Unamfahamu DCI Manumba wewe?

Unamfahamu DCI Manumba wewe?

Wahenga wanasema
Maneno ya watu wengi ni maneno ya mungu
Ya kwangu mimi namuombea mwenyezi mungu ampunguzie mzigo wa maradhi na awe mtu mwema
 
ila ni vizuri kumuua mwenzio?maana polisi wanaua sana jamani
DCI MANUMBA pale Mwanza kwenye msiba wa RPC BARLOW, aliapa.."Jeshi la Polisi litalipa Kisasi kwa wauaji wote pasipo kuacha hata mmoja"....na MUNGU si Kinjekitile, leo yeye ndo yuko DHOFLI hali...anyway, MUNGU amnusuru aungane tena na MKEWE na WATOTO wake...
 
hapa tunachemka kusema wamemnaniii
kuna uchawi wa kumpa mtu malaria vidudu 500?
hapana bwana huu ni ugonjwa wa malaria athari zake ndio hizo
vidudu vyote hivo kwenye damu afu mtu awe mzima?
apone aje ajibu maswali yetu ya kukalia riporti muhimu za ufisaid na mauaji.
 
kamanda Barlow alivyouliwa kwenye maswala yake ya uzinzi huyu Manumba alikimbilia mwanza kuwasaka wahusika kwa vitisho vikali ila hapo musoma watu zaidi ya 20 wamekatwa vichwa kama kuku ila huyu Manumba hajaonyesha reaction yeyote kama aliyoionyesha kwa mzinzi Barlow.
 
Aga Khan = MNH?? kweli hawa viongozi wetu wamepotoka! au wanaogopa kivuli chao wenyewe? usimuombea mwanzako afe! akipona sasa hivi atakuwa mtu mwingine safi! atajua kwamba ipo siku!
 
Usamehewe makosa yako kwa HURUMA YAKE MUUMBA WETU, akupumzishe kwa amani, AMEN!
 
Manumba hafi, wala msifurahi, manumba atapona na ataokoka aishi ili asimulie maajabu ya Mungu,kesho atatoka Hospitali kwa jina la Yesu. kwa sababu yeye alikuja kwa wenye dhambi ili wawe huru na dhambi. mtashangaa na roho zenu mbaya.
 
Ungekuwa Doct. Ulimboka ungemwombea nini HEMEDI MSANGI?
 
Kwa vitendo viovu vya polisi kama uuaji, utekaji, na ukandamizaji wa haki za raia, mimi sina hamu nao hata kidogo. Polisi wa Tanzania wapo kwa maslahi ya watawala tu, siyo raia.
 
Manumba sasa utafahamu umuhimu wa Dr. ulimboka na walichokuwa wanakigomea. Ubora wa vifaa tiba, Mazingira ya kazi n.k. Sasa uhai wako uko mikononi mwao, wanaweza kuamua lolote.

Napenda upate afya njema ili uje kuwashukuru madaktari hadharani kwa kupigania uhai wako.
 
Aga Khan = MNH?? kweli hawa viongozi wetu wamepotoka! au wanaogopa kivuli chao wenyewe? usimuombea mwanzako afe! akipona sasa hivi atakuwa mtu mwingine safi! atajua kwamba ipo siku!
Jasiri haachi asili!
 
Duh! Kwakweli taifa lilipo fikia ni pabaya sana, yani mpaka tuna ombeana kufa? Duh! Hiikali, hebu pata pc angekua ni babaako hata kama angekua muuaji kiasi gani usinge furahi na post hii. Tuache maskhara kwenye mambo ya kweli

ndio ujue jinsi gani polisi walivyo kero Tanzania!
 
pamoja na yote mtu asiye na uchungu na binadamu wenzange hakika naye hatoonewa huruma ivo woooote wafe tu tena hata angekuwa baba angu kama haumii roho za wengine zinapo angamia bila hatia nayeye afe tu hata kama ni mama yako akiwa hana uchungu na roho ya binadamu wengine haina maana ya kumuonea huruma na yeye afe tu tena mapema kabisa kumbuka kila binadamu ni nduguyo ndio mana ukipatwa na tatizo hata kama nduguzo hawapo waliopo karibu nawe watakupa msaada kama nduguzo so yabid kuwa na uchungu na kila roho inayo jaali roho za wengine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom