Unaweza kurudisha Muamala wa Fedha iliyotumwa kimakosa kwenye akaunti yako ukiwa umefulia mbaya?

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Chukulia umekata ringi balaa halafu mtu kajichanganya katuma fedha kwako iwe kwenye akaunti ya Benki au Simu halafu akaomba urudishe, utatuma hiyo hela?

1705327220464.png
 
Mimi niliwahi kukosea no,pesa ikaenda sehemu nyingine,nika mpigia jamaa akasema nakutumia kesho asubuhi ili nijilizishe,kama hatatokea mwingine wa kunipigia,nikaandika maumivu lakini jamaa alikua mwema sana kweri alinitumia.

Tangu siku hiyo akawa lafiki yangu,badae nika muuliza aliwezaje kuludisha? Akasema asingeweza kula pesa ambayo sio jasho lake pia labda pesa ilikua inaenda kwa mgonjwa ili akapate matibabu,jamaa anaishi ukerewe Mungu ampe maisha malefu.
 
Hii hali imewahi kunitokea mara 3 na zote nimepigwa ! Mara ya kwanza alipokea kijana nikamfahamisha nimekosea nimetuma pesa kimakosa , akanijibu ngoja aangalie, baadaye nilipompigia akanijibu ni kweli ila ameitoa na kaitumia akipata atanirudishia !! Nikamjibu sawa ila isimuumize kichwa akiona ni haki yangu anirudishie lkn akiona ni haki yake sina KINYONGO.

Mwingine nilikosea yy hakutaka hata kupokea simu yangu. Nikamuandikia sms kuwa ni fedha kwa ajili ya mgonjwa hakujibu.

Mwingine nilipokosea nikamjulisha yule niliyekuwa namtumia nikampa namba ya simu , alipopiga AKAOGA matusi nikawasiliana na VODA nikapewa jibu Jamaa kesha itoa .

Live nikiwa natembea barabarani nikaiona 5,000/= nikaiokota, halafu nikahisi yawezekana ni ya hawa vijana wanaouza miwa barabarani wakati nataka kwenda kuwauliza kijanja.

Nikamuona jamaa mbele yangu kwa mbali anajipekuapekua , nilipomsogelea nikamuuliza vp, akajibu nimepoteza fedha nikamuuliza shilingi ngapi?

Akajibu 5,000/= nikamwambia haya hii hapa basi tukaendelea kupiga stori nikamwambia kwangu mm ni ngumu ssna kula fedha kama hiyo yaani sitapata AMANI ya moyo kabisaa
 
Ntairudisha tu....
Maana nishawahi kosea muamala pesa nyingi tu kwenda kwa mama, niliurudisha chap na ile namba ilikua haipatikani, nlikosea digit moja tu.
Aisee nlipata jasho la maana, huyo mtu Angesepa nayo sijui ingekuwaje.
Toka hapo siku nikipokea muamala wa mtu ntaurudisha tu
 
Mimi niliwahi kukosea no,pesa ikaenda sehemu nyingine,nika mpigia jamaa akasema nakutumia kesho asubuhi ili nijilizishe,kama hatatokea mwingine wa kunipigia,nikaandika maumivu lakini jamaa alikua mwema sana kweri alinitumia.

Tangu siku hiyo akawa lafiki yangu,badae nika muuliza aliwezaje kuludisha? Akasema asingeweza kula pesa ambayo sio jasho lake pia labda pesa ilikua inaenda kwa mgonjwa ili akapate matibabu,jamaa anaishi ukerewe Mungu ampe maisha malefu.
ilikuwa sh. Ngapi mkuu
 
Mama mtoto wangu wa kwanza nilimpata kwa njia hii,...
Alikosea kutuma 520,000 alikuwa anamtumia kaka yake huko kijjn..ile hela nikaihamishi betway yote(nlipokuwa hapakuwa na huduma ya kutoa),..

Story ndefu lakini niliirudisha ile fedha yote na sikumtafuta wala kutaka shukran bc alijua me tajiri kweli..
 
Hii hali imewahi kunitokea mara 3 na zote nimepigwa ! Mara ya kwanza alipokea kijana nikamfahamisha nimekosea nimetuma pesa kimakosa , akanijibu ngoja aangalie, baadaye nilipompigia akanijibu ni kweli ila ameitoa na kaitumia akipata atanirudishia !! Nikamjibu sawa ila isimuumize kichwa akiona ni haki yangu anirudishie lkn akiona ni haki yake sina KINYON
Pole sana
 
Mimi niliwahi kukosea no,pesa ikaenda sehemu nyingine,nika mpigia jamaa akasema nakutumia kesho asubuhi ili nijilizishe,kama hatatokea mwingine wa kunipigia,nikaandika maumivu lakini jamaa alikua mwema sana kweri alinitumia.

Tangu siku hiyo akawa lafiki yangu,badae nika muuliza aliwezaje kuludisha? Akasema asingeweza kula pesa ambayo sio jasho lake pia labda pesa ilikua inaenda kwa mgonjwa ili akapate matibabu,jamaa anaishi ukerewe Mungu ampe maisha malefu.
Ulimpa zawadi gani?
 
R&L,zingatia.
 
Huwa nikipata pesa bila taarifa siitoi
Kwa muda wa saa 48 au zaidi ili kwamba imekosewa irudi ilipotokea, vinginevyo ndani ya muda huo huwa napigiwa simu ya hama pesa imekosewa au kuna mtu kanilipa.
 
Back
Top Bottom