Unapofanya kitu cha umma wa Tanzania unafanya kwa maslahi ya nchi au ya kwako au kikundi fulani?

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
8,402
4,069
Nchi yetu inapitia kipindi kigumu kidogo kwa miongo kadhaa kiasi kwamba jambo hili limeota mizizi au linaota mizizi nalo ni katika kufanya mambo yetu tunaweka nafasi zetu au ubinafsi mbele kuliko maslahi ya nchi au aliyekuajiri mbele, matokeo yake ni kuua kile kilichokuweka pale iwe shirika la umma au Biashara ya mtu binafsi na hili suala lina kwenda hata katika kufanya teuzi zetu.

Je, tunayemweka pale tuna muweka Kwa sababu ya uwezo wake au kwa sababu ninayo mamlaka ya kuteua.

Pili ninayemuweka pale anaenda kufanya kazi ya Mama Tanzania au ya yule aliyemteua. Tukiweza kushinda nafasi hiyo, basi sisi kama Taifa tunaendelea kinyume cha hapo kiama tutakiona kila mtu kwa wakati wake.

Hivyo wakati wa kujirekebisha ni sasa.
 
Back
Top Bottom