Unakumbuka wanyonya damu mashuleni?

Unakumbuka wanyonya damu mashuleni?

Stori zalongi sana duh! tuliokuwa tunasoma shule za mbali unapita msituni unafika Shule roho uko mikononi, nilikua nakimbia kutoka nyumbani mpaka Shule

dah bush ilikuwa noma tupu, ukiona mtu kwenye kichaka kwa mbali unageuza mbio eti mumiani kajificha anangojea watu, unatimua hadi nywele zote utosini zinasimaa. ukiwa mtoto unatishika kwa urahisi sana
 
Umenikumbusha Forodhani Primary.
Enzi hzo tuko drs la 3.
Kuna gari flani la Red Cross liliingia pale shule kwa minajiri ya kugawa First Aid Kit kwa mwl mkuu Bw. Saiwad.
Sasa pata picha kilichotokea...afu sasa yule baba mhindi alikuwa amevaa gloves na nguo nyeupe, akaja moja kwa moja kule juu darasani.
Kama si busara za masista siku hiyo...sijui kama mngemjua Madame B.
Tulipagawa mpaka wengine tulizima chali.

Khaa@ madame B kumbe ni wa forodhani primary...unamkumbuka mwalimu chuma...mwalongo..mwalimu asenga...we ni la saba la mwaka gani
 
Last edited by a moderator:
Khaa@ madame B kumbe ni wa forodhani primary...unamkumbuka mwalimu chuma...mwalongo..mwalimu asenga...we ni la saba la mwaka gani

Chuma, Mwalongo, Asenga, Mushi, Kimathi...wote hao walimu wangu.
Sasa huko kwenye miaka ndio hatarishi mazee.
Ila mie mkubwa.
Wewe ni wa mwaka gani kwani?
 
Umesoma mlimani nini?maana dah msitu ulikuwa mkubwa..lazima tukimbizwe.

.......hahahaaa,mlimani primary school!!daahhhh,nyonya damu zilizingua sana mixer na komando yosso kule vichakani mabwawa saba na beach kidimbwi palikua hapapitiki enzi zile.
 
Yani ilikuwa tabu kweli..tulikuwa kama tunakatiza kipori lazima tuwe wengi pale sheli..maana dah wale wajinga walikuwa wanatuvizia kweli..unakumbuka mpaka mama mmoja wa kihaya alianzisha daladala konda yeye ndio kama unaogopa kukatisha kipori anatubeba..ukichelewa inakula kwako.

....ahhh,kulaaaleki!Mrs Rwiza yule anakaa sinza A,alikua anafundisha UDSM na mzee Rwiza ni mwalimu UDSM(prof).
 
Yeah !nyonya damu,vibwengo,chunusi!mbona tulifedheheka watundu wa miaka hiyo -yaani ukipigwa pini hiyo hujiulizi marambili wala hutaki ushahidi unatoka balu tu!
 
ngoja nikirudi itabidi tukumbushane pia enzi za sekeseke la tambaza
 
Asanteni wote mliochangia huu uzi. Nimecheka sana nikikumbuka Mumiani. Nakumbuka siku moja na wadogo zangu twatoka kanisani mitaa ya Ukonga, mzee mmoja alikuwa anaitwa BOGI (walikuwa wanasema ni mumiani - RIP ) akatuuliza njia ya kwenda FFU Ukonga iko wapi huku anatusogelea.

Wadogo zangu wakawa wanamuelekeza, nilistukia nimeanza Marathon, kutahamaki wadogo zangu wakanipita ktk hizo mbio. Tulikutana nyumbani umbali wa kama 2kms nakuanza kusimuliana.
 
Asanteni wote mliochangia huu uzi. Nimecheka sana nikikumbuka Mumiani. Nakumbuka siku moja na wadogo zangu twatoka mafundisho ya kumunio mitaa ya Ukonga, mzee mmoja alikuwa anaitwa BOGI (walikuwa wanasema ni mumiani - RIP ) akatuuliza njia ya kwenda FFU Ukonga iko wapi huku anatusogelea.

Wadogo zangu wakawa wanamuelekeza, nilistukia nimeanza Marathon, kutahamaki wadogo zangu wakanipita ktk hizo mbio. Tulikutana nyumbani umbali wa kama 2kms nakuanza kusimuliana.

...hebu pata picha mmekuwa wakubwa afu mnasimuliana.
Waweza kujiona bonge la zoba.
Utoto jamani...acheni upite tu.
 
Chuma, Mwalongo, Asenga, Mushi, Kimathi...wote hao walimu wangu.
Sasa huko kwenye miaka ndio hatarishi mazee.
Ila mie mkubwa.
Wewe ni wa mwaka gani kwani?
Nimeamini we born intown....it was a niiice school....full kipupwe cha bahari ya hindi...kwenye miaka hapo tupaache kwakwelii
 
.......hahahaaa,mlimani primary school!!daahhhh,nyonya damu zilizingua sana mixer na komando yosso kule vichakani mabwawa saba na beach kidimbwi palikua hapapitiki enzi zile.
Dah niko hoi kwa kucheka..unanikumbusha mbali watu walivyokuwa wanakimbizwa mabwawa saba..haaa beach kidimbwi lol jamani tumetoka mbali..
 
