Unakumbuka wanyonya damu mashuleni?

Unakumbuka wanyonya damu mashuleni?

Wale waliokuwepo Iringa miaka 80 kuna jamaa aliogopeka sana kwa tuhuma hizo alikuwa akifahamika kama Sekeni

Daaaaaaah ingawa nilikuwa mtoto lakn hilo jina nalikumbuka vizr sana tulikuwa tunajikusanya makundi makundi alfajiri ya saa kumi 7bu shule ilikuwa 7km halafu katkri hapo ni pori tupu bac viroho juu juu
 
Yeah !nyonya damu,vibwengo,chunusi!mbona tulifedheheka watundu wa miaka hiyo -yaani ukipigwa pini hiyo hujiulizi marambili wala hutaki ushahidi unatoka balu tu!

kwi kwi kwi.....kweli palikuwa hakuna kuuliza mara mbili.
 
Issue ya nyonyadamu mpaka leo na utu uzima wangu baba wake mtu bado NAOGOPA! Kila nikiwaza hivi natetemeka sababu ile picha niliyokuwa napata kipindi kile balaa.

Kuna siku ilipita combi yenye king'ora karibu na primary skuli daaaaaah hakubaki mtu shule. Nilijikuta niko home.

Pia ukitaka shule ifungwe we sema Tambaza wanakuja!

Tulikuwa tunapenda kwenda kucheza maeneo ya karibu na maeneo ya reli inapopita. Kikipita kiberenge hata mtu mzima(mkubwa) hutamwona maeneo hayo. Tulijua viberenge ni vya wanyonya damu.
 
Hivi hadi leo sikuwahi kusikia serikali ikitolea ufafanuzi wa hili suala la mumiani, maana lilivuma sana hasa miaka ya 80 na mpaka leo kuna baadhi ya watu walikua wananyooshewa vidole kua ni wanyonya damu wapo mitaani,
 
Hahahaaaa.....Ware wa kure kwetu enzi za primary, ilikuwa inasemekana kuwa kuna watu wanaiba watoto na kwenda kutoa KAFARA migodin...

Enzi hizo alivuma mzee mmoja kwa jina MALEMBERA ambaye alikuwa anamiliki mashimo kadhaa ya Dhahabu NYAMONGO, Sasa wakawa wanasema huyo mzee alikuwa akipiga hizo issue....Basi mtoto ukitishiwa tu... "Malembera huyo yuaja...mbiooooooo, au hata kama kuna kitu umezuiwa kufanya hutofanya ukihofia utapelekwa kwa huyo Mzee.....

Aione: Think pad, Mwita Maranya na platozoom...
 
Last edited by a moderator:
duu! wayback kongwa s/m waliitwa chinja chinja ila gari za wanyonya damu,uzinduz wa theatre hospital eti watu walipotea!
 
Umenikumbusha mbali. Kuna siku tulikuwa tunachezea kwa jirani, mara mmoja wetu akasema wanyonya damu hao.. Basi tulikimbia mbio mmoja wetu alikanyaga ndizi sukari iliyoiva alikula mweleka wa nguvu na hakuna aliyemjali, kila mmoja alikimbia kuokoa maisha yake. Kesho yake ndo tukaja kuambiwa kumbe aliumia vibaya. Nilijua hiyo ishu ilikuwa ni kwetu tu kumbe ilikuwa ni nchi nzima??? Sijui nani alikuwa akisambaza hii propaganda.
 
Heheheheh usinikumbushe
Wakati niko darasa la pili
Kida lilikuja gari jekundu sijui nani akatangaza kuwa ni la wanyonya damu

Ilikuwa patashika shule nzima

Hahaaaaa aiseee, umenikusha mbali mi nakumbuka kipindi hicho tulikwenda likizo kumsalimia bibi, sasa watoto wa rika langu pale nyumbani kwa bibi wote kwa pamoja tukaambiwa tukatafute kuni.

Tulienda umbali kama kwa km 7 hivi lakini hatukuwa mbali sana na baraabara basi kwa mbali tu mwungurumo wa gari uliposikika kila mmoja wa wale wenzangu wali-pay anttention kuangalia ni mlio wa gari gani kwa mbali kidogo tuliona gari rangi nyekundu likiwa linazidi kusonga.

Mara kidogo tukiwa mita kama mia Moja kutoka barabarani tuliona gari likipunguza mwendo jamani kilichotokea hapo nilijikuta nipo mwenyewe sehemu ile wale wenzangu wakiwaa wana-shout wakiita jina langu na kusema kimbia wanyonya damu hao karibu kilaa mmoja alijitahidi kuu-shout kuwa nikimbie wanyonya damu.

Wale jamaa waliuliza tu njia inayoelekea sehemu fulani nikawaelekeza kuwa ndiyo ile wanyooshe moja kwa moja.

wakati huo wale ndugu zangu yaani wa rika langu walitokomea maporini na nakumbuka tulikutana kwa bibi saa Moja jioni yaani masaa kama 7 ya kupoteana!

usiku sasa ndo wakaanza kunipa somo kuwa nnikiona magari mekundu au yenye msalaba mwekundu nikimbie sana maana ni ya wanyonya damu. walisistiza kuwa yale malorry aina ya fiat ni hataari zaidi maana wasomali wakikunyonya damu wanakuyonya yote hawakuachi na hhata kidogo ya kuufiksiha nyumbani!
aiseee acheni kabisa mnenikumbusha kitambo mno!

Zamani jamani duh!
 
Hahahaaaa.....Ware wa kure kwetu enzi za primary, ilikuwa inasemekana kuwa kuna watu wanaiba watoto na kwenda kutoa KAFARA migodin...

Enzi hizo alivuma mzee mmoja kwa jina MALEMBERA ambaye alikuwa anamiliki mashimo kadhaa ya Dhahabu NYAMONGO, Sasa wakawa wanasema huyo mzee alikuwa akipiga hizo issue....Basi mtoto ukitishiwa tu... "Malembera huyo yuaja...mbiooooooo, au hata kama kuna kitu umezuiwa kufanya hutofanya ukihofia utapelekwa kwa huyo Mzee.....

Aione: Think pad, Mwita Maranya na platozoom...

Malembera alivuma si kidogo, nasikia kwenye harusi yeye alikuwa wa mwisho kutaja zawadi kwa Wanaharusi, ilikuwa balaa. Kuna wakati aliweka rekodi ya mtu aliyeuza dhahabu nyingi kwa NBC Bank.

Ila hivi sasa nasikia yuko hoi kifedha!!
 
ilikuwa ni kampeni ya uchangiaji damu , lakini ilikumbwa na mizengwe mingi si wasomi hata wakulima ambao hawakuamini kama damu inaweza changiwa , wakiamini kama unatafuta damu basi hata mtu unaweza kuua na iliaminika hivyo , mzee wangu alikuwa msomi lakini aliwahi kuamini hivyo ,mpango huu ulifeli vibaya kwa nilivyosikia, hiyo ndiyo tz ya nyerere enzi hizo full comedy
 
Umeona ee!
Shule ilikuwa ina raha ile.
Akina Babu Jing.a, Masudi, Mussa muuza chips na Sun-vita.
Unapakumbuka Snow-Cream?
Sa hvi imehamishiwa Upanga,near Upanga Pharmacy.

Haha nawakumbuka..masudi kaniozesha meno sitosahau nikifika tu getin ni chocolate na biscut..chips za mausa pia...haha me nilikua napendaje shingo zao za kukaanga...chips ndani ya mfuko wa karatas mweupe .snow cream yap naikumbuka..umesahau tahfif tunaenda nunua kalamu..vifuto..pen za kubonyeza na kunukia aiseee mpk leo ipo pale palee...yn tulienjoy jaman...yn km umjini watu tumeufaidi haswaaa
 
Mama alikuwa ananiuliza hao wanyonya damu,wanakuja kila siku maana ata kama kuna mwalimu mlangu autoshi tunavyokimbia..watoto wetu haya mambo wanayakosa mbona...
Hahahahaha umenikumbusha mbali sana . Nimewahi kujiuliza hivi kwanini tulikua tunatishwa vile lol.
 
