Unakumbuka wanyonya damu mashuleni?

Unakumbuka wanyonya damu mashuleni?

ilikuwaje maana hii insu ilikuwa nchi nzima, then kila mkoa lazima awepo mtu anayeogopewa kwamba ni mumian, nakumbuka pale mji kasoro bahari walikuwepo wale wagiriki, wakitokeza na 109 zao kama za bushman hakuna atakayebakia
 
Dah niko hoi kwa kucheka..unanikumbusha mbali watu walivyokuwa wanakimbizwa mabwawa saba..haaa beach kidimbwi lol jamani tumetoka mbali..

Mitaa hiyo tulikuwa hatukatizi tukija kuokota maembe chuo kikuu hahaha.
 
Rest in Peace my "fiancee“ wa kitoto toto....Mary Abonike,nikikumbuka haya mambo ya chinjachinja sijui nyonya damu namkumbuka sana Mary wangu,1991 tukiwa Mwadui “A“ Primary School,tunapita pembezeni mwa barabara ya boidi,mara mwanafunzi mmoja akatushitua kuwa mnyonya damu wa kijiji cha Utemini anakuja...katika harakati za kukimbia tukajichomeka kwenye barabar...Gari aina ya Peugot ukatupitia...nilivunjika mkono na mguu...lakini mwenzangu Mary alifia Hospitali ya Misheni pale Mipa...
Alikuwa jirani na "mchumba" wangu wa kombolela na mchezo wa chekecha...darasani hadi kanisani pamoja..tukapewa kipaimara na Askofu Castor Sekwa(R.I.P) Parokia ya Msalaba Mtakatifu-Mwadui...sijawahi kumsahau wala kulisahau tukio la kumkimbia Mnyonya damu...picha za kipaimara na mazishi ninazo...hunipa kumbukumbu ya rafiki wa utotoni niliompoteza kwa vitisho ambavyo leo nakuja kujua havikuwepo....R.I.P MARY ABONIKE

Pole sana mkuu, ingawa tangia mwanzo wa hii thread nacheka sina mbavu lakini baada ya kufika hapa simanzi imenijaa. Sikujua kama kuna wengine iliwapelekea hadi vifo na wengine kuumia vibaya. R.I.P Marry
 
Rest in Peace my "fiancee“ wa kitoto toto....Mary Abonike,nikikumbuka haya mambo ya chinjachinja sijui nyonya damu namkumbuka sana Mary wangu,1991 tukiwa Mwadui “A“ Primary School,tunapita pembezeni mwa barabara ya boidi,mara mwanafunzi mmoja akatushitua kuwa mnyonya damu wa kijiji cha Utemini anakuja...katika harakati za kukimbia tukajichomeka kwenye barabar...Gari aina ya Peugot ukatupitia...nilivunjika mkono na mguu...lakini mwenzangu Mary alifia Hospitali ya Misheni pale Mipa...
Alikuwa jirani na "mchumba" wangu wa kombolela na mchezo wa chekecha...darasani hadi kanisani pamoja..tukapewa kipaimara na Askofu Castor Sekwa(R.I.P) Parokia ya Msalaba Mtakatifu-Mwadui...sijawahi kumsahau wala kulisahau tukio la kumkimbia Mnyonya damu...picha za kipaimara na mazishi ninazo...hunipa kumbukumbu ya rafiki wa utotoni niliompoteza kwa vitisho ambavyo leo nakuja kujua havikuwepo....R.I.P MARY ABONIKE

pole sana kwa yaliyowapata. Mi nashangaa serikari ilikuwa wapi kukanusha huo uvumi
 
Umenikumbusha mbali sana. Huku kwetu Tanga tulikuwa tunawaita mumiani hao na jina la Msekwa ambaye ni mwanamke lilivuma sana enzi hizo
 
Hivi siku hizi hawapo? Nakumbuka mtu akisimama na nyie mnakaa mnamwambia "kaa, unatunyonya damu".
Hivi jamani hili suala ni nani alikuwa analianzisha ?maana katika miaka yangu yote 7 ya primary school sijawahi kuwashuhudia though story zilikuwa haziishi..siku nyingine tunanusurika na kuumia kisa mmoja kalianzisha kaona wanyonya damu.je ni kweli walikuwepo ama ilikuwa ni imani tu
 
Hahahaaaa.....Ware wa kure kwetu enzi za primary, ilikuwa inasemekana kuwa kuna watu wanaiba watoto na kwenda kutoa KAFARA migodin...

Enzi hizo alivuma mzee mmoja kwa jina MALEMBERA ambaye alikuwa anamiliki mashimo kadhaa ya Dhahabu NYAMONGO, Sasa wakawa wanasema huyo mzee alikuwa akipiga hizo issue....Basi mtoto ukitishiwa tu... "Malembera huyo yuaja...mbiooooooo, au hata kama kuna kitu umezuiwa kufanya hutofanya ukihofia utapelekwa kwa huyo Mzee.....

