Unataka kuwa dereva Dsm? Soma hapa

Unataka kuwa dereva Dsm? Soma hapa

ChescoMatunda

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2009
Posts
1,232
Reaction score
443
KAMA UNGEPENDA KUWA DEREVA JIJI LA DSM SOMA KWA MAKINI
1:Uwe mvumilivu sana Usiekata tamaa kusubiri wenzio wakupishe
2:Ujue kusafiri masaa mawili hadi matatu umbali wa km 10 tuu.
3:uwe unatembea na chenji na noti noti za faini kwa trafiki hata kama gari yako mpya
4:Kama unapita mitaa huijui usishangae mzee wa makamo kajigongesha kwa mbele ya gari yako na anataka alipwe hela hapohapo!
5:usiombe upite mitaa ya mdada poa utakoma watakavyokujalia kwenye kioo.
6:jiaandae kudaiwa hela na wahuni kwenye mataa kwa lazima hata kama hujawahi kuwakopa
7:usiombe gari yako izime afu ukute vijana wanakusaidia kuisukuma ukadhani wanahuruma utadaiwa laki kama gharama ya kusukuma utadhani umetolewa na greda
8:Uwe tayari kuchomekewa na daladala popote wakati wowote
9:ukiwa kwenye foleni Biashara Zipo utauziwa kila kitu hata chipsmayai unaweza kukaangiwa
10:Ukiwa na hasira utagombana asubuhi mpaka jioni barabarani. kazi kwako.,
 
Hahahaha!kwenye jam utatamani uikunje gari km karatasi then uiweke mfukoni then usepe kwa miguu!Mistari yako ina ukweli mtupu!kazi kwao madreva wanaotaka kazi Dar.
 
Kuna wakati nilikataa kupandishwa cheo kazini kwa kutokutaka kusafiri kwenda katikati ya jiji (Dar) kazini kila siku. Niliona heri nibaki na nafasi ileile huko nje kabisa ya jiji.
 
halafu eti ni jiji la maraha. na cha ajabu walio wengi wakiingia hapa jijini hawarudi makwao.
 
11. Ukiingia kwenye gari hasira ziache nje.
12. Ujue unakazi ya kukihudumia kitambi cha trafiki na nyumba zake zoote ndogo.
 
Hahah ni kweli kabisa ndg...


Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Inabidi ufunge vioo vya gari lako hasa kwenye mataa, vinginevyo utatemewa makoozi na mateja ambao umewanyima pesa!
 
hapo ukiwa na appointment inabid uongeze masaa 2 mbele
 
usishangae kuoshewa vioo vya gari lako kwa lazima mara tu ukisimama kwenye mataa
 
...hiyo no.9 nimeipenda,kama inawezekana iwepo na huduma ya choo...
 
11. Ukiingia kwenye gari hasira ziache nje.
12. Ujue unakazi ya kukihudumia kitambi cha trafiki na nyumba zake zoote ndogo.
13.usiombee ndo kuwe na mvua dsm utakoma kwa foleni utadhani kuna msiba wa nyerere maana uwanja wa taifa..
 
13.usiombee ndo kuwe na mvua dsm utakoma kwa foleni utadhani kuna msiba wa nyerere maana uwanja wa taifa..
14) Unapoingia Petrol Station, make sure macho yako hayabanduki kwenye kisoma bei cha pampu, hukawii kulipishwa/kuunganishiwa na bei aliopita kabla halo ukalipa zote.
 
Back
Top Bottom