Unawezaje kumsamehe aliyekukosea?

Unawezaje kumsamehe aliyekukosea?

Hivi unaweza kumsamehe mtu ambaye anakusemea mabaya kwa Mabosi? Yan anakusemea, na mnaitwa Kikaangoni? Unaanzaje hapo kwa mfano kumsamehe?
 
Magonjwa mengi ya moyo pamoja na presha zinasababishwa na msongo wa mawazo! Mtu unatumia nguvu nyingi sana kumchukia na kumbeba mwenzako moyoni. Mtu akikosea ukamsamehe haimaanishi unamfaidisha yeye ila ni kwa faida yako.
Kama ni rafiki kakukosea sana inabidi umsamehe tu ila haimaanishi umuamini kama zamani.

Muombe Mungu akusaidie kukupa moyo mwepesei na wa kusamehe... Si kazi rahisi.
 
Ila mimi mkuu sijui binadamu wa namna gani huwa situnzii kitu. Ukinikosea kesho yameshaisha nakuona mpya
Yaani mimi ukinikosea namwambia wala silali nalo. Nikimwambia tu moyo wangu unalegea na kusamehe
 
Magonjwa mengi ya moyo pamoja na presha zinasababishwa na msongo wa mawazo! Mtu unatumia nguvu nyingi sana kumchukia na kumbeba mwenzako moyoni. Mtu akikosea ukamsamehe haimaanishi unamfaidisha yeye ila ni kwa faida yako.
Kama ni rafiki kakukosea sana inabidi umsamehe tu ila haimaanishi umuamini kama zamani.

Muombe Mungu akusaidie kukupa moyo mwepesei na wa kusamehe... Si kazi rahisi.
Sawa mkuu shukrani kwa ushauri wako.
 
Yaani mimi ukinikosea namwambia wala silali nalo. Nikimwambia tu moyo wangu unalegea na kusamehe
maisha yanaenda hivyo. sio unafurisha moyo kama andaziii....
 
Ni vizuri kusamehe whether umeombwa msamaha au hujaombwa msamaha it's gud for ur health

Hadi nitoe chozi Kweli hicho kitu kinakuwa kimeniuma sana, though kulia kunanipa relief
 
Wakati mwingine ni ngumu sana kusamehe si mambo ya mchezo mchezo, na hilo cyo tatizo lako pekee yako ila mm ninachofanya ninasamehe haraf siwi tena karibu na huyo mtu hata kucheka naye mara kwa mara sitaki kabisa.
 
Kwa mfano kama kidume kakupa mimba halafu kakukataa, bhasi unamchukulia kawaida tu ili usilee mimba kwa hasira hata ukamuathiri mtoto aliyetumboni mwako, unakiri mbele za Bwana kuwa umemuachilia kosa lake bila kumlipa lolote baya, endelea na maisha yako, ukijifungua lea mtoto kwa upendo na siyo kumwambia maneno ya chuki/mabaya aliyokufanyia baba yake.
 
Kusamehe ni maamuzi magumu sana kuyachukua hasa pale inapokuja kuumizwa kihisia au kiuchumi....inahitaji ukomavu wa kiakili na kimtazamo kwa ujumla kukubali kupitisha msamaha kwa aliyekukosea
Lakini ukweli kusamehe kutakuweka huru sana kuliko kukaa na fundo la hasiri/chuki kifuani mwako
 
Watu wengi muhimu katika maisha yangu wameniangusha sana tu.Wote hao nimewasamehe ILA SIWIZI KUWASAHAU.
Hawapo ktk moyo wala mdomo wangu.Ndio kwanza Na waona Na kuwasikia.
 
Hivi unaweza kumsamehe mtu ambaye anakusemea mabaya kwa Mabosi? Yan anakusemea, na mnaitwa Kikaangoni? Unaanzaje hapo kwa mfano kumsamehe?
Huyo unamsamehe usiku tu ukilala, ila kukikucha chuki ziendelee maana ndo muda wa kutafuta riziki af yeye anazifunga.
 
Kuna tofauti kati ya KUSAMEHE na KUPUUZA. Ukisamehe inamaana unamfutia mtu hatia ya kosa lake anakua kama hajakukosea kisha uhusiano unaendelea. Ukiua uhusiano hujasamehe umefanya kitu ingine. Kupuuza ni kutotaka kufanya suluhu wala nn ila unachikulia poa tu nafsini mwako ila kuna namna utamuavoid au kubadilisha mazingira etc. The best way ninkusamehe. Hii inaonesha advanced maturity behaviour.

Mfano wazazi wetu tuliwakosea sana tukawakwaza sana pengine walilia sababu yetu lakini waliamua kutusamehe na bado wakatusaidia kufikia ndoto zetu. Japo wapowazazi wachache waliosusa watoto wao kwa sababu ya makosa fulani

Mkuu naomba tujadili theory yako ya kusamehe. Umesema, "Ukisamehe inamaana unamfutia mtu hatia ya kosa lake anakua kama hajakukosea kisha uhusiano unaendelea. Ukiua uhusiano hujasamehe umefanya kitu ingine."

Je, ukisamehe na kuua uhusiano unakuwa umefanyaje?

Haiwezekani kusamehe na ku-move on na mwingine?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom