Unampenda lakini hakupendi

Unampenda lakini hakupendi

Habari wana JF,

Umemtumia mtu text lakini hajakujibu, meseji imepokelewa lakini hajajihangaisha kukujibu. Ukaamua kuiweka simu pembeni kuendelea na mambo mengine baadae unarudi bado unaona kimya hajakujibu.

Lakini ukitizama WhatsApp unaona yuko online busy akichati na kubadili DP na status. Unabaki ukijiuliza ana chat na nani mpaka asizione meseji zako na kuzijibu? Unabaki ukiendelea kujiuliza umemkosea nini?

Unaanza kujiambia kuwa labda amekuchoka. Inauma sana kupuuzwa na mtu umpendae kwa moyo wote. Je unajua kuna uwezekano nae anapitia kipindi kigumu kama hicho? Sawa anaweza akakwambia anakupenda au amekumiss, lakini anae mtu mwingine ambae anampenda haswa.

Unavyohangaika kumpigia, kumtumia meseji na asizijibu nae aweza kuwa anafanyiwa hivyo na ampendae. Anamtumia meseji, anamcall lakini nae simu zake hazipokelewi kama wewe. Nao wanapitia magumu kama wewe!

Kufikia hatua hii, unafikiri kukata tamaa juu ya huyo mtu lakini inakuwa sio rahisi. Unafikiri kumuacha huyo mtu, kumblock hata kum "unfriend" Fb lakini bado unaona moyo wako bado unampenda. Na unamatumaini ipo siku atarudi.

Kila muda unapotaka kuichukua simu yako unaomba Mungu ukute meseji yake lakini ukishika tu simu unakuta meseji ya TIGO wakikukumbusha kulipa deni ulilokopa kwa ajili ya muda wa maongezi.

Unajikuta unaichukia simu yako na unamchukia kila mtu anaye kuongelesha, unatamani uipasue simu vipande vipande. Lakini kwanini ifikie hatua hiyo? Kwa hali kama hiyo inaonesha kabisa wewe hupendwi labisa. Kwanini upoteze muda wako kumpenda mtu asiyekupenda?

Usimlazimishe akupende, wewe sio mzee kiasi kwamba huwezi kupata mtu mwingine. Usijipe stress kwa asiyekupenda kuwa na ujasiri wa kumuacha aende na wewe enenda na maisha yako.

Hata iwe vipi maisha lazima yaendelee.
"MWACHE AENDE" kuna uzi upo hapa,utafute tu utapata a lesson
 
Hahaha
Haiwagi that simple shunie , katika vitu niliwahi kujifunza ila kwa taabu ni hiyo kitu
Mtu yaan unampenda mpaka unahisi umerogwa, halafu ukimuangalia yuko na wewe kwa sababu flani tuu, ila yuko disgusted yaan kuwa na wewe
Shidaaaaa!!
inategemea na mtu na mtu nishapitia mm hizo situation
 
inategemea na mtu na mtu nishapitia mm hizo situation
Ujue kwa nyie kina dada najua inakuwa ina pain, ila iwa mwanaume ina pain halafu inakushangaza, yaan unakuwa unajilaum, unajiona kuna kitu umekosea mwanaume mzina uta tendewaje hivo!!! hahaha

To women its painful
To men its painful and awkward
 
209142.jpg

Hicho kifaa huwa tunapenda kukitumia sana kwenye nyumba zetu lakini huwa tunasahau kukitumia kwenye mioyo/nafsi yetu...futa delete kabisa!

Utashangaa unavyo-move on very fast.
 
Yaani mkuu hicho ndio kinachoendelea kwangu na binti flani hivi ????? Huwezi amini nikimwambia i miss u? au a love u? atakaa aidha nusu saa ndio anijibu au hata asiwasiliane na mm kwa mda . sometimes yupo online either fb au whatsapp na asini cheki? Inaniuma ila na jipya moyo mybe someday to come i might let her go.... Najipaga moyo tu
 
Anae wa kuwa nae busy we utabaki kua spaire jipe moyomoyo hivyohvyo siku atakwambia hakutaki wala huendani nae tafta mwanamke mwingine
 
Yaani mkuu hicho ndio kinachoendelea kwangu na binti flani hivi ????? Huwezi amini nikimwambia i miss u? au a love u? atakaa aidha nusu saa ndio anijibu au hata asiwasiliane na mm kwa mda . sometimes yupo online either fb au whatsapp na asini cheki? Inaniuma ila na jipya moyo mybe someday to come i might let her go.... Najipaga moyo tu
Hapa ndo huwa tunakosea. Why unajipa matumain kwenye sehem ambayo indicators zooote zinaonesha HAKUNA MAPENZ?Yaani unaamini kuwa iko siku atakupenda?KWELI?Mdau me nakushaur "MWACHE AENDE"
 
Hapa ndo huwa tunakosea. Why unajipa matumain kwenye sehem ambayo indicators zooote zinaonesha HAKUNA MAPENZ?Yaani unaamini kuwa iko siku atakupenda?KWELI?Mdau me nakushaur "MWACHE AENDE"
Mungu anisaidie tu km nipo kifungoni mwa huyu dada
 
Yaani mkuu hicho ndio kinachoendelea kwangu na binti flani hivi ????? Huwezi amini nikimwambia i miss u? au a love u? atakaa aidha nusu saa ndio anijibu au hata asiwasiliane na mm kwa mda . sometimes yupo online either fb au whatsapp na asini cheki? Inaniuma ila na jipya moyo mybe someday to come i might let her go.... Najipaga moyo tu
Ha ha nacheka kwa huzun kumbe wahanga tupo wengi..moyo machine
 
Wanaokutana na vinuka mkojo vya college haya ya kufikia tu taka usitake.
 
Back
Top Bottom