Chapati za kusukuma za mayai, iliki, siagi na maziwa ya unga

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,492
9,264
Mahitaji
  • Unga wa ngano kilo 1
  • Mayai 2
  • Chumvi
  • Maji
  • Siagi (butter) vijiko 3 vikubwa
  • Mafuta ya kula kwa ajili ya kuchomea
  • Iliki ya unga
  • Maziwa ya unga vijiko 3 vikubwa

Maelekezo
  • Weka unga kwenye beseni au sufuria kavu kisha weka chumvi kiasi, maziwa vijiko 3 vya chakula na hiriki. Changanya mpaka uhakikishe vimechanganyikana vizuri.
  • Weka butter vijiko vitatu kwenye unga kisha changanya. Changanya hadi butter ishikane na unga vizuri na iwe na uwiano mzuri (isionekane kabisa).
  • Pasua mayai pembeni, yakoroge vizuri na kisha weka kwenye unga. Changanya zaidi hadi upate uwiano unaofaa.
  • Ukiona uwiano mzuri wa unga wako, weka maji ya uvuguvugu kwenye unga na anza kukanda. Kanda unga mpaka uwe laini na haushikani na chombo unachokandia wala haunati kwenye mikono. Hapo unga utakua tayari.
  • Kata mabonge ya unga kwa umbo la mviringo kisha weka kwenye chombo pembeni. Rudia hili zoezi hadi unga uishe.
  • Chukua donge mojamoja, paka unga weka kwenye kibao cha kusumia chapati. Sukuma chapati hadi iwe sawa. Paka mafuta kwenye chapati na anza kukunja.
  • Rudia hilo zoezi kwa madonge yote yaliyobaki. Ukimaliza, anza kusukuma chapati zako kwa ajili ya kupika.
  • Bandika kikaango jikoni. Acha kipate moto vizuri.
  • Weka chapati, acha iive hadi iwe rangi ya kahawia. Geuza upande wa pili, paka mafuta upande uliokua wa kahawia. Geuza, paka mafuta tena upande mwingine.
  • Hakikisha chapati inaiva vizuri na inachambuka,hapo utakua umemaliza kazi na tayari kula chapati zako.
 
duh! dunia uwanja wafujo at mimi nawasaga kama hii mama yaleo haiko na time,je itafanyaaje? but asante sana mwanike nahene
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom