Unakumbuka Mchezo gani ukiwa Mtoto?

Makamura

JF-Expert Member
May 19, 2022
352
547
Nikiwa mtoto bhana, Nilikuwa napenda sana michezo, moja ya mchezo ni Kuendesha lingi, Kuwinda ndege kwa manati.

Kuna ile Unatengeneza gari la mbao na mipira inakuwa kama spring na unaweka kamba mbele na mti inakata hadi kona, na kukata malapa (Kanda Mbili) kama matairi

Kingine bhana Niliwahi kwenda kuoga kwenye bwawa kubwa mnoo ambalo kingo zake ni za mfinyanzi, hivyo mvua ikinyesha au zikilowa huwezi kutoka, na bwawa lilikuwa kubwa mnoo

Wewe unakumbuka mchezo gani?
Young-South-African-children-play-with-wheel-rims.jpg
 
Kuchimba udongo na kutengeneza watoto.

Kwenda dukani kuiba vitu (mchele) na kujipikilisha kwenye vikopo.
Kuna siku niliiba dagaa nikakimbia toilet daaaah nilifatwa hadi toi yani
Ukucheza baba na mama..??
 
Baiskeli ya miti ya miguu mitatu, hii hata maza alikuwa anaipenda maana ilikuwa inasaidia kubeba kuni na mahindi.

Kuna baiskeli ya miguu miwili, hii nilikuwa napaki kwa rafiki yangu jirani. Ilikuwa ikionekana nyumbani inafyekwa panga maana haikuwa na msaada zaidi ya kuchezea na kupoteza muda.
 
Nikiwa mtoto bhana, Nilikuwa napenda sana michezo, moja ya mchezo ni Kuendesha lingi, Kuwinda ndege kwa manati.

Kuna ile Unatengeneza gari la mbao na mipira inakuwa kama spring na unaweka kamba mbele na mti inakata hadi kona, na kukata malapa (Kanda Mbili) kama matairi

Kingine bhana Niliwahi kwenda kuoga kwenye bwawa kubwa mnoo ambalo kingo zake ni za mfinyanzi, hivyo mvua ikinyesha au zikilowa huwezi kutoka, na bwawa lilikuwa kubwa mnoo

Wewe unakumbuka mchezo gani?
View attachment 2918070
Kuwinda ndege kwa manati ni mchezo au ni kutafuta mboga ya ugali?
 
Kombolela .... unakaa unasubiria mwenzio aja akapige debe mkimbie kujificha tenaa.... kumbe wawili hao walikoenda kujificha wanacheza mchezo mwingine tena wa tia maji ...baba na mama
 
Game and watch, video games (PS), one touch, last card, albastini, snake and ladder, monopoly infact utoto ulikua murua kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom