Unapoambiwa 'Akhsante' unaitikiaje?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,485
40,014
Nimefanya kautafiti ka haraka haraka na kugundua kuwa Watanzania wanashukuru kwa namna tofauti kwa kufuata jinsia zao. Na hasa pale ambapo wanajibu shukrani zinazotelewa kwao kwa kiingereza au kwa kiswahili. Hawa hasa wale walioko nje ya nchi.

Kina Dada:


Ukimwambia dada wa Kiswahili "Thank you" anajibu kwa Kiingereza "You are welcome".
Ukimwambie dada huyo huyo "asante" yeye anajibu "Karibu" (akitafsiri 'you are welcome')

Kina kaka.


Ukimwambia kaka wa Kiswahili "thank you" atajibu aidha "you are welcome" au "no problem man/hun.etc"

Ukimwambia kaka huyo huyo kwa Kiswahili "asante" yeye atasema "hamna neno, pouwa," au atajibu kwa kiingereza "anytime man, no problem" lakini hasemi "you are welcome" - ni nadra au hasemi kabisa "karibu".

Lakini ukienda kwetu kule Usukumani ukimwambia mtu "wabecha" jibu utakalolipata bila kujali jinsia ni "wabecha kulumba". Sasa siku hizi wakazi wengi wa maeneo ya Usukumani na labda imeanza kuenea maeneo mengine ya Tanzania ukiwaambia kwa kiswahili "asante" wanasema "Asante kushukuru" wakitafsiri "wabecha kulumba".

Sasa:

Mtu anapokushukuru kikwenu, jibu lake linaendena kwa ukaribu na "you are welcome" au linaendana kwa ukaribu na "asante kushukuru"?

Unafiriki kwa lugha yetu, ili ni jibu sahihi mtu anapokushukuru kwa Kiswahili na kusema "asante"? Na ipi inapaswa kufaa?
 
Ukimwambia kaka huyo huyo kwa Kiswahili "asante" yeye atasema "hamna neno, pouwa," au atajibu kwa kiingereza "anytime man, no problem" lakini hasemi "you are welcome" - ni nadra au hasemi kabisa "karibu".
Sasa Mwanakijiji unataka baba au dume zima akukaribishe kitu gani?- Si wewe mwenyewe utaanza kumwangalia ki dizaini?

On serious note, unajua kiitikio cha Ahsante mara nyingi kinatokana na mazowea au mtu alipoishi, kukulia au lugha ya pili anayozungumza- Wanaume-Ma brazameni watakujibu, anytime, kwani wanahisi wanasound a bit tough, vile vile wanapojibu powa, au no problem man etc, yote wanahisi ina sound kiume zaidi.

Akina dada wanajibu Karibu, au ahsante kwa kuashiria upole, ukarimu au tuseme utulivu wao (hata kama siyo watulivu in real life)

Pia lugha nyingine ya huwa inachangia sana, kwani wengine huwa wanakwenda kwa direct translation, kama vile you are welcome- karibu nk. Pia nina uhakika shemeji zangu wasukuma (waliokulia kwenye lugha hiyo watakuwa wanajibu wabecha kulumba kwani watakuwa wanatafsiri jibu kutoka lugha ya kusukuma!
 
sasa kabla ya hapo mtu akisema "asante" tulikuwa tunasemaje? was it "asante na wewe"..
 
sasa kabla ya hapo mtu akisema "asante" tulikuwa tunasemaje? was it "asante na wewe"..

Nafikiri ukiambiwa "Asante" unapaswa kujibu "Asante kwa kushukuru",Ikiwa na maana ile ile ya Wabecha kulumba(kisukuma), inaleta maana kidogo kuliko kusema "unakaribishwa" kidogo inakufanya ukodolewe macho haswa neno hilo ikisemwa na lijidume!!!
 
sasa na wale kule Kisangara Juu au Sanya.. tukisema "Havache" jibu lake linakuwaje?

Na wale tunaotoka "Bomba hii, nyumba hii" tunaposema "Usengwile" jibu lake linakuwaje?

Na wa kule kwenye "Malori na Mapijo" tunaposema "Ndaga" jibu sahihi ni "ndaga fijo na lori".. (sijui inatafsiriwa vipi kwa Kiswahili) ..
 
Mkjj, kama nilivyosema, kutokana na kiswahili kuwa na mapungufu yake, ujibuji wa ahsante mara nyingi unategemea background ya huyo anayetakiwa kujibu.

Pia kutona na wengi wetu kujua kiingereza au kufahamu waingereza wanajibu vipi "thank you", ndiyo maana nasi tunajaribu kuwa na jibu la ahsante. Kutokana na influence ya lugha nyingine kwenye kiswahili nadhani siyo rahisi kuwa na na jibu moja, mradi tu yote yakubalike au yawe yanaleta maana fulani ya jibu la ahsante.
 
..mjj,

..inategemea shukrani inatolewa kwa tendo lipi lililofanywa!

..mfano,wa kina dada...mwanaume anaweza kutumia maneno yafuatayo:

...asante nawe!unakaribishwa!asante kwa kushukuru!bila shaka!hamna neno!karibu!karibu sana!karibu tena!nafurahi umeshukuru!n.k!

..kwa ma brotha...mwanaume atasema..poa!hamna noma!shukrani!imetulia!easy!usijali mtu wangu!bila shaka!haisumbui!eeh bwana poa!n.k!
 
Mimi napenda kwanza kukushukuru kwa uchunguzi wako, hali kadhalika kwa kutuletea changamoto hii, ukumbini humu.

Kiswahili kama lugha nyingine yoyote kinakua sambamba na utamaduni wetu unavyokua na kupanuka.

Neno "ahsante" linaashiria kushukuru kwa kuridhika mtu na kile alichofanyiwa. Ni wajibu kwa yule anayeshukuriwa kuitambua shukurani anayopewa kwa kumjibu anayeitoa shukurani hiyo.

Hili la majibu yayotolewa kutokana na jinsia ya mtu, kwangu mimi, halina mtazamo tofauti. Nafikiri tofauti inaletwa na fikra pia mtazamo wa mtu anayeiona hiyo tofauti.

Majibu yote ya "ahsante" uliyoyatoa kama mifano, naona ki-maana, hayana kasoro. Ahsante (kwa) kushukuru, ni kwamba nawe kwa upande wako unampa shukurani kwa kukushukuru.

"Unakaribishwa" au "karibu," unamrahihishia, akiwa na tatizo jingine asisite kukujia kwa msaada.
Uko tayari kumsaidia kwa mara nyingine tena.

"Hakuna/Hamna neno/taabu, Poa(Cool), ni kwamba haikuwa tatizo kwako kumsaidia au kumfanyia ulichomfanyia huyo anayekushukuru.

Yote hayo, kwangu mimi, ni sahihi na sioni sababu ya kimsingi ya kuufanya mwitikio wa "ahsante" uwe wa namna moja tu maalumu au utofautishe jinsia ya anayeshukuru au anayeshukuriwa.
 
Back
Top Bottom