Serikali inapoenda kinyume na maslahi ya Nchi inakuwa ni adui wa taifa

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,555
41,066
Kila taasisi, kila muhimili, kila chombo cha umma au binafsi, na mtu mmoja mmoja, kila mmoja kwa nafasi yake, ana wajibu wa msingi wa kulinda maslahi ya Taifa.

Na kila kinachotakiwa kulinda maslahi ya Taifa, kina uwezo wa kugeuka na kuwa adui wa Taifa kwa ama kuhujumu au kuhatarisha maslahi ya Taifa.

Serikali ikifanya jambo lolote lililo kinyume cha kulinda na kutetea maslahi ya Taifa, inakuwa adui wa Taifa. Mahakama ikifanya jambo lolote lililo kinyume au linalohatarisha maslahi ya Taifa, inakuwa adui wa Taifa. Halikadhalika kwa Bunge, raia yeyote na hata chama cha siasa.

Kwa hiyo kila raia, kila taasisi, iwe ya umma au binafsi, pamoja na Serikali, bunge, mahakama, vyombo vya ulinzi na usalama, tuna wajibu wa msingi wa kuchunguza mwenendo wa Serikali, mahakama, bunge, taasisi mbalimbali, vyama vya siasa, na hata raia mmoja mmoja, kuona kama matendo yake hayahujumu au kuhatarisha maslahi ya Taifa.

Sababu hii ya msingi ya kila mmoja kuwa mlinzi wa maslahi ya Taifa, ndiyo katika baadhi ya nchi, ilisababisha Serikali kufurushwa kabla ya muda wa kikatiba kumalizika pale ambapo umma uliona Serikali imegeuka kuwa adui wa Taifa kwa kuhujumu maslahi ya nchi na ya umma.

Na kwa nchi nyingine, mabunge yaliwahi kufurusha serikali zao pale yalipojiridhisha kuwa Serikali iligeuka kuwa adui wa Taifa kwa kujumu maslahi ya Taifa na wananchi. Lakini pia wapo marais waliowahi kuvunja mabunge, pale ambapo marais hao walijiridhisha kuwa bunge limekuwa adui wa Taifa kwa kuhujumu maslahi ya Taifa. Lakini mwamuzi wa mwisho huwa ni umma wa wananchi.

Bunge likisema Serikali imegeuka kuwa adui wa Taifa, lazima litafute uungwaji mkono wa umma. Rais akisema bunge limegeuka kuwa adui wa Taifa, lazima atafute uungwaji mkono wa umma. Chama cha siasa, wanaharakati, na awaye yeyote atakayesema Serikali imegeuka na kuwa adui wa Taifa ni lazima apate uungwaji mkono wa umma.

Umma ni mwamuzi wa mwisho. Umma upo juu ya Serikali, juu ya Rais, juu ya Polisi, juu ya jeshi, juu ya CCM, juu ya TISS, juu ya vyama vya upinzani na juu ya kila taasisi. Lakini kwa bahati mbaya, katika nchi yetu, umma haujui ukubwa wa mamlaka ilio nao juu ya yeyote, na mara nyingi umejiweka chini ya Serikali na vyombo vyake. Huu ni udhaifu mkubwa wa umma wa Watanzania.

Kwa sintofahamu inayoendelea sasa, ni jukumu la umma na kila taasisi kuipima Serikali, kulipima bunge na kuipima mahakama, na kuona kama kweli vyombo hivi bado ni wasimamizi wa maslahi ya Taifa au vimegeuka na kuwa maadui wa Taifa.

Wazee wetu walipambana na Serikali za kikoloni kwa sababu waliziona ni maadui wa Taifa kwa sababu hazikuwa na lengo la kulinda maslahi ya Taifa, zikiwemo rasilimali zetu mbalimbali ambazo zilitumika kuendeleza mataifa ya nchi watawala. Ikidhihirika chombo chochote kipo kinyume na ulinzi wa maslahi ya Taifa, ni adui wa Taifa, na wananchi tunatakiwa kupambana kufa na kupoma kuhakikisha maslahi ya Taifa hayahujumiwi.
 
Katika ripoti ya Jaji Nyalali ,80% walikataa kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi na 20% wakakubali yakafanyika maamuzi ya wachache wapewe na wengi wanyimwe.

Kufanya maamuzi Kwa uamuzi ya wachache usiwe ni utamaduni uliozoeleka bali lilifanyika huko nyuma kwa sababu mbalimbali.

Kulingana na utaratibu wa demokrasia ya kileo, wananchi wengi wanawakilishwa na wachache kwenye kufanya maamuzi na Kwa hapa ni wabunge kuwawakilisha wananchi.

Maamuzi ya wabunge ni maamuzi ya wananchi, kura Moja ya mbunge ni uwakilishi wa wananchi wote waliopo kwenye Jimbo lake. Serikali ni watu/wananchi na wananchi wanawakilishwa na wabunge wao.

Hivyo basi, ninaona upotoshaji mkubwa kwenye mada yako.

Kwanza, unataka kutuamisha kwamba maamuzi yanayofanywa na serikali hayaangalii maslahi ya Umma. Umma ndio hao wawakilishi wetu, maamuzi ya wabunge yamebeba maslahi ya nchi na wananchi.

Pili, naona unaangalia kwenye suala la maoni ya wachache na kutaka maoni yao yazingatiwe. Mtazamo huu ukijengeka hivi siku Moja tutakuja tuseme mshindi wa pili ndio atangazwe mshindi.
 
Hao wabunge bandia ambao hawakuchaguliwa na umma, wanamwakikisha nani?
 
Serikali isiyosikiliza wananchi wake haipo kwa ajili ya wananchi hao.
Na serikali ya namna hiyo, automatically inakuwa adui wa wananchi, na adui wa wananchi ni adui wa Taifa.
 
Back
Top Bottom