Unayopitia yote ni mpango wa mungu.

Unayopitia yote ni mpango wa mungu.

Then the concept of freewill becomes an illusion.

Kama kila kitu kitokeacho kwa mwanadamu ni mpango wa huyo Mungu, ina maanisha kwamba binadamu  hana uhuru na hiari ya kuchagua na kufanya mambo yake mwenyewe.

Kwenye kitabu cha philosophy of religion hii ishu imeongelewa.

Kwamba, God's foreknowledge and human freewill are incompatible.

Ujuzi wa Mungu kujua na kupanga yote na Hiari ya mwanadamu kuamua na kupanga mambo yake mwenyewe, haviendani na havipatani.

Kwa sababu,

Ikiwa Mungu ndiye mpangaji wa kila kitu, then Binadamu hana uhuru wala hiari ya kuamua na kujipangia mambo yake mwenyewe. Kwa vile Mungu ndiye mpangaji.

Ikiwa Binadamu ana freewill, then Mungu sio mpangaji wa kila kitu. Na Binadamu hapangiwi mambo.

Mungu kupanga mambo na hapohapo Binadamu kuwa na freewill kunatengeneza utata wa kimantiki (logical contradiction).
 
Huo nao ulikuwa mpango wa mungu.
Hapana....... MUNGU anajua yote haimaanishi yeye ndiye anayepanga wewe uasi, hata hivyo ameshajua wewe Yoda mwisho wako utakuwaje, na wewe ndiye unaye amua umwamini au usimuamini,.
 
Hii mada haifiki mwisho
kwamba shetani kafanya shambulio la kushtukiza? , ukiangalia muundo ulivyo kimsingi sana waumini wanatakiwa kumsapoti shetani maana anaplay nafasi muhimu sana na jukumu alilopewa, tofauti na hapo ni kama mnasema shetani amemzidi nguvu
 
Kama unamuamini mungu kila unachopitia ni mpango wake mungu.

Kama wewe ni masikini huo ni mpango wake,

Kama umedhulumiwa huo ni mpango wake,

Utawala wa CCM ni mpango wake,

Kama unaumwa huo ni mpango wake,

Ukifiwa ni mpango wake,
Ukifungwa ni mpango wake,

Ukiibiwa ni mpango wa mungu,

Ukibakwa au kupakwa mafuta ni mpango wa mungu,

Wewe kufa kwa kifo chochote ni mpango wake,
Kwa hiyo hata waliotekwa,watakaao tekwa waamini ni mpango wa Mungu,🤔
 
Back
Top Bottom