Aione: Think pad, Mwita Maranya na platozoom...

charminglady kumbe unamkumbuka Malembera? huyu kiumbe alikuwa tishio sana kwa watoto na wazazi kwa miaka ile.

Ila sasahivi amechoka ile mbaya nadhani katika watu wanaoilaani barrick gold basi huyu malembera atakuwa anaongoza kwakuwa kama si ujio wao hawa wawekezaji sasahivi malembera angekuwa ndiye bilionea wa Nyamongo na Tarime kwa ujumla.

Hatahivyo alikuwa na jeuri sana huyo Malembera alikuwa akichezea pesa kama makaratasi. Kweli pesa ni mwanaharamu sasahivi hana kitu amepigika hadi anatia huruma.
 
Last edited by a moderator:
Malembera alivuma si kidogo, nasikia kwenye harusi yeye alikuwa wa mwisho kutaja zawadi kwa Wanaharusi, ilikuwa balaa. Kuna wakati aliweka rekodi ya mtu aliyeuza dhahabu nyingi kwa NBC Bank.

Ila hivi sasa nasikia yuko hoi kifedha!!

Yeah.... Kachoka mbaya ndugu yangu, si unajua pesa za machimboni!!!!

Mwita Maranya enzi hizo anaoa wanawake kama mchezo ... Dah pesa hizi kweli mwana haramu!!!!
 
Last edited by a moderator:
ilikuwa mwaka .1994 nipo la tano mwalimu mkuu alienda mjini hukunyuma ikazuka kaenda kuchukua wanyonya damu wee shuleni hapakutosha!
 
But bado swali langu kwaniini walimu walikuwa hawakanushi?au maredioni hawatangazi kwamba Serikali imetoa tamko?yaani sijui tulikuwaje
 
Umeona ee!
Mie yule mlinzi babu wa pale Tahfif alikuwa ananikeraga na mikwara bubu yake.
Cathedral Book Shop pale.
Nakumbuka siku moja wakati wa mapumziko tulienda pale TTCL kuchezea lifti, tusikwame nini, tulilia...ilibidi mwl mkuu Fadhil aje kututambua kama sisi ni wnfnz wake baada ya kunasuliwa.
Tulipofika skuli tukaambiwa tunaitiwa nyonya damu ili watunyonye...mama weee...nilivyomponyoka mwl ni mbio mpaka ofsn kwa dad (r.i.p).
Jamani utoto...hasa wa kimjini, raha sana.

Aisee kumbe we mtata tangu utoto yani orijinaly mpk ofice za ttcl@ Madame B....mlikua darasa la ngapi hapo...tahfif kuna watu walikua wanaibaga sometimes achaaa
 
Kinondoni?

class letu lilikuwa halina madirisha ya nyavu wala hakuna frem..ni kama boma, basi ukisikia tu 'manyonya' unachomoka ktk uwazi wa dirisha home hapo hadi kesho....... kimsingi sijawahi kuwaona ila nimekimbia mara nyingi
 
Aisee kumbe we mtata tangu utoto yani orijinaly mpk ofice za ttcl@ Madame B....mlikua darasa la ngapi hapo...tahfif kuna watu walikua wanaibaga sometimes achaaa

Yani we acha tu.
Nilikuwa mtata mwisho.
TTCL mama alikuwa anafanya kazi, basi nakwambia twachukuana haooo...
Ni panda shuka...panda shuka.
Hapo niko drs la 3.
Tukitoka hapo twaenda Snow Cream.
Dereva wa home akitufata ye ndio akatuchukulie mabegi ya Dino shule,unayakumbuka?
Tahfif tumedokoa sana vipenseli, viufutio...
 
Vipi zile za kukuta kichwa cha mbuzi chooni? Dah mambo ya long bwana
 
Mitaa hiyo tulikuwa hatukatizi tukija kuokota maembe chuo kikuu hahaha.

Dah maembe tu..mkuu au na kuchukua samaki..maana tulikuwa tunawaona watoto wanaokota embe na kuchukua samaki beach kidimbwi..ulikuwa mitaa gani..
 
Yani we acha tu.
Nilikuwa mtata mwisho.
TTCL mama alikuwa anafanya kazi, basi nakwambia twachukuana haooo...
Ni panda shuka...panda shuka.
Hapo niko drs la 3.
Tukitoka hapo twaenda Snow Cream.
Dereva wa home akitufata ye ndio akatuchukulie mabegi ya Dino shule,unayakumbuka?
Tahfif tumedokoa sana vipenseli, viufutio...

Yeah mabegi ya dino nayakumbuka yalikua classy enzi zile saaana...haha
 
Back
Top Bottom