Unampenda lakini hakupendi

Unampenda lakini hakupendi

Mimi siwezi kuumizwa na mwanamke kiasi hicho, there are so many fishes in the ocean. Kama hakupendi achana naye
 
Hela natoa haswa na sio chini ya elfu 70000 kwa wiki hiyo ni yakumtoa kwenye vishawishi na hapo dada yangu she as not telling me if she needs some amount of money what if she tells me imagine of that? Nikaona hilo sio tatizo navyo chat hapa ss nilikuwa nampango nimfungulie kitega uchumi chochote ifikapo mwakani sio chini ya 5M ila ndio hivyo aleti ushirikiano wowote nami for sure mm binafsi si mwelewi adi ss naninatamani hawe future yangu na sio kupitapita japa mda unanirusu sanaa tu kula ujana ila naamini as Gentleman hupaswi kurukaruka km njiwa. Nikitaka kuvhat nae haitapita dak5 ameshatoa sababu ya kufanya kitu kingine ile chatting moment inapotezewa tu hivyo ooooooh, sipendagi kuchat na simu na au kutokatoka.
Aisee watu wanachezeaga hz bahat arrgh! wengine tunazitafuta
 
Hii kitu imenisaidia sana. Unakuta mtu sio kwamba anatisha sana au vipi lakini basi unajisikia kuwa connected nae sana. Ukimwona unatamani umwangalie, unapenda alivyo, pozi zake,upole wake na anavyoongea n.k Sasa unapoamua kukiri hisia zako kwake na akajua unavyompenda, hayo mashauzi sasa! Mpaka vile vigezo vilivyokufanya uvutiwe nae mwanzoni, vinakuwa havina maana tena maana unaanza kumwona yuko tofauti na ulivyomchukulia.
Upande wa pili, Ukiachana na swala la kuvutiwa na tabia, hata akiwa mzuri sana, yale manyanyaso unayokutana nayo, yanakufanya umwone kama takataka ya jalalani kabisa. Maana ni kama ana enjoy kukufanyia vituko au hathamini ubinadamu ulionao, ukilalamika wenzie watamtetea kuwa anakupima aone tabia yako. Wengine watakwambia, huyo hakupendi ndio maana anakufanyia hayo. Cha ajabu hakwambii kuwa hakutaki ili uendelee na mambo yako, bali anaendelea kukuzinguazingua huku ukibakia bila ufahamu wa status yako ya kimahusiano. Sasa mtu kama huyo unamfuga wa nini?:
Kuna mwingine, unakuwa nae katika relationship baada ya kumfukuzia sana. Ukiangalia, alikusumbua mno, mkianza mahusiano unatarajia atabadilika na kushow some maturity,lakini inakuwa kinyume chake. Ni kama wewe ni baba na yeye ni mtoto wa mwisho. Utaonyeshwa deko, visa plus vituko kila anapojisikia. Ndio hayo ya kutokujibu sms, kutopokea simu na kutoeleweka anataka nini katika uhusiano maana huwezi kuelewa anataka muachane au uhusiano uendelee.
Sasa, unadumu vipi katika uhusiano na mtu wa hivyo? Huwa najitahidi kuwa mjinga ila mara zote nakwama kabisa aisee.
Wakati nikiwa bado mshamba wa mapenzi, kulikuwa na kabinti nilikapenda ambako kalikuwa kakiishi mtaa niliokuwa nikiishi.
Sio siri, yule binti alikuwa mzuri sana isipokuwa alitokea tu kwenye familia yenye maisha ya kawaida sana.
Basi, kwa akili zangu, nikawa napanga mengi sana juu ya yule binti kama uhusiano wa kudumu,ndoa n.k Nilipoona umefika muda mwafaka, nikaona nijitose. Nachojipendea mimi ni kuwa, sijawahi kushindwa kujieleza kwa mwanamke toka nikiwa bado mdogo sana kiumri na kuna wakati wazazi wangu walipokuwa wakizikamata barua zangu za mapenzi na wakiangalia umri wangu, walikuwa hawaamini kama naweza kuandika matured stuff kiasi kile.
Tukirudi kwenye stori. Nikamvaa dada na kutiririka yote bila kumficha na niliona kanielewa sana. Nikatarajia tu nitajibiwa moja kwa moja kuwa nimekubaliwa au sijakubaliwa hata kwa sms tu. Hilo sikuliona. Nikituma sms, inajibiwa kwa mkato tu. Siku akikuuliza yeye kwa text, uko wapi? Kinachofuata ni matatizo tu, mama mkubwa anaumwa, shangazi ameniambia nimfuate Arusha kuna hili na lile. Mara nina wageni, nitumie hela ya Taxi iwalete nyumbani.
Mpaka hapo sijui mimi ni nani kwake. Nikawa mpole sana na kumvuta kwa ukaribu na kwa kiasi fulani nilifanikiwa ila baadae nikagundua mwenzangu hayuko kimahaba zaidi na amewekeza zaidi katika misaada yaani ananifanya mimi kama side kick fulani hivi. Nikaamua kupunguza misaada. Hapo ndipo nilipouona moto. Ndio ikawa nikipiga simu sijui ndio haiangaliwi kabisa? Nikitext najibiwa baada ya siku mbili.
Nikaona huu ni ujinga na kuamua kukaa kimya pia, nikafuta namba zake. Kipindi hicho picha tunatumiana kwa email, na yenyewe nikaifuta. Alipoona changes, nikaona anaanza kujirudirudi,but it was too late. Nilishamtambua yeye ni mtu wa aima gani na sikuwa na hamu nae tena. Baadae Dada yake akaja kunieleza kwa kirefu kuwa alikuwa na mwanaume wake Oman, hakuzoea kudate na wabongo. Nikasema Pambafff, arudi huko basi!
Braza the same to me... but yangu.. ni komesha mpaka sijui status yangu ni nini
 
Hii kitu imekuja wakati muafaka kwangu, asante mtoa mada, nimepata Amani ya roho, baada ya kusoma hii mada nmedelete kabisa namba na msg zote, how comes unaandika msg 10, unajibiwa moja, tena jibu lenyewe unaambiwa "poa" hata kama ni swali linahitaji explanation,,,, halafu dada anaekusumbua hata ajaanza kutengeneza future ya maisha yake,,,,,delete futa kabisa,,,
 
Hela natoa haswa na sio chini ya elfu 70000 kwa wiki hiyo ni yakumtoa kwenye vishawishi na hapo dada yangu she as not telling me if she needs some amount of money what if she tells me imagine of that? Nikaona hilo sio tatizo navyo chat hapa ss nilikuwa nampango nimfungulie kitega uchumi chochote ifikapo mwakani sio chini ya 5M ila ndio hivyo aleti ushirikiano wowote nami for sure mm binafsi si mwelewi adi ss naninatamani hawe future yangu na sio kupitapita japa mda unanirusu sanaa tu kula ujana ila naamini as Gentleman hupaswi kurukaruka km njiwa. Nikitaka kuvhat nae haitapita dak5 ameshatoa sababu ya kufanya kitu kingine ile chatting moment inapotezewa tu hivyo ooooooh, sipendagi kuchat na simu na au kutokatoka.
Futa namba yake na mawasiliano yake na kuwa busy kutafuta mafanikio ya kimaisha.
Mwenyewe nikiwahi ingia kichwa kichwa I know maumivu niliyopara.
 
Habari wana JF,

Umemtumia mtu text lakini hajakujibu, meseji imepokelewa lakini hajajihangaisha kukujibu. Ukaamua kuiweka simu pembeni kuendelea na mambo mengine baadae unarudi bado unaona kimya hajakujibu.

Lakini ukitizama WhatsApp unaona yuko online busy akichati na kubadili DP na status. Unabaki ukijiuliza ana chat na nani mpaka asizione meseji zako na kuzijibu? Unabaki ukiendelea kujiuliza umemkosea nini?

Unaanza kujiambia kuwa labda amekuchoka. Inauma sana kupuuzwa na mtu umpendae kwa moyo wote. Je unajua kuna uwezekano nae anapitia kipindi kigumu kama hicho? Sawa anaweza akakwambia anakupenda au amekumiss, lakini anae mtu mwingine ambae anampenda haswa.

Unavyohangaika kumpigia, kumtumia meseji na asizijibu nae aweza kuwa anafanyiwa hivyo na ampendae. Anamtumia meseji, anamcall lakini nae simu zake hazipokelewi kama wewe. Nao wanapitia magumu kama wewe!

Kufikia hatua hii, unafikiri kukata tamaa juu ya huyo mtu lakini inakuwa sio rahisi. Unafikiri kumuacha huyo mtu, kumblock hata kum "unfriend" Fb lakini bado unaona moyo wako bado unampenda. Na unamatumaini ipo siku atarudi.

Kila muda unapotaka kuichukua simu yako unaomba Mungu ukute meseji yake lakini ukishika tu simu unakuta meseji ya TIGO wakikukumbusha kulipa deni ulilokopa kwa ajili ya muda wa maongezi.

Unajikuta unaichukia simu yako na unamchukia kila mtu anaye kuongelesha, unatamani uipasue simu vipande vipande. Lakini kwanini ifikie hatua hiyo? Kwa hali kama hiyo inaonesha kabisa wewe hupendwi labisa. Kwanini upoteze muda wako kumpenda mtu asiyekupenda?

Usimlazimishe akupende, wewe sio mzee kiasi kwamba huwezi kupata mtu mwingine. Usijipe stress kwa asiyekupenda kuwa na ujasiri wa kumuacha aende na wewe enenda na maisha yako.

Hata iwe vipi maisha lazima yaendelee.
Yamekukuta nin Mkuu. Yaani unampenda mtu unaumia kuona hatii hisia zako. Alafu yeye anakufanya poyoyo
 
Bora anaeonesha mbashara (live) kuwa hakupendi . Utaumia kwa muda tu, lakini mtu anajifanya anakupendaaa kumbe ukiondoka tu anakung'ong'a huyo ni hatari na wako wengiii kwa sasa!!! Yeye anakuwa tu anahitaji kitu flani moyoni wala hakupendi!
Na ndio maana ndoa nyingi za sasa zinasumbua.
 
Hii kitu imekuja wakati muafaka kwangu, asante mtoa mada, nimepata Amani ya roho, baada ya kusoma hii mada nmedelete kabisa namba na msg zote, how comes unaandika msg 10, unajibiwa moja, tena jibu lenyewe unaambiwa "poa" hata kama ni swali linahitaji explanation,,,, halafu dada anaekusumbua hata ajaanza kutengeneza future ya maisha yake,,,,,delete futa kabisa,,,
Ina maana ulikuwa hujui? Ukae unaumia roho wakati kuna wengi tu wanarandaranda wakitaka kampani? Kufanya maamuzi mazito ni jambo linalosaidia sana.
 
Bora anaeonesha mbashara (live) kuwa hakupendi . Utaumia kwa muda tu, lakini mtu anajifanya anakupendaaa kumbe ukiondoka tu anakung'ong'a huyo ni hatari na wako wengiii kwa sasa!!! Yeye anakuwa tu anahitaji kitu flani moyoni wala hakupendi!
Na ndio maana ndoa nyingi za sasa zinasumbua.
Ukiona meseji au simu imeanza na Baby uko wapi? Nimekumic sana, tunaweza kuonana? Unajua tu kuwa ana shida ya pesa na kilichokumbukwa ni wallet yako.
 
Ukiona meseji au simu imeanza na Baby uko wapi? Nimekumic sana, tunaweza kuonana? Unajua tu kuwa ana shida ya pesa na kilichokumbukwa ni wallet yako.
Mi wakwangu huwaga simuelewi kabisa. Yaan kuna kipindi anakuwa vizur.. lakin uchum ukidorora tu.. vituko.. kejeli.. ananijibu hovyo.. haan full vituko. nikilipeleka kwa ndugu zake.. wanasema bado mtoto nimvumilie. nikilia buyu kama wiki.. anakuwa mnyenyekevu.. nikirudisha mapenz dharau zinaanza. Mpaka leo nimeshindwa kumuelewa
 
Back
Top Bottom