....ahhh,kulaaaleki!Mrs Rwiza yule anakaa sinza A,alikua anafundisha UDSM na mzee Rwiza ni mwalimu UDSM(prof).

Mh yule mama alituokoa kweli..maana jamaa walikuwa wanavizia kweli kipori ukiambiwa sasa hivi ndio eneo la mlimani city unaweza usiamni..
 
Issue ya nyonyadamu mpaka leo na utu uzima wangu baba wake mtu bado NAOGOPA! Kila nikiwaza hivi natetemeka sababu ile picha niliyokuwa napata kipindi kile balaa.

Kuna siku ilipita combi yenye king'ora karibu na primary skuli daaaaaah hakubaki mtu shule. Nilijikuta niko home.

Pia ukitaka shule ifungwe we sema Tambaza wanakuja!
 
Umenikumbusha Forodhani Primary.
Enzi hzo tuko drs la 3.
Kuna gari flani la Red Cross liliingia pale shule kwa minajiri ya kugawa First Aid Kit kwa mwl mkuu Bw. Saiwad.
Sasa pata picha kilichotokea...afu sasa yule baba mhindi alikuwa amevaa gloves na nguo nyeupe, akaja moja kwa moja kule juu darasani.
Kama si busara za masista siku hiyo...sijui kama mngemjua Madame B.
Tulipagawa mpaka wengine tulizima chali.

binafsi nikiwa darasa la kwanza ilitoke huo uvumi. na nlikuwa mdogo class nzima si kubanwa mlangoni.

ila lawama zangu nazielekeza kwa waalimu sikuwahi sikia.walimu wakitwambia kuwa hakuna kitu kama hicho
 
Last edited by a moderator:
Nimeamini we born intown....it was a niiice school....full kipupwe cha bahari ya hindi...kwenye miaka hapo tupaache kwakwelii

Umeona ee!
Shule ilikuwa ina raha ile.
Akina Babu Jing.a, Masudi, Mussa muuza chips na Sun-vita.
Unapakumbuka Snow-Cream?
Sa hvi imehamishiwa Upanga,near Upanga Pharmacy.
 
Acha kabisa Madame B utoto una mambo yake na ni raha sana.

Basi mie mwanangu akifanya jambo la kunikumbusha zamani...namwangaliaaaa, namwambia ungejua kote huko tumepita, wala usingejifanya mjanja.
 
Last edited by a moderator:
binafsi nikiwa darasa la kwanza ilitoke huo uvumi. na nlikuwa mdogo class nzima si kubanwa mlangoni.

ila lawama zangu nazielekeza kwa waalimu sikuwahi sikia.walimu wakitwambia kuwa hakuna kitu kama hicho

Hapo hakuna cha mwalimu wala teacher!
Nakumbuka mwl Mushi alikuwa mlangoni (maana yule mhindi aliingilia mlango mwingine)
tulimpiga tobo takatifu.
Afu ghorofani sasa.
Patamu hapo.
 
Dah! hii ni moja ya 'hoax' ambazo zilishika hatamu miaka hiyo tukiwa bado makinda...

Nakumbuka nikiwa Mbeya kuna jina la Msekwa(sio Pius Msekwa) lilikuwa maarufu sana...

Na kipindi kile mji haukuwa umejengwa sana kwani kulikuwa bado na ule uoto wa misitu ya mikaratusi...

Sasa ilikuwa inasemekana huyu bwana ni nyonya damu na anatembelea kibito chekundu na hakitoi mlio...

Suala la kwenda shule asubuhi na mapema au kurudi nyumbani kigiza kikiwa kimeingia ilikuwa tafrani sana...

Duuu!! Mkuu Watu8, hilo jina la Msekwa hata sisi tukiwa shule ya msingi ktk mkoa wa Kilimanjaro katikati ya miaka ya 80 lilikua linavuma sana kua ni mnyonya damu, na eti anatembelea Kibito Chekundu na ndani kuna madumu ya kuwekea damu, alafu kuna dogo mmoja tukiwa darasa la tano miaka ya 80 alikamatwa na watu akafungwa kamba na hao watu huku wakiendelea kusubiri wezao waje sijui kumfanya nini huyo dogo duu, basi dogo bahati yake tu wale jamaa sijui walijisahau nini akachoropoka na kamba zake akakimbia, alivyorudi nyumbani kwao wazazi wake wakakusanyika pamoja na majirani kwenda kuwatafuta hao waliosadikiwa kua ni mumiani, lakini walivyofika ktk hicho kiporu hawakuona mtu yoyote, basi kuazia siku hio hadi leo hicho kipori watu wanakiogopa sana, huyo dogo tumepoteana mda mrefu sana tangu tumalize shule ya msingi, ila nina dukuduku siku moja nikutane naye nimhoji kuhusu hiki kisa kilichomtokea.
 
Back
Top Bottom