Unapogundua jina la mtoto wako

CPU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
3,863
686
Habari wana JF
Nimekuwa nikijiuliza kwa namna fulani suala la uchaguzi wa jina la mtoto.
Mfano, mmezaa mtoto na mpenzi wako.
Wakati wa kupendekeza jina kwa mtoto, mpenzi wako akawa anasisitiza sana apewe jina fulani. Ukakubaliana nae.
Baada ya muda fulani, ukaja gundua kwamba hilo la mwanao ni jina la X-lover wa mpenzi wako
Utajisikiaje, au utafanyaje??
 
haya maswali mengine bana!
unataka niseme nitalibadilisha au?
ndo sababu hutakiwi kufuatilia sana vitu ambavyo hata usipofuatilia havina athari.
umegundua sasa, na ulisha muoa mama yake, na ulishambatiza mtoto.
unaanza kuumia kichwa buure.kumbe hata usingefuatilia isingekua na tatizo.

jamani! msipende sana kutafta opportunity ya kuwa doubt wapenzi wenu manake lazima mtazipatatu!
hata wao wakitafuta za ku wa doubt ninyi watazipatatu, mwisho wa hizi doubt ni kutokuepo kwa imani kwa mwenzio
na hatimae mtafaruku kwa mapenzi yenu.
 
kikubwa ni wewe kujua kwanini ulilikubali hilo jina la mtoto, kama ni maana ya jina,unapenda linavyotamkwa yaani vitu vyote ambavyo vilikufanya ukubali hilo jina.

haya maswali mengine bana!
unataka niseme nitalibadilisha au?
ndo sababu hutakiwi kufuatilia sana vitu ambavyo hata usipofuatilia havina athari.
umegundua sasa, na ulisha muoa mama yake, na ulishambatiza mtoto.
unaanza kuumia kichwa buure.kumbe hata usingefuatilia isingekua na tatizo.

jamani! msipende sana kutafta opportunity ya kuwa doubt wapenzi wenu manake lazima mtazipatatu!
hata wao wakitafuta za ku wa doubt ninyi watazipatatu, mwisho wa hizi doubt ni kutokuepo kwa imani kwa mwenzio
na hatimae mtafaruku kwa mapenzi yenu.

Nadhani unaenda kusiko kabisaaaaaa!
Na ufahamu kwamba, kuja kujua kitu sio mpaka uwe umekipeleleza.
Vingine vinakuja automatically unajikuta umeshagundua hivyo
Usiwe na mawazo ya kufikiria kila kitu kinaletwa kwa lengo la kuchonganisha ndugu

Kwani tukisema tuanze kufuatilia kila afanyalo binadamu kuna mtu atapona?
Think in a positive way ndugu . . .
 
Kikubwa ni kuhakikisha huwi katika mahusiano na mtu ambaye atakufanyia kitu kama hicho, huyo anaweza hata kukulisha mavi.

I guess sijajibu swali, kubadilisha jina si kazi unaweza kufanya hivyo kama inakuuma kihivyo.

Halafu kuanzia siku hiyo marufuku kulisikia jina, on the threat of a divorce.

That is a type of infidelity, cheating actually. It's like every time your love mentions that name he/she comes in his/her mind.
 
Habari wana JF
Nimekuwa nikijiuliza kwa namna fulani suala la uchaguzi wa jina la mtoto.
Mfano, mmezaa mtoto na mpenzi wako.
Wakati wa kupendekeza jina kwa mtoto, mpenzi wako akawa anasisitiza sana apewe jina fulani. Ukakubaliana nae.
Baada ya muda fulani, ukaja gundua kwamba hilo la mwanao ni jina la X-lover wa mpenzi wako
Utajisikiaje, au utafanyaje??

Tafadhari andika jinsia yako (mwanaume/mwanamke) na kisha eleza uhusiano wako na yeye kama ni ndoa, wapenzi mnaoishi pamoja kwa muda mrefu au mfupi na jinsia ya mtoto. Pia eleza jamii inayowazunguka inawatambuaje! Baada ya hapo nitatoa ushauri wangu kutegemea na taarifa nilizoomba. Nina mfano wa kesi yako, inayomhusu rafiki yangu wa karibu
 
Kuna ubaya gani? Binti yangu nimempa jina la binti niyempenda akanitolea nje ikiwa ndio njia pekee ya kumsahau
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Haya yote yanatokana na sie wazazi wa siku hizi kujitia tunakwenda na wakati...wazee wetu walikuwa wanajua majina na maana ya majina ya watoto wao kwa kuwa they used to name them after their relatives and elders. Sasa siku hizi na hizi imani za flani ana tabia mbaya so mtoto akirithi jina lake atakuwa kama yeye, sijui ni jina korofi n.k. ndo hapo kila mtu anatoa jina alipendalo, nasi tunakubali pasipojiuliza linakotokea (na siku hizi kuna vitabu na sites za majina) Mwe!!
 
