Unatumia utaalamu gani kufanya chapati zako za kusukuma ziwe laini?

Black Opal

Senior Member
Jan 22, 2023
199
257
Habari Wakuu,

chapati.jpg

Chapati za kusukuma ni pishi ambalo limekuwa changamoto kwa watu wengi, mtu anajitahidi alkini mwisho wa siku anatoa chapati ngumu na imesimama kama sinia😂🤣.

Mbinu ninayotumia mimi kufanya chapati iwe ni laini, ni kukanda unga na kuhakikisha umekuwa laini kabisa. Tumia hata muda mrefu kama huna nguvu sana mikononi ila hakikisha donge lako linakuwa laini kabisa. Na kipindi unakunja mwanzo fanya iwe nyembamba sana kama karatsi, muda wa kusukuma ili uchome iwe wastani, isiwe nene sana haitaiva na isiwe nyembamba sana itakua kaukau.

Pia wakati wa kuchoma, kama umeweka chapati kwenye kikaango na haifuri jua kuna kitu umekosea, inaweza kuwa hujakanda unga vizuri au umeweka nene.

Lete maujuzi yako mpishi, unatumia njia gani kufanya chapati yako inakuwa laini?
 
Kuna kijiji moja nlienda, kuna migahawa miwili.
Wa kwanza n mams mmoja anajidai mjanja mjanja, akipika chapati anaweka kama 10 hv kwenye kikaango, zikitoka n kama shuka za gesti, nyeupee af mbichi!
Wa pili n mmama mtu mzima, ye hana haraka, taratiibu hatauwe mia, atachoma moja moja. Changamoto yake ni hygiene. Anaeza akasukuma, ghafla akajikuna mguu af akaendelea. Lakini zake zimeiva na tamu.
But kwa hawa wadada wa siku hz kabla hujaeka kambi bora ujue kwanza anaju kuzisukuma au la. Maana unaoa pisi kali, af anakupikia "amoeba" instead of chapoo
 
🤣🤣 bado hujaona anatumia msukumio kukunia mgongo
 
Back
Top Bottom