kule waliko wenzetu wanaoshinda vikombe.
 
Back
Top Bottom