Unampenda lakini hakupendi

Unampenda lakini hakupendi

Mi wakwangu huwaga simuelewi kabisa. Yaan kuna kipindi anakuwa vizur.. lakin uchum ukidorora tu.. vituko.. kejeli.. ananijibu hovyo.. haan full vituko. nikilipeleka kwa ndugu zake.. wanasema bado mtoto nimvumilie. nikilia buyu kama wiki.. anakuwa mnyenyekevu.. nikirudisha mapenz dharau zinaanza. Mpaka leo nimeshindwa kumuelewa
Mkuu, life is too short to waste my precious emotions on someone who doesn't appreciate. Piga chini, wewe sio shule ya kujifunzia kupenda, aende kwingine akajifunze, akigraduate ataenda kwa mwingine, kwako atakuja aliekwishafunzwa na mwingine.
 
Habari wana JF,

Umemtumia mtu text lakini hajakujibu, meseji imepokelewa lakini hajajihangaisha kukujibu. Ukaamua kuiweka simu pembeni kuendelea na mambo mengine baadae unarudi bado unaona kimya hajakujibu.

Lakini ukitizama WhatsApp unaona yuko online busy akichati na kubadili DP na status. Unabaki ukijiuliza ana chat na nani mpaka asizione meseji zako na kuzijibu? Unabaki ukiendelea kujiuliza umemkosea nini?

Unaanza kujiambia kuwa labda amekuchoka. Inauma sana kupuuzwa na mtu umpendae kwa moyo wote. Je unajua kuna uwezekano nae anapitia kipindi kigumu kama hicho? Sawa anaweza akakwambia anakupenda au amekumiss, lakini anae mtu mwingine ambae anampenda haswa.

Unavyohangaika kumpigia, kumtumia meseji na asizijibu nae aweza kuwa anafanyiwa hivyo na ampendae. Anamtumia meseji, anamcall lakini nae simu zake hazipokelewi kama wewe. Nao wanapitia magumu kama wewe!

Kufikia hatua hii, unafikiri kukata tamaa juu ya huyo mtu lakini inakuwa sio rahisi. Unafikiri kumuacha huyo mtu, kumblock hata kum "unfriend" Fb lakini bado unaona moyo wako bado unampenda. Na unamatumaini ipo siku atarudi.

Kila muda unapotaka kuichukua simu yako unaomba Mungu ukute meseji yake lakini ukishika tu simu unakuta meseji ya TIGO wakikukumbusha kulipa deni ulilokopa kwa ajili ya muda wa maongezi.

Unajikuta unaichukia simu yako na unamchukia kila mtu anaye kuongelesha, unatamani uipasue simu vipande vipande. Lakini kwanini ifikie hatua hiyo? Kwa hali kama hiyo inaonesha kabisa wewe hupendwi labisa. Kwanini upoteze muda wako kumpenda mtu asiyekupenda?

Usimlazimishe akupende, wewe sio mzee kiasi kwamba huwezi kupata mtu mwingine. Usijipe stress kwa asiyekupenda kuwa na ujasiri wa kumuacha aende na wewe enenda na maisha yako.

Hata iwe vipi maisha lazima yaendelee.
Kipi ni bora ...umwambie nenda zako au uuchune?
 
Mmmh naona kma umenizungumzia Mimi mkuu sio siri na ujumbe wako umeniingia kiasi kwamba umenihamasisha na najiona mshindi katika hii vita ngumu ya nafsi

Hapa naona ujumbe huu umegusa wengi..ni ngumu kuumeza japo unaumiza
 
aniwaze ashindwe hata kula, atume sms. nikicheleea kujibu aumie skiona sms yoyotr ajue ni mm kumbe ni vida eanakumbudhia deni la nipige tafu loh nitampendaga milele
Basi uko tofauti, wenzio sijui wanakinai kupendwa? Unafanyiwa visa mpaka unakaa chini unajiuliza, hivi najipendekeza ili iweje? Nikimuacha nitakufa? Unaamua kubadilika

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom