Uzi kwa ajili ya mtu uliyempenda na bado unampenda lakini aliondoka ghafla katika ukaribu wenu

V Chief

Member
Aug 20, 2023
69
130
Habari wanaJF,
Naamini kwa idadi kubwa ya watu wa humu, kunaye mtu uliyewahi kumpenda na pia bado unampenda lakini kuna mambo yalitokea hadi hivi sasa haupo karibu nae au haupo nae katika mahusiano.
Je, unamkumbuka ni nani na kilitokea nini hadi hali kama hiyo ikatokea ilhali bado unampenda?
Karibuni kwenye uzi kwa visa vyenu murua.
 
Nilimpenda Mary Cheusi wangu halafu akaja kunifumania na mdogo wake tunazagamuana. Mpaka leo nampenda, lakini hataki kunisamehe miaka 25 mbele.
 
Habari wanaJF,
Naamini kwa idadi kubwa ya watu wa humu, kunaye mtu uliyewahi kumpenda na pia bado unampenda lakini kuna mambo yalitokea hadi hivi sasa haupo karibu nae au haupo nae katika mahusiano.
Je, unamkumbuka ni nani na kilitokea nini hadi hali kama hiyo ikatokea ilhali bado unampenda?
Karibuni kwenye uzi kwa visa vyenu murua.
Move on bro, hayo mawazao yatakufanye uishi kwenye pas si future tena
 
Nikiwa kwenye mafunzo kwa Vitendo hospital moja mkoa ule wa watoto wazuri, katikati ya nchi,,,, nilikutana na mwanadada mmoja(tumwite mama F, herufi ya jina la mtoto wake), alikuwa mwajiriwa wa serikali amekuja kua-upgrade kwa mwaka mmoja, na ni single mother, ni mzuri mpaka huwa najiuliza yule afande( magereza) alipata wapi ujasiri wa kumzalisha na kumuacha mtoto mzuri kama yule, mapenzi yakakolea kama miezi mitatu hivi, nikamaliza utarajari kurudi mtaa kazi hamna akili haiko sawa….nikaanza kumkwepa mama F baada ya muda tukapotezeana…mpaka akamaliza masomo na mimi nikasepa zangu mkoa ule, hatukuwa na mawasiliano tena,,,
Kama utasoma kumbuka.
kwa kweli mama F nilikupenda kweli na nilikuwa tayari kukuweka ndani nikupende wewe na mtoto wako,,,, ila ndio hivo kibarua kilichelewa na nikaona na wewe unahisi mimi ni wale wale.
 
Mama na wanangu itakuwaje?
Hakuna KIUMBE CHOCHOTE kinachopaswa kuvuka kiasi cha upendo ulionao juu yako wewe mwenyewe.

Dunia ya leo usistaajabu mama yako akawa ndio mtengeneza sumu itakayokuua na watoto wako wakakutelekeza pale wanapomaliza haja na wewe.

Sisemi kuwa uwachukie, lakini usipende kupitiliza kiasi kwamba wakikuumiza ujikute unaumia kwa kupitiliza. Katika kila upendo weka akiba ya chuki. Inawezekana usielewe mpaka yakukute na nakuombea Mungu yasikukute.
 
itakuwa umepigwa tukio na familia yako wewe, sio bure:D:D:D:D:D:D
 
Back
Top Bottom