Unapotaka kuagiza gari au chochote nje ya nchi, usikurupuke..

Jun 1, 2021
99
104
Habari za wikiendi pevu wadau wa JF,

Kutokana na uzoefu wetu, tumeshuhudia watu wengi wakipata hasara pale wanapoagiza
bidhaa nje ya nchi kutokana na sababu mbalimbali.

Ni kweli kuagiza kutoka nje ni nafuu kuliko kununua hapa nchini, lakini ni lazima kuwa mwangalifu kuepuka kupata hasara na kupoteza muda.

Yapo mambo muhimu ya kuzingatia kabla hujafanya maamuzi ya kuagiza bidhaa yoyote kutoka nje ya nchi. Leo tutumie mfano wa bidhaa ya gari kwa sababu vijana wengi wanaoagiza kwa mara ya kwanza wamekuwa wahanga wakubwa.

Post inayofuata hapo chini tumekuwekea tahadhari za kuchukua kuhakikisha unaagiza ndinga yako bila wasiwasi:

1. BEI

Kabla ya kununua gari ulitakalo, hakikisha unafanya uhakiki wa bei ya model hiyo sokoni kwa wakati huo, ushuru wa kusafirisha, pamoja na gharama zote za jumla utakazotumia hadi unaipata gari yako. Usikurupuke kulipia gari kabla hujajua utatumia kiasi gani.

2. HALI YA GARI

Kabla ya kufanya manunuzi au malipo, tazama picha zilizopostiwa kwa umakini kuhakiki hali ya gari.

Angalia vioo, matairi, milango na sehemu zote zilizopigwa picha uone kama hazina hitilafu. Hakikisha picha zinakuridhisha na hazikupi mashaka.

3. MUUZAJI (SUPPLIER).

Gari unanunua wapi? Hili ni muimu sana. Hakikisha unanunua gari kutoka kwa kampuni inayoaminika. Uliza kwa mtu unayemfahamu kama aliwahi kununua kwenye hiyo kampuni akupe ABC zake. Ikibidi pitia maoni ya wateja kwenye tovuti kujiridhisha.

4. USHURU WA BANDARI

Angalia gharama utakazolipia baada ya gari kuwasili bandarini. TRA wana calculator yao ya mtandaoni, unaweza kuingiza taarifa za gari unalolitaka kisha itakuletea makadirio ya kodi utakayolipa. Ukiona inaendana na bajeti yako, ruhusa kuagiza.

5. SHERIA NA TARATIBU

Zingatia sheria na taratibu za kuingiza gari nchini. Mfano magari yaliyotumika kwa zaidi ya miaka 5 hutozwa ushuru mkubwa zaidi.

Pia, utaratibu rasmi wa nchi ni kuendesha magari yenye usukani kulia (RHD) na sio yenye usukani kushoto (LHD).

Kwa kuongezea tu:

Tunashauri kutafuta ushauri kutoka kwa mawakala waaminifu kuhusu wakati sahihi wa kununua gari hasa kwa nchi kama Japan, UK na South Africa.

Mawakala huwa wanafahamu misimu ambayo gari hushuka sana bei kutokana na sale offers zinazotolewa na suppliers.

Tunaweza kukusaidia pia juu ya hilo kwa sababu tunashirikiana na suppliers wengi kutoka nchi tajwa.

Karibu tuwasiliane.
 
Kwa kuongezea tu:

Tunashauri kutafuta ushauri kutoka kwa mawakala waaminifu kuhusu wakati sahihi wa kununua gari hasa kwa nchi kama Japan, UK na South Africa.

Mawakala huwa wanafahamu misimu ambayo gari hushuka sana bei kutokana na sale offers zinazotolewa na suppliers.

Tunaweza kukusaidia pia juu ya hilo kwa sababu tunashirikiana na suppliers wengi kutoka nchi tajwa.

Karibu tuwasiliane.
Habari ya mafuta gani hawaulizi kwenye hiyo miaka zaidi ya mitano(5)?Na je km zilizopo kwenye gari hazina madhara yoyote?
 
Habari ya mafuta gani hawaulizi kwenye hiyo miaka zaidi ya mitano(5)?Na je km zilizopo kwenye gari hazina madhara yoyote?
Maswali mazuri na muhimu.

Unapochagua gari, miongoni mwa specifics ambazo unatakiwa kuzifahamu ni pamoja na uchakavu wa gari (kama ni used), umbali iliotembea na aina ya mafuta inayotumia.

Kwa vile gari hutofautiana, WLC tunatoa ushauri elekezi kulingana na aina ya gari analotaka kuagiza mteja.
 
Umekaribisha watu muwasiliane bila kuweka njia ya mawasiliano au ni kupitia hapa hapa JF

Ni kweli. Njia ya kwanza kwa hapa JF ni kututumia PM.

Kwa mawasiliano zaidi, namba zetu za ofisi ni 0784271957 au email info@worldlogisticstz.com

Ofisi zetu zipo Posta, Mtaa wa Mkwepu Jengo la Diplomat House ghorofa ya 3. Jengo hili lipo nyuma ya Ofisi za RITA hapa Dar es Salaam.

Karibu.
 
Back
Top Bottom