john achila mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 141
- 280
Mwajiri Mwenye Mshahara wa Mauti ni Yupi
Mwajiri mwenye mshahara wa mauti ni yupi
Hebu tafakari kuwa umeajiriwa, halafu aliyekuajiri anakutumikisha kwa mateso makali, na mwisho wa siku anakulipa mshahara wa kifo. Je, kabla ya kuanza hiyo kazi, utakubali kusaini mkataba wa kazi? Bila shaka mtu mwenye akili timamu, hawezi kukukubali kusaini mkataba.
Ajabu ni kwamba watu wengi wametia sahihi na huyu mwajiri, ambaye anawatumikisha halafu anawalipa mshahara wa kifo. Je unamfahamu huyu mwajiri mkatili, na tena mwenye mshahara mbaya wa kifo?
Biblia imemtaja mwajiri huyu ni nani katika Yohana 8:34, na mshahara wake ni upi katika Warumi 6:23.
Yohana 8:34 “Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi”.
Mtu anayetenda dhambi, mwajiri wake ni dhambi. Dhambi ni mwajiri mbaya asiye na huruma, na huu ndio mshahara wake: Warumi 6:23: “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti….”.
Mwajiri huyu hamdhulumu mtu. Humlipa mtu mshahara wake, tena kwa wakati. Kwa sababu kila anayefanya kazi anastahili malipo.
Biblia inasema hivyo katika Luka 10:7:
"Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii".
Biblia inasema hivyo pia katika 1Timotheo 5:18: "Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake".
Dhambi inaua
Dhambi inaua mambo gani?
1. Dhambi inaua upendo uliopo ndani yako.
2. Yale mahusiano uliyoyaanza na Mungu wako, dhambi inayaua, inakusababisha kabisa usioune uso wa Mungu.
3. Dhambi inaua furaha ndogo na kubwa uliyonayo.
4. Dhambi inaua amani na kuleta hofu.
5. Dhambi inaua wema mtu alionao.
6. Dhambi inaua ndoa.
7. Dhambi inaua huduma/karama/kipawa.
8. Dhambi inaua heri za mtu.
9. Dhambi inaondoa baraka za mtu
10. Dhambi inaua mwili.
Huyu ni mwajiri asiyefaa, mwenye mkataba mbovu. Tumkimbie na kumwendea Bwana Yesu, ambaye yeye anasema Nira yake ni laini na mzigo wake ni mwepesi, nasi tutapata raha nafsini mwetu (Mathayo 11:28).
Tukimkimbilia Bwana Yesu, anatufungua kutoka kwa huyu mwajiri mbaya (dhambi) na kutuweka huru.
Bwana Yesu anatulipa UZIMA badala ya KIFO, na si uzima tu, bali uzima wa milele.
Anaongeza uzima juu ya upendo wa mtu, lakini dhambi inaua.
Bwana Yesu anaongeza uzima juu ya amani ya mtu, lakini dhambi inaua.
Bwana Yesu anaongeza uzima juu ndoa ya mtu na maisha kwa ujumla, lakini dhambi inaua.
Na zaidi ya yote, Bwana Yesu anamlipa mtu UZIMA WA MILELE.
Kwa nini tusimchague Yesu?
Warumi 6:23 inasema: “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu”.
Uko tayari? Kwa nini dhambi ikukaushie uzima wako wa hapa duniani na ule wa milele ujao?
Matunda ya dhambi ni yale yote yaliyotajwa katika Wagalatia 5:19-20.
19 "Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi".
Hatuwezi kukubali kusaini mkataba na kampuni yenye mshahara wa kifo, hata kama kampuni ni kubwa kiasi gani.
VIVYO HIVYO, TUMKATAE MWAJIRI MWENYE MSHAHARA WA MAUTI. TUKATAE KUTENDA DHAMBI. DHAMBI NDIYE MWAJIRI MWENYE MSHAHARA WA MAUTI.
Kwa vile hatujui siku wala saa, wakati ni sasa, mkaribishe Yesu maishani mwako, akuweke huru.