Hakuna aliyekulazimisha ung'ang'anie.
Ila pia usifanye mapungufu yako kuwa sababu ya kuwashawishi watu wasiingie kwenye vitu usivyoviweza.
Kuna watu wengine hawataki vitu rahisi wanataka fani ambazo ukiziweza vizuri na kuwa 1 out 1,000 unafanya vizuri sana.
Inawezekana hoja yako kimsingi ina mashiko, lakini umeshindwa kutoa sababu za maana kushawishi, umeonesha mapungufu yako tu.
Ungesema msisomee kuenda kuwa walimu kwa sababu fani ya ualimu inaenda kutoweka duniani watu watajifunza kwa AI, hapo ungekuwa una hoja ya msingi kwa sababu fani nzima ingeonekana haina future.
Sasa wewe unalalamikia ualimu kwa sababu wewe mwenyewe ume fail, you are a statistical failure, not an imminent failure, wakati kuna watu wanafundisha wanapanda mpaka kufundisha vyuoni wanachagua wafundishe nchi gani, hapo ukilalamikia fani unajionesha una a failure of imagination tu.