  • Thanks
Reactions: CPU
Ukiona mumeo au mkeo anatoa jina la x kwa mtoto wenu jua wewe ni kama maji kutuliza kiu ya soda. Kwa ufupi ni kuwa umuoa/kakuo basi tu kwa kuwa mwenye hilo jina amemtolea nje. Kha! Hilo kosa kwa kweli ni ngumu sana kupata msamaha. Giving "our childe" your lovers name??? Wazazi kama hao ndio wanaobaka watoto wa kuwazaa. Mapenzi ya ex yanaamia kwa mtoto
 
Haya mambo yapo lakini. Kuna jamaa alisoma na hubby mwanae ana jina la binti nilyesoma nae mimi. Hubby aliwahi nambia kuwa jamaa alikuwa anamzimikia vibaya sana huyo binti ila sidhani kama aliwahi kumchukua. Hiyo stori alinambia wakati tuko wote college. Mume wangu hajuhi jina la mtoto wa huyo jamaa kwani they were not that much close na urafiki si wa kiivyo hasa baada ya kumaliza shule. Mimi najua kuwa mtoto wao ana jina la yule binti kwani nawafahamu wote huyo wife na binti mwenye jina. What I think ni kuwa mke hajuhi kuwa mumewe alikuwa amemzimikia mdada mwenye jina la binti yao. Siwezi kuthubutu kusema na najua mkewe hatakaa ajue.
 
he he heeee halafu siri za aina hiyo huwezi jua
inaweza kuja kufumuka katika mazingira ya ajabu mno........
ni kama filam za kihindi hivi....unakuja kujua ukweli miaka kumi imepita.....
 
Tafadhari andika jinsia yako (mwanaume/mwanamke) na kisha eleza uhusiano wako na yeye kama ni ndoa, wapenzi mnaoishi pamoja kwa muda mrefu au mfupi na jinsia ya mtoto. Pia eleza jamii inayowazunguka inawatambuaje! Baada ya hapo nitatoa ushauri wangu kutegemea na taarifa nilizoomba. Nina mfano wa kesi yako, inayomhusu rafiki yangu wa karibu

Daaaah
Anyway, SO mimi ni kijana wa kiume, na habari niliyoandika sio tukio lililonikuta, la hasha!!
Ni kitu ambacho kimenijia akilini wakati nafikiria haya masuala ya mahusiano, na nimeweka hapa jamvini nikijua linaweza kutokea kwa yeyote.
So kushauriana ni vyema kiasi kwamba hata likitutokea kati yetu mbele ya safari tunakuwa angalau na kujiandaa
Mwaga maoni yako
 
Haya yote yanatokana na sie wazazi wa siku hizi kujitia tunakwenda na wakati...wazee wetu walikuwa wanajua majina na maana ya majina ya watoto wao kwa kuwa they used to name them after their relatives and elders. Sasa siku hizi na hizi imani za flani ana tabia mbaya so mtoto akirithi jina lake atakuwa kama yeye, sijui ni jina korofi n.k. ndo hapo kila mtu anatoa jina alipendalo, nasi tunakubali pasipojiuliza linakotokea (na siku hizi kuna vitabu na sites za majina) Mwe!!

Sikujua, Siyawezi, Majuto, Fikiri, Sikudhani, Pilli,Tatu............ do you mean these names?
 
Kuna ubaya gani? Binti yangu nimempa jina la binti niyempenda akanitolea nje ikiwa ndio njia pekee ya kumsahau

Hakuna ubaya ndugu, ni vile tu kila mtu anavyojisikia.
Wewe umempa jina la mrembo ambaye simply haujawahi kuwa nae kimapenzi. Lakin kwa mwingine si rahisi kuamua hivyo.
Assume umepata mtoto mwingine wa kiume na mkeo akampa jina la bwana wake kabla yako . . . kwako utajisikiaje?
 
Back
Top Bottom