Umenikumbusha mbali. Kuna siku tulikuwa tunachezea kwa jirani, mara mmoja wetu akasema wanyonya damu hao.. Basi tulikimbia mbio mmoja wetu alikanyaga ndizi sukari iliyoiva alikula mweleka wa nguvu na hakuna aliyemjali, kila mmoja alikimbia kuokoa maisha yake. Kesho yake ndo tukaja kuambiwa kumbe aliumia vibaya. Nilijua hiyo ishu ilikuwa ni kwetu tu kumbe ilikuwa ni nchi nzima??? Sijui nani alikuwa akisambaza hii propaganda.
Pia unakumbuka ukimuona mlemavu ngozi kwa mbali unatemea mate kifuani
 
Yeah !nyonya damu,vibwengo,chunusi!mbona tulifedheheka watundu wa miaka hiyo -yaani ukipigwa pini hiyo hujiulizi marambili wala hutaki ushahidi unatoka balu tu!
Hahahahahahahaha yaani ukiona gari nyeupe inaendeshwa pole pole karibu na eneo la shule halafu atokee mtu aseme mkiwa darasani kwamba gari ya wanyonya damu aka mumiani ileee alikua habaki mtu hapo.
 
Umenikumbusha mbali kweli yani..wanyonya damu hao tulikua tunadanganyana eti kuna gari moja la mzee flani lina mirija chini ya viti ukikaa tu anabonyeza alaf unanyonywa damu anakutupa..zamani hzo la pili cjui la tatu hukooo
 
Rest in Peace my "fiancee“ wa kitoto toto....Mary Abonike,nikikumbuka haya mambo ya chinjachinja sijui nyonya damu namkumbuka sana Mary wangu,1991 tukiwa Mwadui “A“ Primary School,tunapita pembezeni mwa barabara ya boidi,mara mwanafunzi mmoja akatushitua kuwa mnyonya damu wa kijiji cha Utemini anakuja...katika harakati za kukimbia tukajichomeka kwenye barabar...Gari aina ya Peugot ukatupitia...nilivunjika mkono na mguu...lakini mwenzangu Mary alifia Hospitali ya Misheni pale Mipa...
Alikuwa jirani na "mchumba" wangu wa kombolela na mchezo wa chekecha...darasani hadi kanisani pamoja..tukapewa kipaimara na Askofu Castor Sekwa(R.I.P) Parokia ya Msalaba Mtakatifu-Mwadui...sijawahi kumsahau wala kulisahau tukio la kumkimbia Mnyonya damu...picha za kipaimara na mazishi ninazo...hunipa kumbukumbu ya rafiki wa utotoni niliompoteza kwa vitisho ambavyo leo nakuja kujua havikuwepo....R.I.P MARY ABONIKE

Pole sana mkuu barafu
 
Last edited by a moderator:
Haha nawakumbuka..masudi kaniozesha meno sitosahau nikifika tu getin ni chocolate na biscut..chips za mausa pia...haha me nilikua napendaje shingo zao za kukaanga...chips ndani ya mfuko wa karatas mweupe .snow cream yap naikumbuka..umesahau tahfif tunaenda nunua kalamu..vifuto..pen za kubonyeza na kunukia aiseee mpk leo ipo pale palee...yn tulienjoy jaman...yn km umjini watu tumeufaidi haswaaa

Umeona ee!
Mie yule mlinzi babu wa pale Tahfif alikuwa ananikeraga na mikwara bubu yake.
Cathedral Book Shop pale.
Nakumbuka siku moja wakati wa mapumziko tulienda pale TTCL kuchezea lifti, tusikwame nini, tulilia...ilibidi mwl mkuu Fadhil aje kututambua kama sisi ni wnfnz wake baada ya kunasuliwa.
Tulipofika skuli tukaambiwa tunaitiwa nyonya damu ili watunyonye...mama weee...nilivyomponyoka mwl ni mbio mpaka ofsn kwa dad (r.i.p).
Jamani utoto...hasa wa kimjini, raha sana.
 
Hahahaaa! Nimeipenda hii mada,mi kuna siku nilibadilisha njia mana kuna mwenzetu mmoja alizusha kwenye kanjia tulipokuwa tunapita kuna manyonya damu.. Aisee! Ilikuwa inatugharimu sana!
 
Na ulikuwa ukikimbia unaambiwa usiangalie nyuma, kioo kitakuvuta. Basi dah ni mbio tu mpaka nyumbani kitandani.

Hahaha ilinitesa sana hii kitu uzuri wake kutoka xul kijitonyama primary school hadi hom hapakuwa mbali sana ni mwendo wa robo km so habari zilikua zikivuma oh mara wako shule ya makumbusho au mugabe sinza ni nduki hakuna kuangalia nyuma haha.
 
Back
Top Bottom