Unatumia utaalamu gani kufanya chapati zako za kusukuma ziwe laini?

Mie huwa nachemsha maji kidogo yawe vuguvugu, nitatia chumvi na sukari kidogo (napenda zenye sukari)kwenye maji.. 👍

Naweka unga wangu kwenye bakuli alafu nitatia mafuta wastani(mie natia mafuta baridi tu) nikipenda natia iriki ilio sagwa na yai au blueband (ila sio lazima).😀😀

Nachanganya hapoo mvurugo wangu alafu natia yale maji vuguvugu yenye mchanganyiko wa sukari na chumvi.. Nakanda taratibu, hadi donge liwe laini laini sana kiasi kinichovya kidole kwenye donge kinafika hadi chini.. Hapo naendelea kukanda vizuri na kusawazisha donge langu, nafunika dakika 5 alaf naanza kuandaa vidonge vidogo vya size ninayotaka, nita sukuma ijae duara alafu nitapaka mafuta na kuzikunja..👌

Nikimaliza kukunja naanza kusukuma kwa ajili ya kuchoma, moto pia uwe wastan maana hazitaki moto mwingi wala kidogo,huenda zikaungua kabla ya kuiva vizuri au zikawa mbichi.
Basi natia kwny flying pan hapo ukiiva upande wa kwanza na kuwa fluffy (zinapanda hivi) nageuza upande wa pili ukiiva ndo natia mafuta kidogo kila upande nageuza. Apo ikipoa inakua tam na tiari kwa kuliwa.. Sis Depal 😜😜😜
 
Back
Top Bottom