Unaweza kuizungumziaje Picha hii??

Unaweza kuizungumziaje Picha hii??

1554364_591839254230755_1557013582_n.jpg

Je wanajitambua na wanajua wanachoshabikia,au wanafata mkumbo tu?

Ingependeza ungeonyesha upande wa pili wanapoamkia ili uonyeshe umasikini wao ulivyotamalaki hiki chama kinatumia umasikini km nyenzo kuu kushinda uchaguzi
 
Hao ndo wapiga kura nchini Tanzania. Wengi humu tunawasakama lakini kura hatupo tayari kupiga!

Tusiwalaumu kwa maamuzi wanayofanya; tuwasaidie kufanya maamuzi sahihi!
 
Hongera sana kwa kulitambua hilo. Si kama hizi saccos ambazo wengine ndo hupata sababu za kujipatia mahawara wa chee

kama mwiguru alivyojipatia kashonza kupitia ngo iitwayo ccm, uko sahihi mkuu nakuunga mkono
 
CCM ni chama makini katika kuhakikisha mavazi na nguo na vyakula vyote vinawafikia watu wakati wote wa mikutano yao.
ImageUploadedByJamiiForums1389699163.970392.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1389699197.729969.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1389699226.221741.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1389699261.960127.jpg
 
Hao ndo wapiga kura wakuu wa CCM na wanapatikana vijiji vyote vya Tanzania.Mtaji mkubwa kabisa wa CCM ni kufanikiwa kuwanyima ELIMU watu hawa!
 
"..vigelegele & makofi tafadhali kwa chama cha Mapinduzi..."
 
!
!
huko ni pwani kwa akina yakheeeeee, kama sio bagamoyo au mwambao wa pwani basi ni kigoma kwa akina Ziggo
 
Bila kumung'unya maneno, hao hapo kwenye picha wameletwa kwa fuso kutoka mbali. Mwaliko wao kadi ni hiyo khanga na hiyo tshirt ya yello. Wangeangaliwa miguuni, hao hawana hata yeboyebo.
Nilipomsikiliza msemaji au huyo mwenye kuhutubia nilisikia akisema. Sasa tumemaliza na wazee wangu mmekaa sana hapa, najua mmetoka mbali na mna njaa. Pale mbele palee chini ya mbuyu kuna pilau na nyama pori ya tembo. Mkimaliza kula mtarudishwa kwenu na kila mmoja atapewa buku 2 ila nawaapisha msipokichagua hiki chama mtalaaniwa kwa kula bila kukichagua chama chenu.
Siisiieem Oyee. Wakapiga kelele; Oyeeee. Ndipo nikawapiga hii picha. nawasilisha
 
Ha ha ha! Mbavu zangu!
 
hao hawana hata uwezo wa kuhoji kwanini hawatibiwi bure wakati CCM iliahidi kufanya hivyo, mwalimu wa chekechea kwao n kama rais...kwa kifupi hawajui haki zao hata moja zaidi ya kuvaa hizo khanga, vilemba na t-shirt. Kweli CCM hawana huruma, wanawatesa hadi hawa wazee kwa kuwahonga chumvi!!!
Ee Mungu tusaidie.
 
Back
Top Bottom